Njoo, Unifuate
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Nyenzo za Zaida

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kutohoa shughuli zozote kutoka kwenye nyenzo hii kwa matumizi katika darasa lako la Shule ya Jumapili. Kama washiriki wa darasa wametumia shughuli hizi katika kujifunza kwao injili binafsi au kama familia, wahimize washiriki kushiriki uzoefu na umaizi wao.

Majarida ya Kanisa

Majarida ya New Era, Ensign,, na Liahona yanatoa makala na habari za ziada ambazo zinaweza kuongezea kanuni ambazo unafundisha kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kama nyongeza kwa matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, unaweza kupata nyimbo nyingi na nyimbo za watoto zilizorekodiwa kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika LDS Music na LDS Media Library app.

Maktaba ya Kazi za Sanaa

Sanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zilizopo katika Kitabu cha Mormoni. Tembelea medialibrary.ChurchofJesusChrist.org kupitia mkusanyiko wa nyenzo za sanaa, ikijumuisha mkusanyiko wa video za Kitabu cha Mormoni, ambazo zinaonyesha matukio katika Kitabu cha Mormoni. Nyenzo za vyombo vya habari pia zinapatikana kwenye LDS Media Library app.

Sanaa ya Injili

Sanaa inaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili, katika medialibrary.ChurchofJesusChrist.org, na kwenye LDS Music na LDS Media Library apps.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya kiada vya seminari na chuo vinatoa chimbuko la kihistoria na fasili ya mafundisho kwa kanuni zinazopatikana katika maandiko. Vinaweza pia kuchochea mawazo kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili.

Mada za Injili

Kwenye topics.ChurchofJesusChrist.org unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo za kusaidia kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa majibu ya kina ya maswali ya injili na ya kihistoria.

Kweli kwa Imani

Nyenzo hii inatoa maelezo rahisi ya mada za injili, zilizoorodheshwa kwa mpangilio wa kialfabeti

Hubiri Injili Yangu

Mwongozo huu wa wamisionari hutoa maelezo ya jumla ya kanuni za msingi za injili.

Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana

Nyenzo hii inatoa muhtasari wa viwango vya Kanisa ambavyo vinaweza kutusaidia kubakia wenye kustahiki baraka za Bwana. Fikiria kuirejelea mara kwa mara, hasa ikiwa unawafundisha vijana.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Nyenzo hii inaweza kukusaidia kujifunza na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kufanyiwa kazi katika mikutano ya baraza la walimu.

Jedwali likionyesha Maktaba ya Injili