Mafundisho na Maagano 2021
Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11: “Kwamba Uweze Kutoka Mshindi”


“Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11: ‘Kwamba Uweze Kutoka Mshindi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Mswada wa Kitabu cha Mormoni

Nakala ya mswada wa kwanza wa Kitabu cha Mormoni.

Februari 1–7

Mafundisho na Maagano 10–11

“Kwamba Uweze Kutoka Mshindi”

Ni mawazo gani uliyopata ulipokuwa ukisoma Mafundisho na Maagano 10–11? Ni mawazo gani yalikujia kuhusu mahitaji ya wale ambao unawafundisha?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwapa washiriki wa darasa nafasi ya kuzungumza kuhusu kile ambacho walijifunza walipojifunza maandiko wao binafsi na kifamilia, ungeweza kuandika ubaoni Mafundisho na Maagano 10 na Mafundisho na Maagano 11. Washiriki wachache wa darasa wangeweza kuandika, chini ya mojawapo ya vichwa vya habari, nambari ya mstari ambapo walipata ukweli muhimu. Chagua baadhi ya hiyo mistari, na uwaalike washiriki wa darasa washiriki kweli walizozipata pale.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 10:1–33

Shetani anatafuta kuharibu kazi ya Mungu.

  • Mafundisho na Maagano 10 inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua na kustahimili juhudi za Shetani kuangamiza imani yao. Ili kutoa muktadha wa kihistoria wa sehemu hii, ungeweza kumualika mshiriki wa darasa ashiriki historia ya Martin Harris kupoteza kurasa 116 za tafsiri ya Kitabu cha Mormoni (ona kichwa cha habari cha sehemu ya Mafundisho na Maagano 3 na Watakatifu, 1:50–53). Washiriki wa darasa kisha wangeweza kupekua Mafundisho na Maagano 10:1–33 ili kupata mpango wa Shetani juu ya kurasa zilizopotea. Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu njia ambazo Shetani hufanya kazi na kwa nini yeye hufanya mambo haya? (ona pia mstari wa 63). Ni kwa jinsi gani anafanya kazi kwa njia sawa katika siku zetu? Ni kwa jinsi gani Bwana anatusaidia kumshinda Shetani katika maisha yetu?

Mafundisho na Maagano 10:34–52

“Hekima ya Bwana ni kuu kuliko hila ya ibilisi.”

  • Wakati tunapohisi kukata tamaa kuhusu dhambi zetu, tunaweza kupata tumaini katika kufahamu jinsi Bwana alivyoifidia dhambi ambayo Joseph Smith na Martin Harris walitenda wakati walipokosa kumtii Bwana na kupoteza kurasa 116 za tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Fikiria jinsi unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata tumaini katika historia hii. Kwa mfano, unaweza kuwaalika kushiriki kitu ambacho wanajifunza kuhusu Bwana kutoka Mafundisho na Maagano 10:34–52 (ona pia Mafundisho na Maagano 3:1–3). Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi ambavyo wameona kwamba “hekima ya Bwana ni kuu kuliko hila ya ibilisi” (Mafundisho na Maagano 10:43). Ni kwa jinsi gani ufahamu huu huimarisha imani yetu kwake Yeye?

    Mormoni akifupisha mabamba ya dhahabu

    Mormoni Akifupisha Maandishi ya Mabamba, na Tom Lovell

Mafundisho na Maagano 11

Kama tutamuomba Mungu, tutapokea.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unatualika tusome Mafundisho na Maagano 11 kana kwamba iliandikwa kwa ajili yetu. Labda washiriki wa darasa wangekuwa tayari kushiriki kitu kutoka kwenye sehemu ambayo hasa ni muhimu kwao. Je, wanapanga vipi kutumia kile walichojifunza?

  • Njia moja ya kuhimiza majadiliano kuhusu Mafundisho na Maagano 11 ni kwa kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta kanuni katika sehemu hiyo kisha waandike swali juu yake. Maswali kama hayo yangeweza kujumuisha “Je, humaanisha nini kuambatana na Kristo kwa moyo wako wote?” (mstari wa 19) au “Ni kwa jinsi gani tunalipata neno la Mungu?” (mstari wa 21). Washiriki wa darasa wangeweza kuyaweka maswali yao kwenye sehemu ya juu ya karatasi na kuzipitisha kote chumbani, wakiongeza mawazo na majibu ya kila maswali yao. (Ingeweza kusaidia kwa kuligawanya darasa katika makundi madogo kwanza.) Kisha washiriki wa darasa wangeweza kushiriki na darasa baadhi ya umaizi ambao wengine waliandika kuhusu swali lao.

Mafundisho na Maagano 11:8–26

Mungu atatupa Roho Wake tunapojitayarisha katika njia Yake.

  • Je, washiriki wa darasa lako wangenufaika kutokana na kuzungumzia kuhusu namna ya kutambua ufunuo wa binafsi kupitia kwa Roho Mtakatifu? Kama ndivyo, ungeweza kuanzisha mjadala kwa kuwaalika kufikiria kwamba waliombwa kuandika kweli kadha wa kadha kuhusu jinsi ya kupokea ufunuo wa binafsi. Ni nini wangejumuisha kutoka katika Mafundisho na Maagano 11:8–26? Kwa mfano, wangeandika nini kuhusu kujitayarisha ili kupokea mwongozo kwa ajili ya maisha yetu na majibu ya maswali yetu? Ni nini wangesema kuhusu jinsi ya kutambua majibu yanapokuja? Waalike washiriki watafakari jinsi watakavyotumia kile walichojifunza wanapojitahidi kutafuta ufunuo wa binafsi.

    Kama sehemu ya shughuli hii, ungeweza kushiriki kauli hii kutoka kwa Dada Julie B. Beck, aliyekuwa Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama: “Uwezo wa kuwa na sifa ya kufaa, kupokea na kutenda juu ya ufunuo binafsi ni ujuzi pekee muhimu ambao unaweza kupatikana katika maisha haya” (“Na Juu ya Watumishi Wanawake katika Siku Zile, Nitamimina Roho Yangu,” Ensign au Liahona, Mei 2010, 11).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajumuishe wale wote wanaosumbuka. Unaweza kufanya nini wakati mshiriki wa darasa anapoonekana kutokuwa sambamba na darasa? Wakati mwingine anahitaji tu kujumuishwa. Fikiria kumpangia mtu huyu jukumu ili ashiriki katika somo lijalo. Kama hatajibu juhudi zako mara ya kwanza, endelea kuonyesha upendo na kujali. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8–9.)