Mafundisho na Maagano 2021
Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Historia ya—Joseph Smith 1:66–75: “Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”


“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Historia ya—Joseph Smith 1:66–75: ‘Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Historia ya—Joseph Smith 1:66–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021

Mto Susquehanna

Februari 8–14

Mafundisho na Maagano 12–13; Historia ya—Joseph Smith 1:66–75.

“Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”

Jinsi vile Roho Mtakatifu alivyoangaza akili za Joseph Smith na Oliver Cowdery kuhusu maandiko, Anaweza kukutia msukumo unapojifunza kwa moyo wa kusali Mafundisho na Maagano 12–13 na Historia ya—Joseph Smith 1:66–75.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia mojawapo ya kutia moyo kushiriki ni kuwauliza washiriki wa darasa jinsi wanavyojifunza maandiko. Walifanya nini ili kupata umaizi katika maandiko wiki iliyopita?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 13

Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa na Yohana Mbatizaji.

  • Njia mojawapo ya kujadili kweli katika Mafundisho na Maagano 13 inaweza kuwa kwa washiriki wa darasa kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo sehemu hii inaweza kuwasaida vijana kuelewa Ukuhani wa Haruni vyema zaidi. Ni nini sehemu ya 13 inafundisha kuhusu Ukuhani wa Haruni ambacho wavulana na wasichana wanapaswa kuelewa? Ili kumpa kila mtu nafasi ya kuchangia, ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kujadiliana maswali haya katika jozi na kisha washiriki na darasa kile ambacho wamejifunza wao kwa wao.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza nyenzo zinazoweza kueleza baadhi ya virai katika Mafundisho na Maagano 13. Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki walichojifunza kutokana na kujifunza nyenzo hizi. Ili kuchochea majadiliano kuhusu funguo ambazo zimetajwa katika sehemu hii, unaweza kuonyesha funguo na uwaalike washiriki wa darasa wazungumze kuhusu kile funguo zinatuwezesha kufanya. Ufafanuzi kutoka kwa Dada Ruth na Mzee Dale G. Renlund katika “Nyenzo za Ziada” pia unaweza kusaidia. Ni baraka gani funguo za Ukuhani wa Haruni zinatuwezesha kupata? Ni kwa namna gani maisha yetu yangekuwa tofauti bila baraka hizi?

  • Sehemu ya uzuri wa injili iliyorejeshwa ni kwamba inatuhusisha katika kazi sawa kama watu waliokuwa katika maandiko: kujenga ufalme wa Mungu duniani. Hii inatufanya sisi, kwa namna fulani, “watumishi wenza” pamoja nao. Je, inamaanisha nini kuwa mtumishi mwenza katika kazi ya Bwana?? Mathayo 3:13–17; Luka 1:13–17; 3:2–20 yaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema kazi aliyofanya Yohana Mbatizaji.

    Joseph Smith akimbatiza Oliver Cowdery

    Joseph Smith akimbatiza Oliver Cowdery, na Del Parson

Historia ya—Joseph Smith 1:66–75

Ibada hutupatia njia ya kufikia nguvu za Mungu.

  • Ili kuwapa washiriki wa darasa nafasi ya kushuhudiana wao kwa wao kuhusu baraka zinazotokana na kupokea ibada za ukuhani, ungeweza kuwaalika wafanye mapitio ya Historia ya—Joseph Smith 1:66–75, ikijumuisha maelezo ya mstari wa 71, wakitafuta baraka walizopokea Joseph na Oliver baada ya ubatizo wao na kutawazwa kwao katika ukuhani. Ni kwa jinsi gani ibada huleta nguvu za kiroho. Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wao wenyewe wakati walipohisi nguvu za Mungu zinazokuja kutokana na kupokea ibada za ukuhani kama vile ubatizo, sakramenti, au ibada za hekaluni. Pia ungeweza kuonyesha video “Blessings of the Priesthood” (ChurchofJesusChrist.org) kama sehemu ya mjadala.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kubuni jedwali linaloonyesha baraka zinazokuja kutoka kwa ibada za ukuhani. Kwa mfano, ungeweza kuandika ubaoni vichwa vya habari Ibada na Baraka. Washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza maandiko kama yafuatayo ili kujaza jedwali: Yohana 14:26; Matendo Mitume 2:38; Mafundisho na Maagano 84:19–22; 131:1–4; Historia ya—Joseph Smith 1:73–74. Pia wanaweza kujumuisha baraka nyingine ambazo wamepokea kwa sababu ya ibada hizi. Labda wangeweza kushiriki uzoefu wa wakati walipohisi kwamba ibada walizopokea zilileta nguvu za Mwokozi katika maisha yao.

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Funguo za ukuhani ni nini?

Mzee Dale G. Renlund na mkewe, Ruth, walitoa maelezo haya kuhusu funguo za ukuhani.

“Istilahi funguo za ukuhani inatumika kwa njia mbili. Ya kwanza inarejelea haki maalum au haki inayotunukiwa kwa wale wote wanaopokea Ukuhani wa Haruni au Melkizedeki. … Kwa mfano, wenye Ukuhani wa Haruni hupokea funguo za kuhudumu za malaika na funguo za injili ya matayarisho ya toba na ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi (ona Mafundisho na Maagano 13:1; 84:26–27). Wenye Ukuhani wa Melkizedeki hupokea ufunguo wa siri za ufalme, ufunguo wa ufahamu wa Mungu, na funguo za baraka zote za kiroho za Kanisa (ona Mafundisho na Maagano 84:19; 107:18). …

“Jinsi ya pili istilahi funguo za ukuhani inavyotumika inarejelea uongozi. Viongozi wa ukuhani hupokea funguo za ziada, haki ya kusimamia mpangilio wa kitengo cha Kanisa au akidi. Kuhusu swala hili, funguo za ukuhani ni mamlaka na nguvu za kuelekeza, kuongoza, na kutawala Kanisa” (Ukuhani wa Melkizedeki: Kuelewa Mafundisho, Kuishi Kanuni [2018], 26).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda wako kila mara. “Ushuhuda wako rahisi, wa kweli kuhusu ukweli wa kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wale unaowafundisha. … Hauhitajiki kuwa wa maelezo sana au mrefu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11). Fikiria kushiriki ushuhuda wako binafsi wa Ukuhani wa Haruni unapojadili Mafundisho na Maagano 13.