Mafundisho na Maagano 2021
Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: “Kile Kilicho cha Mungu ni Nuru”


“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: ‘Kile Kilicho cha Mungu ni Nuru,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
dimbwi wakati wa machweo

Mei 10–16

Mafundisho na Maagano 49–50

“Kile Kilicho cha Mungu ni Nuru”

Ili “kulihubiri neno la kweli kwa njia ya Mfariji” (Mafundisho na Maagano 50:17), tafuta mwongozo wa kiungu unapotafakari Mafundisho na Maagano 49–50. Kisha kuwa tayari kufuata mwongozo wa Mungu unapofundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kwa kuongezea kwenye kushiriki umaizi waliopokea wakati wakijifunza maandiko, washiriki wa darasa wanaweza kufaidika kutokana na kujadili namna ambavyo umaizi huo huja. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki wao kwa wao umaizi kuhusu mstari katika Mafundisho na Maagano 49–50 na wajadili kile ambacho kiliwaelekeza kwenye umaizi huo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 49; 50:1–36

Kweli za injili zinaweza kunisaidia kutambua mafundisho ya uongo.

  • Sehemu ya 49 ilitolewa ili kuthibitisha mafundisho ya kweli ambayo yalirekebisha kile ambacho wengine walikuwa wakifundisha (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya maelezo ya kihistoria). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza sehemu hii, ungeweza kuwagawanya washiriki wa darasa katika vikundi na kukipangia kila kikundi mojawapo ya mada za mafundisho zilizojumuishwa (kama ilivyoorodheshwa katika kichwa cha habari cha sehemu ya 49). Vikundi hivyo vinaweza kujadiliana maswali yafuatayo: Ni kweli zipi Bwana alifundisha kuhusu mada hii katika sehemu ya 49? Ni nini watu wanaamini kuhusu mada hii leo? Ni kweli gani zingine ambazo Bwana amefundisha kuihusu kupitia manabii wetu wa siku za mwisho? Wape washiriki wa darasa nafasi ya kushiriki shukrani zao kwa ajili ya kweli zilizofunuliwa katika siku yetu?

  • Kama wazee waliokuwa kule Kirtland ambao “walikuwa hawaelewi kujionyesha kwa roho tofauti” (Mafundisho na Maagano 50, kichwa cha habari cha sehemu), wakati mwingine tunajiuliza ikiwa kitu tunachohisi au tunachoona kinatoka kwa Roho au kutoka kwenye ushawishi tofauti. Tunaweza kujifunza nini kutoka Mafundisho na Maagano 50:1–36 ili kutusaidia kutambua ushawishi wa Roho? Unaweza kumruhusu kila mshiriki wa darasa kuchagua vifungu vya mistari atakayojifunza na kisha waombe washiriki wa darasa kushiriki kile watakachopata.

Mafundisho na Maagano 49:15–17

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa mpango wa Mungu.

  • Kwa sababu ndoa ni muhimu kwa mpango wa Baba wa Mbinguni, Shetani ana hamu ya kusababisha mkanganyiko juu yake. Darasa lako linaweza kufaidika kutokana na kutengeneza orodha ubaoni ya kweli ambazo Bwana amefunua kuhusu ndoa. Kwa mfano, ni kweli zipi kuhusu ndoa tunajifunza kutoka Mafundisho na Maagano 49:15–17? Maandiko mengine yanayosaidia ni pamoja na Mwanzo 2:20–24; 1 Wakorintho 11:11; au mengine yanayopatikana katika “Ndoa, Oa” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wanaweza pia kupata kweli katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Kulingana na kile tunachojifunza kutoka kwenye nyenzo hizi, kwa nini ndoa baina ya mwanamume na mwanamke ni muhimu katika mpango wa Mungu? (ona “Nyenzo za Ziada”).

    Picha
    wanandoa nje ya hekalu

    Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.

Mafundisho na Maagano 50:13–22

Walimu na wanafunzi wanajengwa pamoja na Roho?

  • Maagizo ya Bwana kuhusu kuhubiri na kupokea ukweli yanaweza kutoa nafasi nzuri ya kujadili wajibu shirikishi wewe kama mwalimu na washiriki wa darasa mnao katika kuchochea kujifunza injili. Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kufanya mapitio ya Mafundisho na Maagano 50:13–22 katika jozi na kujadili majukumu ya Roho, walimu, na wanafunzi. Baadhi ya jozi zinaweza kushiriki na darasa kile walichojifunza. Ni zipi baadhi ya “njia zingine” sisi hujaribu wakati mwingine kufundisha au kujifunza injili? (mstari wa 17). Tunawezaje kuwa bora katika kupokea kwa Roho? Ni nini tunashawishika kufanya nyumbani kwetu na kanisani ili kufundisha na kujifunza injili vizuri zaidi?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Ndoa ni muhimu kwa mpango wa Baba wa Mbinguni.

Mzee David A. Bednar alieleza kwa nini ndoa ni muhimu kwa mpango wa Mungu wa wokovu.

“Kupitia mpango mtakatifu, wanaume na wanawake wamekusudiwa kuendelea pamoja kuelekea ukamilifu na utimilifu wa utukufu. Kwa sababu ya mienendo na uwezo wao bainishi, wanaume na wanawake kila mmoja analeta katika uhusiano wa ndoa mitazamo na uzoefu wa kipekee. Mwanamume na mwanamke huchangia kwa njia tofauti lakini kwa usawa katika umoja na ulinganifu ambao hauwezi kupatikana kupitia namna nyingine. Mwanamume humkamilisha mwanamke na mwanamke humkamilisha mwanamume wakifundishana na kuimarishana wao kwa wao na kubarikiana. …

“Nyumba yenye mume na mke mwenye upendo na mwaminifu ni mazingira ya upeo wa juu ambapo watoto wanaweza kulelewa kwa upendo na uadilifu na ambapo mahitaji ya watoto ya kiroho na ya kimwili yanaweza kutoshelezwa. Kama vile sifa za kipekee za wote wawili wanaume na wanawake zinavyochangia kwenye utimilifu wa uhusiano wa ndoa, ndivyo pia sifa hizo zilivyo muhimu kwa matunzo, malezi, na kufundisha watoto” (“Ndoa Ni Muhimu kwenye Mpango Wake wa Milele,” Ensign, Juni 2006, 83–84).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ongoza majadiliano yenye kutia moyo. Kila mtu ana jambo la kushiriki, lakini mara nyingine si kila mtu anapata nafasi. Kwa kufuata ushawishi wa Roho, tafuta njia za kuongeza idadi ya washiriki wa darasa ambao wanaweza kushiriki mawazo na hisia zao.

Chapisha