Mafundisho na Maagano 2021
Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58–59: “Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema”


“Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58-59: ‘Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58–59,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

Picha
Mtaa wa Independence Missouri

Independence, Missouri, na Al Rounds

Mei 24–30

Mafundisho na Maagano 58–59

“Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema”

Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 58–59, fikiria kuhusu maswali yafuatayo: Ni nini unahisi kuvuviwa kushiriki na darasa lako? Ni nini unatumaini kuwa watagundua? Ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia kugundua vitu hivi?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwachochea washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho walijifunza katika maandiko yao, unaweza kuandika kwenye ubao maswali yafuatayo: Tulijifunza nini? Ni jinsi gani tutaishi kile ambacho tulijifunza? Washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha chini ya swali la kwanza kweli walizopata katika Mafundisho na Maagano 58–59. Kisha wanaweza kutumia dakika chache wakijadiliana mawazo kwa ajili ya kuishi kulingana na kweli hizo na kuyaandika mawazo yao chini ya swali la pili.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 58:1–5; 26–33

Miujiza inatokea kulingana na muda wa Mungu na bidii yetu.

  • Mafundisho na Maagano 58 inafundisha kwamba kweli zinaweza kuleta amani katika nyakati za majaribu. Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamegundua baadhi ya kweli hizi wakati wakijifunza sehemu hii; waalike kushiriki kile walichojifunza. Au wanaweza kutafuta mistari 1–5, 26–33 darasani, kibinafsi, au katika vikundi, kwa ajili ya kitu ambacho kinaweza kuwa cha usaidizi kwa mtu fulani ambaye anataabika au ambaye anasubiri baraka iliyoahidiwa. Baada ya kushiriki walichokipata, labda baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu au maandiko mengine ambayo yamedhihirisha kweli zilizo katika mistari hii.

  • Kama sehemu ya mjadala wenu wa kanuni hii, unaweza kuonesha video “Hope Ya Know, We Had a Hard Time” (ChurchofJesusChrist.org) na kujadiliana kile ambacho tunaweza kufanya ili kuwasaidia wale ambao wanapitia katika nyakati ngumu. Nukuu ya Dada Linda S. Reeves katika “Nyenzo za Ziada” ingeweza pia kusaidia mjadala wenu. Je, ni kwa jinsi gani maneno ya Dada Reeves yanaathiri jinsi tunavyochukulia changamoto zetu?

Mafundisho na Maagano 58:26–29

Tunaweza “kutekeleza haki nyingi” kwa “hiari yetu wenyewe.”

  • Je, washiriki wa darasa walijifunza nini kutokana na kujifunza Mafundisho na Maagano 58:26–29 wiki hii? Labda unaweza kuligawa darasa katika vikundi na kuwaalika washiriki wa darasa wajadili katika vikundi vyao virai ambavyo waliviona vikiwa muhimu katika mistari hii. Ni jinsi gani mistari hii inatushawishi sisi “kutekeleza haki nyingi? (mstari wa 27). Kwa nini Bwana hataki “tulazimishwe katika mambo yote”? (imstari wa 26). Ni kipi ambacho mistari hii inapendekeza kuhusu kile Bwana anachotaka sisi tuwe?

Mafundisho na Maagano 59:9–19

Sabato ni siku ya Bwana.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza kile ambacho Bwana aliwafundisha Watakatifu wa mwanzo kule Missouri kuhusu siku ya Sabato, unaweza kuwaalika wachunguze Mafundisho na Maagano 59:9–19 na waorodheshe kwenye ubao kile ambacho kila mstari unatufundisha kuhusu Sabato. Washiriki wa darasa pia wanaweza kushiriki jinsi ambavyo ushuhuda wao juu ya siku ya Sabato umekua wakati walipoitakasa siku ya Sabato. Sabbath.ChurchofJesusChrist.org ina video kadhaa ambazo zinaweza zikasaidia kuanzisha mjadala.

  • Katika Mafundisho na Maagano 59, Bwana alifundisha kuhusu siku ya Sabato kwa kutumia maneno kama vile “kufurahi,” “changamfu,” na “furaha” (mistari 14–15). Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta maneno kama haya katika mistari 9–19. Washiriki wa darasa kisha wanaweza kushiriki kile ambacho wao hufanya kusababisha siku ya Sabato kuwa yenye furaha. Tunawezaje kutumia mistari hii kuwafundisha wengine sababu ya kuheshimu siku ya Sabato?

  • Mjadala huu pia unaweza kuwa nafasi ya washiriki wa darasa kushiriki mawazo kuhusu jinsi ambavyo wao na familia zao hutumia Sabato kufanya nyumba zao kitovu cha kujifunza kwao injili. Waalike kushiriki jinsi juhudi zao zinavyowasaidia kusalia “kikamilifu zaidi … wamejilinda na dunia pasipo mawaa” (mstari wa 9).

    Picha
    mkate na vikombe vya sakramenti

    Sakramenti ni sehemu muhimu ya kuheshimu Sabato.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Majaribu yetu yanaweza kutuelekeza kwa Mwokozi.

Linda S. Reeves, mshiriki wa awali katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alifundisha:

“Mungu huruhusu tujaribiwe na kupimwa, wakati mwingine ili kufikia uwezo wetu wa juu. Tumeona maisha ya wapendwa wetu—na pengine yetu wenyewe—kistiari yakiteketezwa na tumejiuliza ni kwa nini Baba wa Mbinguni mwenye upendo na mwenye kujali angeruhusu mambo kama haya kufanyika. Lakini hatuachi katika majivu; Anasimama na mikono iliyonyooka, akitualika kwa shauku kuja Kwake. …

“… Ana shauku ya kutusaidia, kutufariji, na kutuliza uchungu wetu wakati tunapotegemea uwezo wa Upatanisho na kuheshimu maagano yetu. Majaribu na taabu ambazo tunapitia vinaweza kuwa hasa vitu ambavyo vinatuelekeza kuja Kwake na kushikilia maagano yetu ili tuweze kurudi katika uwepo Wake na kupokea yale yote ambayo Baba anayo” (“Claim the Blessings of Your Covenants,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 119–20).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Hakikisha kwamba unafundisha mafundisho ya kweli. “Kila mara jiulize, ‘Ni kwa jinsi gani kile ninachofundisha kitawasaidia washiriki wa darasa langu kujenga imani katika Kristo, kutubu, kufanya na kushika maagano na Mungu, na kupokea Roho Mtakatifu?’” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20).

Chapisha