“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22: ‘Kukua kwa Kanisa la Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Machi 1–7
Mafundisho na Maagano 20–22
“Kukua kwa Kanisa la Kristo”
Andika misukumo yako ya kiroho unapojifunza Mafundisho na Maagano 20–22. Baadhi ya misukumo hii inaweza kukuelekeza kwa mawazo ambayo yatakusaidia wakati unapofundisha.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wakati wa kujifunza kwao nyumbani, washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamepata umaizi kuhusu baraka za kuwa na Kanisa la Kweli ulimwenguni. Waalike kushiriki kifungu kutoka kwenye sehemu hizi ambacho kinaonyesha kwa nini wana shukrani Kanisa lilirejeshwa.
Fundisha Mafundisho
Kanisa la Yesu Kristo limerejeshwa.
-
Washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kujifunza mifanano kati ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na Kanisa ambalo Kristo alianzisha siku za kale. Unaweza kuchora ubaoni jedwali lenye safu nne zinazotambulika Mafundisho, Ibada, Mamlaka ya Ukuhani, na Manabii. Ungeweza kutoa marejeleo yafuatayo kuhusu Kanisa la Kristo katika siku za kale: Mathayo 16:15–19; Yohana 7:16–17; Waefeso 2:19–22; 3 Nefii 11:23–26; Moroni 4–5. Washiriki wa darasa wangeweza kutambua kile ambacho kila kifungu kinafundisha kuhusu Kanisa la Kristo na waandike rejeleo katika safu inayofaa ubaoni. (Baadhi ya marejeleo yanaweza kutumika kwa zaidi ya safu moja.) Wanaweza kufanya sawa na hivyo kwa marejeleo yafuatayo kuhusu Kanisa la Kristo lililorejeshwa: Mafundisho na Maagano 20:17–25, 60, 72–79; 21:1–2. Je, unajifunza nini kuhusu Urejesho wa Kanisa la Kristo kutoka katika mlingano huu?
Mafundisho na Maagano 20:37, 75–79; 22
Ibada takatifu hutusaidia kuwa kama Mwokozi.
-
Wape washiriki wa darasa muda wajifunze masharti ya ubatizo yaliyoelezewa katika Mafundisho na Maagano 20:37, na uwaombe watafakari maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani masharti haya yanatusaidia kujitayarisha kwa ajili ya kubatizwa katika Kanisa la Bwana? Inamaanisha nini kujichukulia jina la Kristo juu yetu? (ona Mosia 5:5–12). Ni nini hukusaidia kudumisha “dhamira ya kumtumikia [Yesu Kristo] hadi mwisho”?
-
Ni nini sehemu ya 22 inafundisha kuhusu ubatizo? Waombe washiriki wa darasa kufikiria wana rafiki ambaye amebatizwa katika kanisa tofauti. Wanaweza kusoma sehemu hii ili wapate ushauri wa kumsaidia rafiki aweze kuelewa kwa nini kubatizwa katika Kanisa la Mwokozi lililorejeshwa ni muhimu. Washiriki wa darasa wanaweza kuigiza mpangilio huu kama darasa au katika jozi.
-
Someni Mafundisho na Maagano 20:75–79 kwa pamoja, na uwaalike washiriki wa darasa wafikirie kile mistari hii inafundisha kuhusu Mwokozi na uwezo Wake katika maisha yetu. Ni maneno au virai gani vinajitokeza sana wakati tunaposoma sala za sakramenti? Kwa nini ni muhimu kupokea sakramenti kila wiki?
Mafundisho na Maagano 20:38–60
Huduma ya ukuhani hubariki washiriki wa Kanisa na familia zao.
-
Maelezo ya wajibu wa ukuhani katika Mafundisho na Maagano 20:38–60 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kupanua uelewa wao wa huduma ya ukuhani. Pengine ungeweza kuwaalika wafikirie kwamba rafiki au mwanafamilia aliyebatizwa hivi karibuni anakaribia kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani. Watatumiaje mistari hii kumsaidia kuelewa wajibu wake? Ni mifano ipi wangeshiriki ili kumsaidia aelewe jinsi kutimiza wajibu huo kunaweza kukamsaidia kuwa kama Yesu Kristo? Labda wangeweza kuigiza mazungumzo haya.
Kwa kuongezea, wanawezaje kutumia mistari hii kumsaidia dada mgeni aliyebatizwa aone jinsi anavyoweza kuchangia katika kazi iliyoelezwa hapa? (Kauli katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kusaidia.)
Tunabarikiwa wakati tunapopokea neno la Bwana kupitia nabii Wake.
-
Mafundisho na Maagano 21 ina kauli zenye nguvu kuhusu kumfuata nabii wa Bwana. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari na kujadili kauli hizi, waombe wachunguze mistari ya 4–7 kwa ajili ya kirai ambacho wangependa kuelewa vizuri zaidi na kuandika kirai hicho ubaoni. Chagua baadhi ya virai, na mjadiliane kama darasa kile vinaweza kuwa vinamaanisha. Virai hivi vinatufundisha nini kuhusu kumfuata nabii wa Bwana?
Nyenzo za Ziada
Sote tunafanya kazi kwa nguvu za ukuhani.
“Wanaume hutawazwa katika ofisi za ukuhani, huku wote wake kwa waume wanaalikwa kushiriki nguvu na baraka za ukuhani katika maisha yao. …
“… [Wanawake] huubiri na kusali katika mikutano, wako katika nafasi nyingi za uongozi na kutoa huduma, wanashiriki katika mabaraza ya ukuhani katika maeneo na sehemu kuu, na wanahudumu katika misheni rasmi za kuhubiri kote duniani. Katika njia hizi na nyinginezo, wanawake hutumia mamlaka ya ukuhani ingawaje hawatawazwi katika ofisi ya ukuhani. …
“… Katika wito wa kidini, ibada za hekaluni, mahusiano ya familia, na huduma binafsi, tulivu, wanawake na wanaume Watakatifu wa siku za Mwisho husonga mbele kwa nguvu na mamlaka ya ukuhani. Kutegemeana huku kwa akina kaka na akina dada katika kutimiza kazi ya Mungu kupitia nguvu Zake ni kiini cha injili ya Yesu Kristo” (Mada za Injili, “Mafundisho ya Joseph Smith Kuhusu Ukuhani, Hekalu, Wanawake,” topics.ChurchofJesusChrist.org).