Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36: “Umeitwa Ili Kuhubiri Injili Yangu”


“Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36: ‘Umeitwa Ili Kuhubiri Injili Yangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Aprili 5–Aprili 11. Mafundisho na Maagano 30–36,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Wamisionari wa awali wa Kanisa

Aprili 5–Aprili 11

Mafundisho na Maagano 30–36

“Umeitwa Ili Kuhubiri Injili Yangu”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 30–36, ni jumbe gani zinaonekana muhimu kwa wale unaowafundisha? Ni nini kitawatia msukumo kushiriki injili na wengine?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kitu ambacho walisoma katika Mafundisho na Maagano 30–36 kushiriki injili.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 30–36

Tumeitwa kuhubiri injili ya Yesu Kristo.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kupekua Mafundisho na Maagano 30–36 kwa ajili ya kile Bwana Anachotaka kutoka kwa wamisionari Wake na kile Anachowaahidi. Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kile wanachokipata. (Ona, kwa mfano, Mafundisho na Maagano 30:8; 31:3–5; 32:1, 5; 35:24.) Labda ungeweza kuwaalika waandike barua kwa mtu anayehudumu misheni au anayejitayarisha kuhudumu misheni na ujumuishe baadhi ya maagizo na ahadi za Bwana.

  • Je, unawafundisha vijana wanaojitayarisha kuhudumu kama wamisionari? Kama ni hivyo, ungeweza kumwalika kila mshiriki wa darasa kupekua sehemu moja kutoka Mafundisho na Maagano 30–36 na kutafuta kitu kinachowatia msukumo kuhudumu. Unaweza kueleza kwamba wamisionari waliotajwa katika sehemu hizi walikuwa wageni na wasio na uzoefu mwingi Kanisani. Ni nini kiliwastahilisha kushiriki injili? Pia ungetaka kuonyesha mojawapo ya video iliyoorodheshwa katika “Nyezo za Ziada.” Ni nini video hizi zinapendekeza kuhusu sababu ya kuhudumu kama wamisionari na jinsi tunavyoweza kujitayarisha?

  • Siyo kila mtu ana nafasi ya kuhudumu misheni, lakini sote tunaweza kuwaalika wengine kuja kwa Kristo na kusikiliza ujumbe wa Urejesho. Washiriki wa darasa wangeweza kutengeneza orodha ya njia tofauti wanazoweza “kufumbua vinywa [vyao]” (Mafundisho na Maagano 33:8–10). Ni baadhi ya fursa zipi za kiuhalisia ambazo tunazo kwa ajili ya kushiriki shuhuda zetu na wengine? Ni ushauri gani katika Mafundisho na Maagano 30–36 hutumika katika kushiriki injili katika njia hizi? Fikiria kuwaomba baadhi ya washiriki wa darasa ambao wamekuwa na uzoefu chanya wa kushiriki injili washiriki mawazo yao na wajibu maswali ambayo darasa linaweza kuwa nayo.

  • Bwana alimuahidi Ezra Thayer na Northrop Sweet kwamba kama wangefumbua vinywa vyao kushiriki injili, wao “wangekuwa kama Nefi wa kale” (Mafundisho na Maagano 33:8). Ni sifa zipi Nefi alikuwa nazo ambazo zinaweza kuhusishwa na kushiriki injili? (ona, kwa mfano, 1 Nefi 3:7; 4:6; 10:17; 17:15; 2 Nefi 1:27–28). Ni kwa jinsi gani sifa hizi zinaweza kutusaidia katika juhudi zetu za kushiriki injili?

    Picha
    wamisionari wakifundisha

    Bwana anatuomba tuhubiri injili katika wakati wetu kama katika Kanisa la kale.

Mafundisho na Maagano 32–3335

Bwana hutuandaa sisi kwa kazi ambayo Yeye anataka tufanye.

  • Ni kwa jinsi gani Bwana ametusaidia kuifanya kazi Yake? Mjadala kuhusu maisha ya watu walioelezewa katika Mafundisho na Maagano 32–3335 waweza kuwa mahali pazuri pa kuanzia kwa ajili ya kutafakari uzoefu huu. Kwa mfano, unaweza kushiriki na darasa historia ya ono la Ezra Thayer katika “Nyenzo za Ziada” na kisha uwaalike washiriki wa darasa wasome Mafundisho na Maagano 33:1–13, ambayo ni sehemu ya ufunuo kwa ajili ya Ezra Thayer. Ni kwa jinsi gani Bwana alikuwa akimuandaa Ezra kwa ajili ya kazi Bwana aliyomtaka atimize? (ona Mafundisho na Maagano 33:2). Ungeweza pia kumuomba mshiriki wa darasa ashiriki taarifa ya usuli kuhusu uhusiano baina ya Parley P. Pratt na Sidney Rigdon (ona “Voices of the Restoration: Early Convert Testimonies” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Ni kwa jinsi gani uhusiano huu ulibariki Kanisa? Je, ushahidi gani tunaouona kwamba mkono wa Bwana ulikuwa katika maisha ya watu hawa? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao uliwasaidia wao kuona kwamba Bwana aliwafahamu kwa njia sawa na hiyo.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Ono la Ezra Thayer.

Ezra Thayer aliandika kwamba muda kidogo kabla ya yeye kubatizwa, alipata ono na katika ono hilo “mtu alikuja na kuniletea karatasi lililokunjwa na kuliwasilisha kwangu, na tarumbeta na kuniambia [niicheze]. Nilimwambia kwamba sikuwahi [kucheza] chombo chochote maishani mwangu. Alisema unaweza [kuicheza], jaribu. … Ilitoa sauti nzuri sana ambayo nilikuwa nimewahi kusikia” (“Revelation, October 1830–B, Revelation Book 1,” historical introduction, josephsmithpapers.org). Wakati Joseph Smith baadaye alipokea ufunuo kwa ajili ya Ezra Thayer na Northrop Sweet, ulionakiliwa sasa kama Mafundisho na Maagano 33, Ezra alifafanua ufunuo huo kama lile karatasi lililokunjwa katika ono lake.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza mazingira yenye heshima. “Wasaidie washiriki wa darasa lako kuelewa kwamba kila mmoja wao anaathiri roho ya darasa. Wahimize wakusaidie kujenga mazingira yaliyo wazi, ya upendo, na heshima ili kwamba kila mtu ajisikie yuko salama kushiriki uzoefu, maswali, na ushuhuda wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,15).

Chapisha