Mafundisho na Maagano 2021
Februari 15–21. Mafundisho na Maagano 14–17: “Kusimama kama Shahidi”


“Februari 15–21. Mafundisho na Maagano 14–17: ‘Kusimama kama Shahidi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 15–21. Mafundisho na Maagano 14–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Joseph Smith na Mashahidi Watatu wakisali pamoja wakiwa wamepiga magoti

Februari 15–21

Mafundisho na Maagano 14–17

“Kusimama kama Shahidi”

Fikiria kuhusu mafundisho na matukio yaliyoelezewa katika Mafundisho na Maagano 14–17. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwatia msukumo watu unaowafundisha “kusimama kama shahidi wa mambo [haya]”? (Mafundisho na Maagano 14:8).

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ni nini washiriki wa darasa lako walikiona kuwa muhimu katika kujifunza maandiko kwao binafsi na kama familia? Labda ungeweza kulialika darasa kushiriki umaizi mmoja kuhusu kushiriki katika kazi ya Bwana kutoka kila sehemu katika Mafundisho na Maagano 14–17.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 14–16.

Mwokozi anatualika tushiriki katika kazi Yake.

  • Washiriki wa darasa wanafahamu nini kuhusu familia ya Whitmer? (ona Watakatifu, 1:68–69). Yaweza kuwa msaada kwao kuorodhesha ubaoni baadhi ya kweli kuhusu akina Whitmer. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinatusaidia kuelewa vyema ushauri wa Bwana kwa akina Whitmer katika sehemu za 14–16? Kwa mfano, ni kwa nini Bwana anaweza kuwa alifananisha kazi yake na kuvuna shambani?

  • Ili kuwapa nafasi washiriki wa darasa kushiriki mawazo yao kuhusu kuchangia katika kazi ya Bwana, ungeweza kuandika marejeleo yafuatayo ubaoni: Mafundisho na Maagano 14:1; 14:2–4; 14:5, 8; 14:6–7; 14:9–11; 15:6. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mojawapo ya vifungu hivi vya maandiko katika jozi na kujadiliana kile wanachojifunza kuhusu kazi ya Bwana. Baadhi ya jozi zinaweza kushiriki na darasa kile walichojadiliana.

  • Waalike washiriki wa darasa washiriki uzoefu wao walipowasaidia wengine kumkaribia Mwokozi, ikijumuisha kama wamisionari wa muda au wa huduma na kupitia kuhudumia. Ni kwa jinsi gani wameshuhudia maneno ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 15:6 na 16:6 yakitimizwa maishani mwao? Tunajifunza nini kutoka kwenye sehemu hizi ambacho kitatusaidia kujitayarisha kushiriki injili?

    Picha
    wafanyakazi shambani wakivuna ngano

    Kielelezo cha wafanyakazi wa shamba la ngano na Greg Newbold

Mafundisho na Maagano 17

Tunaweza kubaki waaminifu kwa kile tunachokijua, hata kama wengine watatukataa.

  • Kwa nini Bwana alitoa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mawazo ambayo yaliwajia walipokuwa wakisoma Mafundisho na Maagano 17. Mawazo ya ziada yanaweza kupatikana katika maandiko yaliyorejelewa katika kichwa cha habari cha sehemu ya 17 au katika “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu,” unaopatikana mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni. Ni kwa namna ipi ushuhuda wa wale Mashahidi Watatu umeathiri ushuhuda wetu wa Kitabu cha Mormoni?

  • Hata kama hatujawaona malaika au kuyagusa mabamba ya dhahabu, bado tunaweza kushuhudia juu ya Kitabu cha Mormoni. Ni nini washiriki wa darasa wanapata katika sehemu ya 17 (ikijumuisha kichwa cha habari cha sehemu hiyo) ambacho wanafikiria kinatumika kwao? Kama mtu angekuuliza kwa nini tunaamini Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, ungesema nini? Labda washiriki wa darasa wanaweza kuandika jibu fupi, na unaweza kuwaalika baadhi yao kushiriki kile ambacho wameandika. Nukuu kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa kushuhudia Kitabu cha Mormoni.

  • Inaweza kuwa ya kutia msukumo kuwa na mshiriki wa darasa akishiriki uzoefu wa mashahidi wengine wa mabamba ya dhahabu (ona “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” katika Kitabu cha Mormoni na historia ya Mary Whitmer katika Watakatifu, 1:70–71). Je, tunajifunza nini kutoka kwenye uzoefu wa mashahidi hawa?

  • Unaweza shiriki sehemu fulani za video “A Day for the Eternities” (ChurchofJesusChrist.org) kama sehemu ya mjadala wenu kuhusu mashahidi wa Kitabu cha Mormoni (sehemu kuhusu Mashahidi Watatu inaanza karibia dakika ya 15:00).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kushiriki ushuhuda wetu juu ya Kitabu cha Mormoni.

Rais Ezra Taft Benson alitoa mwaliko ufuatao kwa washiriki wa Kanisa mnamo mwaka wa 1988.

“Kitabu cha Mormoni ni kifaa ambacho Mungu aliunda ‘kifagie dunia kama vile kwa gharika, ili kuwakusanya wateule [Wake].’ (Musa 7:62.) Juzuu hii takatifu ya maandiko inahitaji kuwa kiini zaidi katika mahubiri yetu, kufundisha kwetu, na kazi yetu ya umisionari.

“… Katika zama hizi za vyombo vya habari vya kielektroniki na usambazaji mkubwa wa maneno yaliyochapishwa, Mungu atatuwajibisha kama sasa hatutakichukulia Kitabu cha Mormoni kwa umuhimu mkubwa.

“Tunacho Kitabu cha Mormoni, tunao waumini, tunao wamisionari, tunazo rasilimali, na ulimwengu unahitaji. Wakati ni sasa!

“Kaka zangu na dada zangu wapendwa, bado hatufahamu vizuri nguvu za Kitabu cha Mormoni, au wajibu mtakatifu ambao lazima kitimize, wala kiwango ambacho ni lazima kipelekwe” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson [2014], 143–44).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali ambayo yanaalika ushuhuda. Swali lenye msukumo linaweza kuwa njia ya nguvu ya kumualika Roho. Kwa mfano, wakati unapofundisha Mafundisho na Maagano 14:9, unaweza kuuliza swali kama “Je, Umekuja kujua kwa namna gani kwamba Yesu Kristo ni ‘nuru ambayo haiwezi kufichika gizani’?” (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 32.)

Chapisha