Mafundisho na Maagano 2021
Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18–19: “Thamani ya Nafsi Ni Kuu”


“Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18-19: ‘Thamani ya Nafsi Ni Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
shamba la Martin Harris

Shamba la Martin Harris na Al Rounds

Februari 22–28

Mafundisho na Maagano 18–19

“Thamani ya Nafsi Ni Kuu”

Ni kupitia tu kwa Roho Mtakatifu moyo wa mtu hubadilika. Rais Henry B. Eyring alifundisha, “Kama utafundisha Kanuni za Injili, Roho Mtakatifu atakuja” (“Mazungumzo na Mzee Richard G. Scott na Mzee Henry B. Eyring” [matangazo kupitia satelaiti ya mafunzo ya Mfumo wa Kielimu ya Kanisa, Ago. 11, 2003]).

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe washiriki wa darasa washiriki uzoefu wao wa maandiko, someni pamoja Mafundisho na Maagano 18:34–36. Waalike washiriki wa darasa washiriki mstari waliousoma wiki hii na ndani yake wakaitambua sauti ya Bwana.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 18:10–16; 19:15–20, 39–41

Bwana anafurahia wakati tunapotubu.

Mafundisho na Maagano 18:10–16

“Thamani ya nafsi ni kubwa machoni mwa Mungu.”

  • Unawezaje kuwasidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi kila mmoja wetu ana thamani machoni mwa Mungu? Pengine wanaweza wakasoma Mafundisho na Maagano 18:10–16 na kushiriki uzoefu ambao kupitia huo waliweza kuelewa thamani yao kwa Mungu. Je, ni kwa jinsi gani mistari hii huathiri jinsi tunavyojitambua sisi wenyewe? watu wengine? Ni kwa jinsi gani Mungu hutuonyesha kwamba sisi ni wenye thamani kubwa Kwake?

    Picha
    Yesu akiwa amembeba mvulana mdogo

    Thamani ya Nafsi, na Liz Lemon Swindle

Mafundisho na Maagano 19:15–19

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili ya wanadamu wote.

  • Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuhisi ushuhuda wa Roho Mtakatifu wanapotafakari maelezo ya Mwokozi Mwenyewe kuhusu mateso Yake ya upatanisho? (Mafundisho na Maagano 19:15–19). Pengine ungeweza kumualika mtu fulani aimbe wimbo wa kanisa aupendao kuhusu Mwokozi. Waweza pia kuonyesha picha ya Mwokozi na kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mistari ya 15–19; kisha wanaweza kuandika mawazo na hisia zao. (Maneno ya Mzee D. Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada” pia yanaweza kuongeza uelewa wa washiriki wa darasa kuhusu mateso ya Mwokozi.) Sentensi kama hii ubaoni inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari: Nina shukrani kwa ajili ya Upatanisho wa Yesu Kristo kwa sababu … Washiriki wachache wa darasa wanaweza kuwa tayari kushiriki walichoandika na kutoa shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Mafundisho na Maagano 19:16–26, 34–41

Kufanya mapenzi ya Mungu mara nyingi huhitaji dhabihu.

  • Washiriki wa darasa wanapokumbana na hali ambapo inawahitaji kufanya dhabihu kwa ajili ya injili, inaweza kuwa ya kutia moyo kwao kujifunza kuhusu dhabihu ambayo Martin Harris alifanya ili Kitabu cha Mormoni kiweze kuchapishwa. Pengine unaweza kumwalika mtu fulani aje darasani akiwa amejitayarisha kuzungumzia juu ya uamuzi wa Martin Harris kuweka rehani shamba lake ili alipie uchapishaji wa Kitabu cha Mormoni (ona Watakatifu, 1:76–78). Ni mistari ipi kutoka sehemu ya 19 inaweza kuwa ilimsaidia kufanya uamuzi huu? Unaweza kutaka kuwaalika washiriki wa darasa washiriki jinsi Kitabu cha Mormoni kimewabariki na jinsi walivyo na shukrani kwa ajili ya dhabihu ya Martin Harris na kwa ajili ya wengine ambao walitoa dhabihu ili kitabu kiweze kuchapishwa.

  • Labda mtu fulani katika darasa angeweza kushiriki dhabihu ambayo amefanya kwa ajili ya Bwana. Hii inaweza kuwasababisha washiriki wa darasa kufikiri kuhusu utayari wao wa kutoa dhabihu? Wahimize washiriki kitu chochote watakachopata kutoka Mafundisho na Maagano 19 ambacho kinawatia moyo kutoa dhabihu ili watimize mapenzi ya Mungu (ona hasa mistari ya 16–26, 34–41).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Gharama ya upendo wa Mungu.

Tukirejelea Mafundisho na Maagano 19:18, Mzee D. Todd Christofferson alisema: “Hebu tutafakari gharama ya upendo wa Mungu wenye thamani. … Mateso yake pale Gethsemani na pale msalabani yalikuwa makubwa sana kuliko yale ambayo mwanadamu katika mwili wenye kufa anaweza kuyastahamili. Hata hivyo, kwa sababu ya upendo Wake kwa Baba Yake na kwetu sisi, Yeye alivumilia, na kama matokeo yake, anaweza kutupa sisi maisha yote yasiyo na mwisho na uzima wa milele” (“Kaeni Katika Pendo Langu,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 50).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Unda mazingira ambayo yanamwalika Roho. Kuna njia nyingi unaweza kumwalika Roho katika darasa lako. Muziki unaotangulia unaweza kuhimiza unyenyekevu. Maonyesho ya upendo na ushuhuda vinaweza kuleta mazingira, mazuri ya kiroho. (Ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi, 15.)

Chapisha