Mafundisho na Maagano 2021
Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62: “Wenye Mwili Wako Katika Mikono Yangu”


“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62: ‘Wenye Mwili Wako Katika Mikono Yangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Mto Missouri

Moto wa Kambi huko Missouri, Na Bryan Mark Taylor

Mei 31–Juni 6.

Mafundisho na Maagano 60–62

“Wenye Mwili Wako Katika Mikono Yangu”

Mzee Ronald A. Rasband alisema: “Kila mmoja wetu lazima kwanza tujiimarishe wenyewe kiroho na kisha kuwaimarisha wale wanaotuzunguka. Tafakari maandiko kila siku, na kumbuka mawazo na hisia unazopata unapoyasoma” (“Usije Ukasahau,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 114).

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unaweza kuchochea mjadala wenye maana kupitia kuwaalika washiriki wa darasa kujibu swali maalum au wazo ambalo linahusika na maandiko wanayosoma nyumbani. Kwa mfano, unaweza kuwaalika kushiriki kitu ambacho walijifunza wiki hii kuhusu Baba wa Mbinguni au Yesu Kristo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 60:2–3, 7, 13–14; 62:3, 9

Bwana anafurahia tunapofungua vinywa vyetu kushiriki injili.

  • Kama waumini wa Kanisa, tunajua kwamba injili ya urejesho ni hazina ya thamani kubwa ambayo inabariki maisha ya watoto wa Mungu. Kwa nini wakati mwingine tunasita kushiriki ushuhuda wetu kwa wengine? Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha kwenye ubao baadhi ya sababu za sisi kutofungua vinywa vyetu kushiriki injili. Kisha washiriki wa darasa wanaweza kusoma Mafundisho na Maagano 60:2–3, 7, 13–14; 62:39, wakitafuta maneno au virai ambavyo vinawachochea kushiriki injili. Wangeweza kuorodhesha ubaoni kile walichokipata. Labda baadhi ya washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wao wakati waliposhinda hofu na kushiriki injili na mtu mwingine.

  • Kote katika Mafundisho na Maagano 60–62, kuna mafundisho, yote mawili yaliyotajwa na yasiyotajwa, kuhusu kushiriki injili. Ili kuwasaida washiriki wa darasa kugundua mafundisho haya, unaweza kumuomba kila mtu afanye mapitio ya mojawapo ya sehemu hizi na kushiriki kitu chochote ambacho watakipata kinachowafundisha kuhusu kushiriki injili. Inaweza kuboresha mjadala kusoma kuhusu wamisionari walio mfano bora kwingineko katika maandiko (ona, kwa mfano, Matendo 8:27–40; Alma 19:16–17) na kujadili kile tunachojifunza kutoka kwao. Je, ni mifano gani tunaweza kushiriki kutoka katika maisha yetu wenyewe? Je, washiriki wowote wa darasa wanaweza kushiriki jinsi walivyotambulishwa kwenye injili na jinsi walivyohisi kuhusu watu ambao waliwafundisha. Darasa lako linaweza kufaidika kutokana na kuigiza njia ambazo tunaweza “kufumbua vinywa [vyetu]” na kushiriki injili.

    wamisionari ndani ya basi

    Mungu anatutaka tushiriki injili na wengine.

Mafundisho na Maagano 60:2–4; 61:1–2, 20, 36–38; 62:1, 6

Maandiko yanatufundisha kuhusu Yesu Kristo.

  • Alika washiriki wa darasa waandike kwenye ubao kitu chochote walichojifunza kuhusu Mwokozi wiki hii kutokana na kujifunza sehemu za 60–62, pamoja na mistari husika. Au wanaweza kuchunguza Mafundisho na Maagano 60:2–4; 61:1–2, 20, 36–38; 62:1, 6 kutafuta vitu vinavyofundishwa juu ya Mwokozi. Ni hadithi zipi kutoka kwenye maandiko au maisha yetu zinaonesha wajibu na sifa za Mwokozi ambazo tumejifunza juu yake? (Kwa mfano, Yohana 8:1–11; Etheri 2:14–15). Labda ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki shuhuda zao juu ya Yesu Kristo au watafakari peke yao juu ya umuhimu Wake kwao.

Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22; 62:5–8

Bwana anatutaka tufanye baadhi ya maamuzi “kama tunavyoona [sisi] kuwa ni vyema.”

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22; 62:5–8 katika jozi au vikundi vidogo na washiriki kile wanachohisi kinaweza kuwa ujumbe wa Bwana kwetu sisi. Ni wakati gani wamehisi kwamba ni sharti watumie busara yao katika kufanya uamuzi? Fikiria kushiriki maelezo kutoka kwa Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” kama sehemu ya mjadala. Jinsi gani wazazi wanaweza kuwasaidia watoto wao kujifunza kanuni hii muhimu?

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kufanyia kazi uamuzi wetu bora.

Rais DallinH. Oaks alifundisha:

“Hamu ya kuongozwa na Bwana ni nguvu, lakini inahitaji kuambatana na ufahamu kwamba Baba yetu wa Mbinguni hutuachia maamuzi mengi kwa ajili ya uchaguzi wetu binafsi. Kufanya maamuzi binafsi ni mojawapo ya vyanzo vya kukua ambako tunatarajiwa kupitia katika maisha ya hapa duniani. Watu ambao hujaribu kuhamisha ufanyaji uamuzi wote kwa Bwana na kuomba kwa ajili ya ufunuo katika kila uchaguzi baada ya muda mfupi watapata hali ambazo kwazo wanasali kwa ajili ya mwongozo ila hawaupati. Kwa mfano, hili lina uwezekano mkubwa wa kutokea katika hali nyingi tofauti ambazo chaguzi ni ndogo au uchaguzi unakubalika.

Tunafaa kuchunguza mambo akilini mwetu, tukitumia uwezo wa kufikiri ambao Muumba wetu ameweka ndani yetu. Kisha tunapaswa kusali kwa ajili ya mwongozo na kuufanyia kazi kama tutaupokea. Kama hatutapokea mwongozo, tunapaswa kutenda kulingana na maamuzi yetu bora” (“Nguvu Yetu Yaweza Kuwa Anguko Letu,” Ensign, Okt. 1994, 13–14).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajue wale wanaopambana. Mapambano ya wale unaowafundisha yanaweza kuwa magumu kugundua. Lakini kupitia usaidizi wa Roho na viongozi wako, unaweza kujua njia bora ya kuwafikia watu hawa. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8–9.)