Mafundisho na Maagano 2021
Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: “Vitu Vyote Lazima Vitendeke kwa Mpango”


“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: ‘Vitu Vyote Lazima Vitendeke kwa Mpango,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Joseph Smith

Machi 15–21

Mafundisho na Maagano 27–28

“Vitu Vyote Lazima Vitendeke kwa Mpango”

Ingawaje matukio yaliyochochea ufunuo katika Mafundisho na Maagano 27–28 yalifanyika katika wakati na mahali tofauti, kanuni zinazofundishwa katika sehemu hizi zina umuhimu leo hii. Ni kanuni zipi zinaweza kubariki washiriki wa darasa lako katika hali wanazokabiliana nazo?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache ili wapitie Mafundisho na Maagano 27–28 na watafute mstari au kirai wanachokiona ni chenye maana kwao. Ili kumpa kila mtu nafasi ya kushiriki, ungeweza kuwagawanya washiriki wa darasa jozi ili washiriki kile walichopata.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 27:1–2

Tunapaswa kushiriki sakramenti na jicho likiwa kwenye utukufu wa Mungu pekee.

  • Ili kuhimiza mjadala kuhusu Mafundisho na Maagano 27:1–2, fikiria kuandika swali kama hili ubaoni: Mwokozi alitufundisha nini kuhusu lengo la sakramenti? Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta virai katika vifungu hivi ambavyo vinawasaidia kujibu swali hilo. Wanaweza kuwa tayari kushiriki misukumo waliyopokea kuhusu jinsi ya kuwa na uzoefu mtakatifu zaidi wakati wanapopokea sakramenti.

    Washiriki wa darasa wangeweza kupata umaizi wa ziada kwa kusoma kile Mwokozi alichosema wakati alipoanzisha sakramenti (ona Luka 22:19–20; 3 Nefi 18:1–11; ona pia video “The Last Supper” kwenye ChurchofJesusChrist.org). Kama Mwokozi angekuwa katika mkutano wetu wa sakramenti, ni kitu gani tungefanya tofauti?

    mkate wa sakramenti na kikombe

    Sakramenti ina ishara za dhabihu ya Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 27:15–18

Silaha za Mungu zitatusaidia kutulinda dhidi ya uovu.

  • Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi ya kutumia silaha za Mungu ili wastahimili uovu katika siku zetu? Fikiria kumuomba mtu achore ubaoni vazi la kivita lililoelezewa katika mistari ya 15–18. Washiriki wa darasa kisha wangeweza kushiriki umaizi wowote waliougundua katika kujifunza kwao binafsi kuhusu vipande vya vazi la kivita. Au darasa lingeweza kusoma Mafundisho na Maagano 27:15–18 na kubandika majina kwenye vipande vya vazi la kivita lililoko ubaoni na sehemu za mwili linazozilinda. Je, inamaanisha nini kuvaa silaha za Mungu? Labda washiriki wa darasa wangeweza kuzungumza kuhusu jinsi Bwana anavyotulinda kutokana na uovu wakati tunapovaa silaha za Mungu.

  • Kama unawafundisha vijana, unaweza taka kuhusisha Mafundisho na Maagano 27:15–18 pamoja na viwango katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana. Kwa mfano, washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari na kujadili kwa nini tunahitaji silaha za Mungu. Kisha wanaweza kufanya kazi katika jozi na kufanya mapitio ya kiwango kimoja katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana. Je, tunajifunza nini kutoka kwa vyanzo hivi kuhusu mashambulizi ya Shetani dhidi yetu? Silaha za Mungu zinaweza kutusaidia vipi kustahimili mashambulizi haya. Tunawezaje kuvaa silaha Zake?

Mafundisho na Maagano 28

Nabii aliye hai hupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa la Bwana.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kuhusu wajibu wa nabii ungeweza kufanya mapitio ya uzoefu ambao ulimsababisha Joseph Smith kusali na kupokea sehemu ya 28 (ona kichwa cha habari cha sehemu), na kisha ungeweza kusoma mistari ya 2–3, 6–7, 11–13. Je, ni kwa jinsi gani Shetani hujaribu kutushawishi tuwafuate wale ambao Bwana hajawachagua? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki uzoefu ambao umeimarisha shuhuda zao kwamba nabii hupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa.

  • Njia mojawapo ya washiriki wa darasa kufanya mapitio ya Mafundisho na Maagano 28 ni kujifanya kwamba wanafahamu mtu ambaye hivi karibuni alipokea wito Kanisani. Ni nini tunaweza kushiriki kutoka Mafundisho na Maagano 28:1–6, 13–16 ili kumsaidia mtu huyo katika wito wake? Nukuu katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuongeza umaizi kwenye mjadala.

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Ushauri kuhusu ufunuo binafsi.

Rais Joseph F. Smith na washauri wake katika Urais wa Kwanza walifundisha:

“Wakati maono, ndoto, lugha, unabii, misukumo au karama au msukumo wowote wa ajabu, vinaonyesha kitu nje ya maelewano ya funuo zilizokubaliwa na Kanisa au kinyume na maamuzi ya mamlaka yake, Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kujua kwamba hayo si ya Mungu, bila kujali jinsi yanavyoonekana kukubalika. … Katika mambo ya ulimwengu na ya kiroho, Watakatifu hupokea mwongozo mtakatifu na ufunuo unaowahusu wao, lakini hii haileti mamlaka ya kuwaongoza wengine. …

“Historia ya Kanisa inaonyesha funuo nyingi bandia zilizodaiwa na walaghai au watu wa dini ambao waliamini dalili walizotafuta kuwaelekeza watu wengine kuzikubali, na katika kila tukio, majuto, huzuni na maafa yametokea kutokana na hayo” (Joseph F. Smith, Anthon H. Lund, Charles W. Penrose, “A Warning Voice,” Improvement Era, Sept. 1913, 1148–49).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fokasi kwenye mafundisho ya kweli. Rais Boyd K. Packer alifundisha, “Mafundisho ya Kweli, yaliyoeleweka, hubadilisha fikra na tabia” (“Usiwe na Hofu,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 79). Tunapofundisha, ni lazima tulenge katika mafunzo ya Yesu Kristo kama tunataka kusaidia kuleta nafsi Kwake.