Mafundisho na Maagano 2021
Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63: “Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu”


“Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63–11: ‘Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Shamba la Missouri

Springhill, Daviess County, Missouri, na Garth Robinson Oborn

Juni 7–13

Mafundisho na Maagano 63

“Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu”

Andika misukumo unayopokea wakati unapojifunza. Mafundisho na Maagano 63. Msukumo unaweza kuonekana mdogo, lakini kama mbegu, unaweza kukua kuwa kitu cha maana na kuzaa matunda unapozidi kutafuta na kutafakari.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kusaidia kufokasi mjadala wenu juu ya vifungu ambavyo washiriki wa darasa wanaviona kuwa vya maana zaidi kwao, unaweza kuwaalika waandike kwenye vipande vya karatasi baadhi ya mistari kutoka sehemu ya 63 ambayo wangependa kuijadili. Kisha unaweza kuzikusanya karatasi na muanze kujadiliana mistari ambayo ilipendekezwa na washiriki wengi wa darasa. Waulize washiriki kwa nini walichagua mistari hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 63:7–12

Ishara huja kupitia imani na mapenzi ya Mungu.

  • Kuanza mjadala juu ya kanuni zinazofundishwa katika Mafundisho na Maagano 63:7–12, inaweza kuwa yenye kusaidia kufanya mapitio ya mifano michache katika maandiko ya watu walioshuhudia ishara au miujiza. Labda washiriki wa darasa wanaweza kufikiria mifano ya watu ambao imani yao iliimarishwa na ishara (ona, kwa mfano, Luka 1:5–20, 59–64) au watu ambao hawakuwa imara hata baada ya kushuhudia ishara (ona, kwa mfano, 1 Nefi 3:27–31; Alma 30:43–56). Washiriki wa darasa kisha wangeweza kutumia kile wanachojifunza katika Mafundisho na Maagano 63:7–12 ili kuelezea mwitikio wao tofauti kwenye ishara. Au mnaweza kufanya mapitio ya vifungu vingine vya maandiko kuhusu ishara, kama vile vilivyoorodheshwa chini ya “Ishara” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Tunawezaje kuwa na hakika kwamba hatutafuti au hatutegemei ishara kama msingi wa imani yetu?

Mafundisho na Maagano 63:13–16

Usafi wa kimwili unamaanisha kuweka mawazo na vitendo vyetu kuwa safi.

  • Ingawa kiasi kikubwa cha Mafundisho na Maagano 63:13–16 kinazungumzia uzinzi mahususi, kanuni zilizofundishwa zinaweza kutumika kwa ukiukaji wowote wa sheria ya usafi wa kimwili. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kutambua athari zilizoelezwa katika Mafundisho na Maagano 63:13–16. Wanaweza hata kutengeneza “tahadhari” (mstari wa 15) au ishara za tahadhari ambazo zinaonya dhidi ya athari hizi. Pia wanaweza kujadiliana kile wanachodhani ni maana ya athari hizi. Kwa mfano, ni kwa nini kuvunja sheria ya usafi wa kimwili kunaweza kusababisha hukumu kumjia mtu “kama mtego” (mstari wa 15)? Ni kwa nini Bwana anatushauri “tutubu upesi” (mstari wa 15) dhambi ya uzinzi na uasherati? (ona kauli ya Dada Linda S. Reeves katika “Nyenzo za ziada”).

  • Kusoma Mafundisho na Maagano 63:16 kunaweza kuelekeza kwenye mjadala kuhusu kuenea sana kwa ushawishi wa pornografia katika jamii yetu. Ni kwa jinsi gani ushauri katika mstari wa 16 unahusiana na shida hii? (Ingawa ufunuo huu unarejelea mahususi wanaume wanaotamani wanawake, maonyo haya ni kwa kila mtu.) Ni nini tunaweza kufanya kujilinda wenyewe na wapendwa wetu kutokana na pornografia? Washiriki wa darasa wanaweza kuwa tayari kushauriana. Tovuti AddressingPornography.ChurchofJesusChrist.org inaweza kutoa tumaini na msaada kwa yeyote ambaye anaweza kuwa anapambana na pornografia.

    mwanamume na mwanamke nje ya hekalu

    Tunabarikiwa tunapotii sheria ya usafi wa kimwili.

Mafundisho na Maagano 63:58–64

Vitu takatifu vinapaswa kupewa heshima kubwa.

  • Wewe na darasa lako mnaweza kujadili Mafundisho na Maagano 63:58–64 kama onyo dhidi ya kulitaja bure jina la Bwana, na baadhi ya nyenzo katika makala ya Mada za Injili yenye kichwa cha habari “Lugha Chafu” (topics.ChurchofJesusChrist.org) zinaweza kuboresha mjadala kama huu. Ungeweza pia kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia mistari hii kwa upana zaidi. Kwa mfano, mnaweza kujadili jinsi kirai “bila mamlaka” (mstari wa 62) kinavyoongeza uelewa wetu wa kifungu hicho. Washiriki wa darasa wanaweza pia kuorodhesha vitu vikatifu ambavyo huja “kutoka juu,” au kutoka kwa Mungu. Inamaanisha nini kuvitamka vitu hivi “kwa uangalifu”? (mstari wa 64).

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Usafi wa kimwili unatufanya wastahiki wa ushirika wa Roho Mtakatifu?

Dada Linda S. Reeves, mshiriki wa awali katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alifundisha:

“Sijui kitu chochote ambacho kitatufanya wastahiki wa ushirika wa kudumu wa Roho Mtakatifu kama vile uadilifu. …

“Wakati tunapohusika katika kutazama, kusoma, au kushuhudia kitu chochote ambacho hakifikii vigezo vya Baba yetu wa Mbinguni, kinatudhoofisha. Bila ya kujali umri wetu, kama kile tunachotazama, kusoma, kusikiliza, au kuchagua kufanya hakikubaliani na vigezo vya Bwana katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, zima, rarua, tupilia mbali, na funga mlango kwa kishindo. …

“… Ninaamini kwamba kama kila siku tutakumbuka na kutambua kina cha upendo ule Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu walio nao kwetu, tutakuwa radhi kufanya chochote ili kurudi katika uwepo Wao tena, tukizungukwa na upendo Wao milele” (“Worthy of Our Promised Blessings,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 10–11).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki mtakatifu. Ujumbe katika nyimbo za kanisa na nyimbo kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto unaweza kuimarisha mafundisho unayojifunza katika maandiko. Kwa mfano, kuimba wimbo kuhusu kulisifu jina la Mungu, kama vile “Glory to God on High” (Nyimbo za Kanisa, na. 67), kunaweza kuimarisha ujumbe katika Mafundisho na Maagano 63:58–64.