Mafundisho na Maagano 2021
Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: “Kuliimarisha Kanisa”


“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: ‘Kuliimarisha Kanisa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Emma Smith

Machi 8–14

Mafundisho na Maagano 23–26

“Kuliimarisha Kanisa”

Kabla ya kusoma mwongozo huu, soma Mafundisho na Maagano 23–26 na utafakari kanuni unazohisi kwamba zitaimarisha washiriki wa darasa lako. Kisha fikiria ni rasilimali zipi zitakusaidia kufundisha, pamoja na zile ambazo zimependekezwa katika mwongozo huu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ni baraka gani tumezipata wakati “tulitumia muda [wetu] kwa kujifunza maandiko”? (Mafundisho na Maagano 26:1). Ni kwa jinsi gani tumehisi Roho nyumbani kwetu? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyoshinda changamoto na vizuizi ili kutenga muda wa kujifunza binafsi maandiko na kama familia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 23–26

Sote tunaweza kuliimarisha Kanisa.

  • Unaweza kutaka kuchunguza pamoja na washiriki wa darasa ni nini maana ya “kuwashawishi kanisa” (Mafundisho na Maagano 25:7). Pengine mtu angeweza kushiriki ufafanuzi toka kamusi wa shawishi au mifano ipi ya kushawishi wameiona. Ni nafasi zipi ambazo tunazo za kushauriana kila mmoja na mwenzake? Ni kwa jinsi gani hili linaimarisha Kanisa? Ni kipi tena tunachojifunza katika Mafundisho na Maagano 23–26 ambacho kinaweza kutusaidia kuimarisha Kanisa? Ungeweza kutaka kujadili jinsi kanuni hizi zinavyotumika katika kuimarisha nyumba zetu. Ili kutumia kanuni hizi katika kuhudumu kwetu, ungeweza kufanya mapitio ya sehemu za ujumbe wa Dada Bonnie H. Cordon “Kuwa Mchungaji” (Ensign au Liahona, Nov. 2018, 74–76).

Mafundisho na Maagano 24

Mwokozi anaweza kututoa “kutoa katika dhiki [yetu].”

  • Ufunuo katika Mafundisho na Maagano 24 ulitolewa kwa ajili ya “kuwaimarisha, kuwahamasisha, na kuwaelekeza” Joseph na Oliver wakati wa majaribu (Mafundisho na Maagano 24, kichwa cha habari cha sehemu; ona pia Watakatifu, 1:94–96). Ungeweza kulialika darasa kuipekua sehemu hii kwa ajili ya ushahidi kwamba Bwana alimfahamu Joseph na hali yake. Ni kwa jinsi gani ambavyo Bwana alishughulikia mahitaji ya Joseph? Je, anafanyaje sawa na hivyo kwetu sisi leo hii? Fikiria kuwauliza washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wa wakati walipohisi kwamba Bwana alifahamu hali zao binafsi na kuwatoa katika dhiki zao.

    Picha
    Yesu Kristo akiwaponya watu

    Aliponya Magonjwa Mengi Ya Kila Aina, na J. Kirk Richards

Mafundisho na Maagano 25

Emma Smith ni “mwanamke mteule.”

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata kitu muhimu katika ufunuo wa Bwana kwake Emma Smith, fikiria shughuli hii: Uliza nusu ya darasa kupekua sehemu ya 25 kwa ajili ya vitu ambavyo Bwana alimuamuru Emma avifanye, na uiulize nusu ya pili ipekue vitu ambavyo Aliahidi angefanya. Wahimize kuandika kile watakachopata na washiriki wao kwa wao. Washiriki wachache wa darasa wangeweza kushiriki kanuni ambazo ni muhimu kwao.

  • Ni maneno na virai gani katika sehemu ya 25 vinaunga mkono tangazo la Bwana kwa Emma Smith, “Wewe ni mwanamke mteule”? (mstari 3). Washiriki wa darasa wanaweza pia kujadili jinsi Emma alivyoishi kanuni zilizoko katika ufunuo huu. Nyenzo za msaada ni pamoja na video “An Elect Lady” (ChurchofJesusChrist.org), “Thou Art an Elect Lady” (Funuo Katika Muktadha, 33–39), na “Voices of the Restoration” katika mwongozo wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

  • Kulingana na Mafundisho na Maagano 25:11–12, Je, ni kwa namna gani Bwana anahisi kuhusu muziki mtakatifu? Labda washiriki wa darasa wangeweza kujadili njia za kutumia nyimbo za kanisa kualika Roho nyumbani kwao.

Mafundisho na Maagano 25:5, 14

Yatupasa kutafuta kuwa na “roho wa unyenyekevu.”

  • Bwana alimshauri Emma “endelea katika roho wa unyenyekevu” (Mafundisho na Maagano 25:14; ona pia mstari wa 5). Kuchunguza kile hii ingemaanisha, ungeweza kuandika ubaoni Unyenyekevu na uwaalike washiriki wa darasa waandike karibu nalo kile ambacho neno hilo linawasababisha kufikiria juu yake. Kisha wangeweza kupekua sehemu ya 25 kwa ajili ya maneno na virai ambavyo wanahisi vinahusuana na unyenyekevu na kisha washiriki walichokipata. Fikiria kushiriki kauli ya Mzee David A. Bednar katika ”Nyenzo za Ziada.” Kwa nini ni muhimu kuwa mnyenyekevu?

Mafundisho na Maagano 25:10, 13

Yatupasa kutafuta vitu vya ulimwengu bora.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia ushauri wa Bwana “kuyaweke kando mambo ya ulimwengu huu, na kuyatafuta mambo ya ulimwengu ulio bora” (Mafundisho na Maagano 25:10), ungeweza kuwaomba waorodheshe mifano ya “mambo ya ulimwengu huu” na mifano ya “mambo ya ulimwengu ulio bora.” Ni ushauri gani tunaweza kushiriki sisi kwa sisi kutusaidia kufokasi kwenye vitu vya milele? Ni kwa jinsi gani ushauri katika mstari wa 13 unahusiana na lengo hili?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Unyenyekevu ni nguvu.

Mzee David A. Bednar alifafanua: “Sifa ya kama Kristo ya unyenyekevu mara nyingi imeeleweka vibaya katika ulimwengu wetu wa siku hizi. Unyenyekevu ni nguvu, sio udhaifu; tendaji, sio baridi; jasiri, hauogopi; iliyozuiliwa, isiyo na kutokuwa na kiasi, yenye kiasi; isiojivuna na ukarimu, isiyo na ujeuri. Mtu mnyenyekevu hakasiriki kirahisi, hajidai, au sio dhalimu na haraka hukubali mafanikio ya wengine” (“Unyenyekevu na Upole wa Moyo,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 32).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya baraka zilizoahidiwa. Unapowaalika washiriki wa darasa kutenda kulingana na kile wanachojifunza, shuhudia juu ya baraka Mungu ameahidi (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Chapisha