Njoo, Unifuate
Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo


“Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Yesu akiwafundisha watu

Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo

Umeitwa na Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi. Umetengwa katika wito huu kwa mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu. Hata kama wewe sio mwalimu mwenye uzoefu, unapoishi kwa kustahili, kusali kila siku, na kujifunza maandiko, Baba wa Mbinguni atakuzawadia usahwishi na nguvu za Roho Mtakatifu ili kukusaidia kufanikiwa(ona 2Nefi 33:1).

Wale waliowekwa chini ya uangalizi wako ni watoto wa Baba wa mbinguni, na Yeye anajua kile wanachohitaji na jinsi ya kuwafikia vyema. Kupitia kwa Roho Mtakatifu, Mungu atakuongoza wakati wa maandalizi yako na wakati unapofundisha. Atakufunulia kile unachopaswa kusema na unachopaswa kufanya (ona 2 Nefi 32:5).

Dhumuni la muhimu la kufundisha na kujifunza injili ni kubadili maisha. Lengo lako kama mwalimu ni kuwasaidia wale unaowafundisha kufanya kila wawezacho kuwa waongofu katika injili ya Yesu Kristo—juhudi ambazo hupita zaidi muda wa darasani. Waalike wale unaowafundisha kushiriki kwa dhati katika kujifunza kwao wenyewe kanuni na mafundisho ya Yesu Kristo na kutenda yale wanayojifunza. Wahimize kufanya kujifunza kwao binafsi na familia nje ya darasa kuwa lengo la msingi la kujifunza kwao injili. Wanapotenda kwa imani kwa kujifunza kama watu binafsi na familia, watamwalika Roho katika maisha yao na ni Roho ambaye ataleta uongofu wa kweli. Kila kitu ufanyacho kama mwalimu hakina budi kuelekeza katika lengo hili takatifu.

Fundisha tu mafundisho ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo kama yanavyopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho. Mafundisho safi—ya milele, ukweli usiobadilika uliofundishwa na Mungu na watumishi Wake—humwalika Roho na una uwezo wa kubadili maisha.

Wito wa kufundisha ni wajibu mtakatifu, na ni kawaida kuhisi kuzidiwa wakati mwingine. Lakini kumbuka kwamba Baba yako wa Mbinguni alikuita, na Yeye hatakuacha kamwe Hii ni kazi ya Bwana na unapohudumu “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu” (M&M 4:2), Ataongeza uweza wako, karama na vipaji na huduma yako itabariki maisha ya wale unaowafundisha.