Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 26–Mei 2. Mafundisho na Maagano 45: “Ahadi … Zitatimizwa”


“Aprili 26–Mei 2. Mafundisho na Maagano 45–5: ‘Ahadi … Zitatimizwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 26–Mei 2. Mafundisho na Maagano 45,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
vijana nje ya hekalu

Aprili 26–Mei 2

Mafundisho na Maagano 45

“Ahadi … Zitatimizwa”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 45, fikiria kuhusu mistari ipi, dondoo kutoka kwa viongozi wa Kanisa, uzoefu, maswali, na nyenzo zingine ambazo waweza kutumia kufundisha mafundisho. Unapofundisha, waalike washiriki wa darasa waandike misukumo wanayopokea na watengeneze mpango wa kuifanyia kazi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wanaweza kuandika kwenye kipande cha karatasi namba ya mstari kutoka Mafundisho na Maagano 45 ambao uliwapa msukumo. Kisha unaweza kuzikusanya karatasi hizo, kuchagua chache pasi na utaratibu, na kuwaalika washiriki wa darasa walioandika wasome mistari yao kwa darasa na kushiriki ni kwa nini waliichagua. Wahimize wengine washiriki umaizi wao pia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 45:1–5

Yesu Kristo ndiye Mtetezi wetu kwa Baba.

  • Je, mtu katika darasa lako anaweza kuelezea kazi anayoifanya mtetezi? Inaweza kusaidia kuangalia maana ya mtetezi katika kamusi. Wakiwa na uelewa huu, washiriki wa darasa wanaweza kusoma Mafundisho na Maagano 45:3–5 katika jozi. Wanaweza kushiriki na wenzao maneno au virai vyovyote kutoka kwenye mistari hii ambavyo vinawasaidia kuelewa wajibu wa Yesu Kristo kama Mtetezi wetu kwa Baba. (Ona pia 2 Nefi 2:8–9; Mosia 15:7–9; Moroni 7:27–28; Mafundisho na Maagano 29:5; 62:1.) Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki hisia zao kuhusu Mwokozi kuwa Mtetezi Wao.

Mafundisho na Maagano 45:11–75

Hatuhitaji kuwa na hofu kwa sababu ya Ujio wa Pili.

  • Utawasaidia vipi washiriki wa darasa kuona vyote maonyo ya busara na ahadi zenye matumaini katika sehemu ya 45? Kwa mfano, unaweza kuandika kwenye ubao vichwa vya habari Unabii na Baraka Zilizoahidiwa, na washiriki wa darasa wanaweza kuandika chini ya vichwa hivi vya habari mafundisho wanayoyapata katika Mafundisho na Maagano 45:11–75. Kwa nini Bwana anatutaka tufahamu vitu hivi kabla? Je, tunaweza kufanya nini ili kupokea baraka zilizoahidiwa?

  • Labda washiriki wa darasa wanaweza kushauriana kuhusu namna ya kutegemea mazuri na kuwa na matumaini tunapokabiliana na majanga yaliyotabiriwa katika siku yetu (kama yale yaliyoelezewa katika Mafundisho na Maagano 45:11–75). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufokasi kwenye Ujio wa Pili kwa imani badala ya hofu, unaweza kuonesha video “Men’s Hearts Shall Fail Them” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa namna gani watu wanavunjika mioyo katika siku yetu? (ona mstari wa 26). Ni ushauri gani Rais Nelson alitoa katika video hii ili kutusaidia kukabiliana na hali za hofu kwa amani?

Mafundisho na Maagano 45:31–32

“Simameni katika mahali patakatifu,” na wala msiondoshwe.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kuwa radhi kushiriki umaizi wao kuhusu namna ambavyo wanajitahidi “kusimama katika mahali patakatifu,” kulingana na vile Bwana alivyoshauri katika Mafundisho na Maagano 45:31–32. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutengeneza mahali patakatifu katika maisha yetu? Kauli katika “Nyenzo za Ziada” na video “Stand Ye in Holy Places—Bloom Where You’re Planted” (ChurchofJesusChrist.org) vinaweza kuongeza umaizi katika mjadala huu.

    Picha
    wanawali kumi

    Fumbo la Wanawali Kumi, na Dan Burr

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

“Simameni katika mahali patakatifu.”

Dada Ann M. Dibb, mshiriki wa awali wa Urais Mkuu wa Wasichana, alifundisha kwamba maagizo ya kusimama mahali patakatifu na kutoondoshwa “yanaelezea jinsi tunavyoweza kupokea ulinzi, nguvu, na amani katika nyakati za kufadhaisha.” Baada ya kudokeza kwamba sehemu hizi takatifu zinaweza kuwa mahekalu, makanisa, na nyumbani, alisema kwamba “kila mmoja wetu anaweza kupata sehemu zingine nyingi.” Aliendelea:

“Tunaweza kwanza kuangalia neno mahali kama mazingira ya kimwili au eneo la kijiografia. Hata hivyo, mahali panaweza kuwa ‘hali ya kipekee, nafasi, au hali ya akili’ [Merriam-Webster.com Dictionary, “place,” merriam-webster.com]. Hii inamaanisha mahali patakatifu yaweza kuwa ni pamoja na muda mfupi katika wakati—nyakati ambazo Roho Mtakatifu anatushuhudia, nyakati ambazo tunahisi upendo wa Baba wa Mbinguni, au nyakati ambazo tunapokea majibu ya sala zetu. Hata zaidi, ninaamini kwamba wakati wowote unapokuwa na ujasiri wa kutetea haki, hasa katika hali ambazo hakuna mwingine aliye tayari kufanya hivyo, unatengeneza mahali patakatifu” (“Your Holy Places,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 115).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa ushuhuda ulio hai. Unapoishi mafundisho unayofundisha, utaweza kutoa ushuhuda wako binafsi, wenye nguvu kwamba ni ya kweli. Roho Mtakatifu atathibitisha ushuhuda wako kwenye mioyo ya washiriki wa darasa lako. Fikiria kanuni utakazokuwa ukifundisha wiki hii na katika majuma yajayo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuziishi kikamilifu? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13–14.)

Chapisha