Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: “Sheria ya Kulitawala Kanisa Langu”


“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44: ‘Sheria ya Kulitawala Kanisa Langu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 19–25. Mafundisho na Maagano 41–44,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

Picha
Yesu Kristo

Aprili 19–25

Mafundisho na Maagano 41–44

“Sheria ya Kulitawala Kanisa Langu”

Hamtaweza kujadiliana kama darasa kila kanuni inayofundishwa katika Mafundisho na Maagano 41–44. Tafuta msukumo kukusaidia kuchagua kanuni ambazo zitalifaa zaidi darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati ufunuo katika sehemu ya 42 ulichapishwa, Joseph Smith aliandika kwamba Watakatifu “waliupokea kwa furaha” (“Barua kwa Martin Harris,” Feb. 22, 1831, josephsmithpapers.org). Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki kitu chochote kutoka katika kujifunza kwao binafsi au kama familia wiki iliyopita ambacho walipokea kwa furaha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 41–42

Amri za Mungu hutawala Kanisa Lake na zinaweza kutawala maisha yetu.

  • Katika Mafundisho na Maagano 41, Bwana aliwasaidia Watakatifu kujitayarisha kupokea amri Zake, ambazo angefunua siku chache tu baadae. (ona sehemu ya 42). Ni kwa jinsi gani ufunuo katika sehemu ya 41 unaweza kuwa uliwasaidia Watakatifu kupokea amri za Mungu? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujibu swali hili, ungeweza kuwaalika kusoma Mafundisho na Maagano 41:1–6 na watafute kanuni ambazo zinaweza kutusaidia kupokea sheria ya Mungu. Tunawezaje kutumia kanuni hizi wakati tunazo nafasi za kupokea maagizo kutoka kwa Bwana?

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kugawanya sehemu ya 42 katika makundi matano ya mistari, ambayo kila mmoja unawakilisha kanuni muhimu ya injili. Makundi haya yanaweza kufanya iwe rahisi kwenu kuijadili sehemu hii kama darasa. Kwa mfano, unaweza kuandika marejeleo ubaoni na kumualika kila mshiriki wa darasa achague kundi moja. Waombe washiriki wa darasa kusoma mistari yao na kutafuta kitu ambacho wanahisi ni muhimu kwetu sisi katika siku ya leo. Wanaweza kushiriki mifano kutoka maishani mwao na kuonyesha jinsi tunavyobarikiwa wakati tunatawala maisha yetu kwa amri hizi.

Mafundisho na Maagano 41:9–11

Bwana huwaomba watumishi Wake watoe dhabihu.

  • Edward Partridge, askofu wa kwanza wa Kanisa la Urejesho, aliamriwa kuiacha kazi yake na “kutumia muda wake wote” akitumikia katika wito wake. Ingawaje hili halihitajiki kwetu sisi, ni nini tunakipata katika mistari hii ambacho kinaweza kutumika katika huduma yetu kwa Mungu? (Kwa zaidi kuhusu Edward Partridge, ona “Askofu wa Kanisa,” Ufunuo katika Muktadha, 77–83.)

Mafundisho na Maagano 42:61, 65–68; 43:1–7

Ufunuo huleta amani, shangwe, na maisha ya milele.

  • Kama viongozi wa Kanisa wa kale, washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa na maswali ambayo yanaonekana kama “siri” kwa sababu wanahitaji mwongozo kutoka kwa Bwana. Unaweza kuwahimiza waandike swali walilo nalo au shida ambayo wanahitaji kupata ufunuo wa binafsi. Tunapata nini katika Mafundisho na Maagano 42:61, 65–68 ambacho kinaweza kutusaidia tunapotafuta ufunuo?

  • Ili kuwasaidia washiriki kuelewa jinsi Mungu hutoa ufunuo kuliongoza Kanisa Lake, ungeweza kuwaalika kusoma Mafundisho na Maagano 43:1–7. Pia wangeweza kutazama video “Prophets and Revelation—Hearing His Voice” (ChurchofJesusChrist.org).

Mafundisho na Maagano 43:8–10

Tunakutana pamoja “kufundishana na kujengana sisi kwa sisi.”

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia Mafundisho na Maagano 43:8–10 kumfundisha mtu anayehisi kwamba siyo muhimu kwenda kwenye mikutano ya Kanisa? Orodha katika “Nyenzo za Ziada” inaweza ikasaidia kufokasi majadiliano haya kwa madhumuni matakatifu ya akidi ya ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama (orodha hiyo pia inatumika kwenye madarasa ya Wasichana). Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki jinsi kuchangia kwao katika akidi, Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, na madarasa ya Kanisa kumewabariki. Ni nini mistari ya 8–10 inamaanisha kuhusu kile tunachotakiwa kufanya ili kujiandaa na kushiriki katika mikutano?

    Picha
    Darasa la Shule ya Jumapili la vijana

    Kukutana kanisani ni njia mojawapo tunayoweza “kufundishana na kujengana sisi kwa sisi.”

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kwa nini tumepangwa katika akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi ya Akina Mama.

Dada Julie B. Beck, aliyekuwa Rais mkuu wa zamani wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alieleza kwa nini Mungu ametupanga katika akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi ya Akina Mama:

  1. “Kutupanga chini ya ukuhani na kulingana na mpangilio wa ukuhani.”

  2. Kuwaweka wana na mabinti wa Baba wa Mbinguni katika kazi ya wokovu na kuwahusisha katika kazi hiyo. Akidi na Muungano wa Usaidizi ya Akina Mama ni uanafunzi uliopangwa na wajibu wa kumsaidia Baba Yetu wa Mbinguni kusababisha maisha ya milele kwa ajili ya watoto Wake.

  3. Ili kuwasaidia maaskofu kusimamia ghala la Bwana. Ghala la Bwana linajumuisha ‘wakati, talanta, huruma, rasilimali, na uwezo wa kifedha’ wa washiriki wa Kanisa [Handbook 2: Usimamizi wa Kanisa, 6.1.3, ChurchofJesusChrist.org]. Talanta za Watakatifu zinapaswa kutumiwa kuwajali maskini na wenye shida na kujenga ufalme wa Bwana.”

  4. “Kutoa kinga na kimbilio kwa ajili ya watoto wa Baba wa Mbinguni na familia zao katika siku za mwisho.”

  5. “Kutuimarisha na kutusaidia katika wajibu wetu wa familia na majukumu kama wana na mabinti wa Mungu.” (“Kwa nini Tumepangwa katika Akidi na Miungano ya Usaidizi ya Akina Mama” [Ibada ya Brigham Young University, Jan. 17, 2012], speeches.byu.edu.)

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Alika. “Badala ya kutoa mialiko ya kufanya jambo fulani kila wakati, fikiria kuwaalika wanafunzi kufikiria kuhusu njia ambazo wanaweza kutumia kufanya yale ambayo wamejifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Chapisha