Mafundisho na Maagano 2021
Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48: “Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”


“Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48: ‘Takeni Sana Karama Zilizo Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
watu wakikutana karibu na dimbwi

Mkutano wa Kambi, na Worthington Whittredge

Mei 3–9

Mafundisho na Maagano 46–48

“Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 46–48, Roho Mtakatifu anaweza kukushuhudia kuhusu kweli katika sehemu hizi. Kuandika na kufanya mapitio ya misukumo kunaweza kukusaidia kupata mbinu za kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua kweli hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Inaweza kuwa yenye kusaidia kwa washiriki wa darasa kushiriki, mara kwa mara, jinsi kujifunza kwao injili kibinafsi na kifamilia kunavyoendelea. Kwa mfano, wakati washiriki wa darasa wanaposhiriki umaizi kuhusu kitu ambacho wao au mwanafamilia aligundua wiki iliyopita, unaweza kuwauliza kile walichokuwa wakifanya wakati wakijifunza ambacho kilivuvia umaizi huo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 46:1–7

Tunapaswa kuwakaribisha wote katika Kanisa la Yesu Kristo.

  • Kwa wengi, jinsi na namna wanavyohisi katika mikutano Kanisani kunaweza kushawishi kwa sehemu kubwa kushiriki kwao Kanisani. Maagizo ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 46:1–7 yanaweza kuwasaidia washiriki wa kata yako kuleta uzoefu wa ibada yenye mapokezi mazuri zaidi, na ya maana kwa kila mmoja na kwa ajili ya wageni. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari hii, wakitafuta kanuni zinazohusiana na mikutano ya Kanisa na kuorodhesha ubaoni kile wanachokipata. Kwa kila kipengele katika orodha, darasa linaweza kujadili namna ambavyo kanuni hiyo inatumika.

  • Ni kwa jinsi gani maagizo ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 46 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuona mikutano ya Kanisa kama fursa za kuhisi Roho Mtakatifu? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mafundisho na Maagano 46:2 na wajadiliane wakati ambapo wameshuhudia viongozi na walimu wakiongoza mikutano kwa Roho Mtakatifu. Ni nini wajibu wa wale wanaohudhuria mikutano? Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki nyakati walipohisi mkutano ukielekezwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu.

  • Labda ungeweza kuwaalika baadhi ya washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wao kuhusu wakati walipohudhuria mkutano wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa mara ya kwanza. Nini kiliwasaidia kuhisi mapokezi mazuri? Ni ushauri gani wangeweza kuwapa washiriki wengine ili kuifanya mikutano ya Kanisa kuwa yenye mapokezi mazuri zaidi? Tunawezaje kutumia ushauri wa Bwana unaopatikana katika Mafundisho na Maagano 46:1–7? Waruhusu washiriki wa darasa wafanye mazoezi ya kile ambacho wangesema ikiwa watamuona mgeni akiingia kanisani kwa mara ya kwanza.

  • Wimbo kama vile “’Tis Sweet to Sing the Matchless Love” (Nyimbo za Kanisa, na. 176 au 177) unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria kuhusu na kujadiliana jinsi ya kufanya mikutano yetu ya Kanisa kuwa yenye mapokezi mazuri zaidi na yenye kuinua. Labda washiriki wa darasa wanaweza kuimba wimbo pamoja na kushiriki mawazo kutoka kwenye maneno ya wimbo kuhusu jinsi ya kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Mungu Kanisani.

    Picha
    waumini kanisani

    Bwana alifundisha kwamba wote wanakaribishwa katika Kanisa Lake.

Mafundisho na Maagano 46:7–33

Baba wa Mbinguni anatoa vipawa vya roho kwa manufaa ya watoto Wake.

  • Watakatifu wa kale waliamini kwa dhati katika vipawa vya Roho Mtakatifu. Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuongeza imani yao kwamba vipawa hivi vinaweza kuonekana katika maisha yetu leo hii? Unaweza kuanza kwa kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mafundisho na Maagano 46:7–33 katika jozi au vikundi vidogo. Waombe watafute angalau vipawa vitano vya roho na wajadiliane jinsi ambavyo wameshuhudia vipawa hivyo vikidhihirika maishani mwao au katika maisha ya mtu ambaye wanamfahamu—ikiwa ni pamoja na watu walio darasani. Ni kipi walichokipata ambacho wanaweza kushiriki na darasa ili kujenga imani katika vipawa hivi.

  • Bwana alisema kwamba vipawa vya Roho vina manufaa kwa wale ambao ni waaminifu na “hawaombi kwa ishara” (mstari wa 9). Labda washiriki wa darasa wanaweza kujadiliana jinsi ambavyo vipawa vya roho huwasaidia waaminifu. Ni jinsi gani vipawa hivi vinaweza kuwasaidia wale wanaotaka kupata au kuimarisha ushuhuda wao wa injili?

  • Baadhi ya watu wanampenda Mungu na wanajaribu kushika amri Zake lakini hawahisi kuwa wamepata uzoefu wa vipawa vyovyote vya Roho. Ni jinsi gani ushauri katika Mafundisho na Maagano 46:7–33 unasaidia?

Mafundisho na Maagano 47

Roho Mtakatifu anaweza kutuongoza sisi wakati tunapotimiza miito yetu.

  • Watu wengi wanaweza kujihusisha na kile ambacho John Whitmer alihisi wakati alipohitaji kuondolewa shaka kwamba wito wake ulitoka kwa Mungu. Pengine washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu sawa na huo ambao wamekuwa nao. Tunapata nini katika Mafundisho na Maagano 47 ambacho kinaweza kuwa kilimpatia John Whitmer imani katika wito wake?

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajibu wako kama mwalimu. Kufundisha ni zaidi ya kuwasilisha taarifa ambayo umeitayarisha. Miongoni mwa vitu vingine, kunajumuisha kutengeneza mazingira ambapo washiriki wa darasa wanaweza kujifunza na kugundua kweli wao wenyewe na kushiriki kile ambacho wamejifunza pamoja na wengine. Kwa mfano, wakati wote wa somo, waulize washiriki wa darasa kuhusu uzoefu wao wa kusoma maandiko nyumbani.

Chapisha