“Machi 29–Aprili 4. Pasaka: “Mimi Ni Yeye Aliye Hai, Mimi Ni Yule Aliyeuawa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Machi 29–Aprili 4. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Machi 29–Aprili 4
Pasaka
“Mimi Ni Yeye Aliye Hai, Mimi Ni Yule Aliyeuawa”
Hakuna kilicho muhimu zaidi kwetu sisi kuelewa kuliko Upatanisho wa Yesu Kristo. Fikiria kuhusu watu ambao watakuwa wakihudhuria darasa lako; nini kitawasaidia kikamilifu ili wawe na imani katika Yesu Kristo?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wakati washiriki wa darasa lako wamejifunza Mafundisho na Maagano mwaka huu, wanaweza kuwa wamepata vifungu ambavyo ni vya maana kwao. Anza darasa kwa kuwapa nafasi za kushiriki vifungu hivi. Ni kwa jinsi gani kujifunza kwako Mafundisho na Maagano kufikia sasa kumeimarisha imani yako katika Yesu Kristo?
Fundisha Mafundisho
Yesu Kristo alitimiza “upatanisho kamili.”
-
Kwa sababu Upatanisho wa Yesu Kristo ni fundisho muhimu sana, fikiria kutumia wakati wa kutosha kuhakikisha kwamba washiriki wa darasa wanalielewa. Ili uweze kufanya hivi, unaweza ukaandika ubaoni maswali kama haya: Upatanisho wa Yesu Kristo ni nini? Ni kwa jinsi gani unaathiri maisha yangu ya kila siku? Ni kwa namna gani unaathiri maisha yangu ya milele? Nawezaje kupokea nguvu za Mwokozi za ukombozi maishani mwangu? Wape washiriki wa darasa dakika chache ili watafakari maswali haya na kutafuta maandiko ambayo yanasaidia kuyajibu. Washiriki wa darasa wangeweza kuandika marejeleo yao ya maandiko ubaoni, na mngeweza kujadili baadhi yake kama darasa. Hii ni baadhi ya mifano: Luka 22:39–44; 1 Yohana 1:7; 2 Nefi 2:6–9; Mosia 3:5–13, 17–18; Alma 7:11–14; Moroni 10:32–33; Mafundisho na Maagano 19:16–19; 45:3–5.
-
Yaweza kuwa ya manufaa kwa washiriki wa darasa kutazama video “The Savior Suffers in Gethsemane” (ChurchofJesusChrist.org) kabla ya kusoma maneno ya Mwokozi Mwenyewe kuhusu Mateso Yake katika Mafundisho na Maagano 19:16–19. Ni kwa jinsi gani mistari hii inaongeza kwa kina shukrani zetu kwa ajili ya dhabihu ya Yesu Kristo? Video zingine za Pasaka ambazo unaweza kushiriki zimeorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.”
Mafundisho na Maagano 76:11–14, 20–24; 110:1–10
Nabii Joseph Smith alishuhudia kuwa Yesu Kristo yu hai.
-
Joseph Smith alimuona Mwokozi aliyefufuka na akatoa ushuhuda wenye nguvu kwamba Yesu Kristo yu hai. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza ushuhuda wa Joseph Smith, ungeweza kuwagawanya katika vikundi viwili na kukipangia kila kikundi kusoma Mafundisho na Maagano 76:11–14, 20–24 au 110:1–10. Waalike washiriki wa darasa kutafuta angalau neno moja katika mistari hii ambalo linaeleza kuhusu Mwokozi. Washiriki wa darasa wanaweza kuchukua zamu kuandika maneno waliyoyapata ubaoni, na unaweza kuyatumia maneno haya kuongoza mjadala kuhusu sifa na nguvu za Mwokozi. Ni kwa jinsi gani ushuhuda wa Joseph Smith unaimarisha imani yetu katika kazi takatifu ya Yesu Kristo?
-
Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamehusisha mafundisho katika Mafundisho na Maagano na maneno na kanuni katika wimbo wa injili “I Know That My Redeemer Lives” (Nyimbo za Injili, na. 136; ona mwongozo wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Labda wangekuwa tayari kushiriki kile walichogundua. Pia mngeweza kusoma au kuimba wimbo huu kama darasa na mtafute uhusiano katika maandiko yafuatayo: Mafundisho na Maagano 6:34; 45:3–5; 84:77; 98:18; 138:23. Ni kwa jinsi gani tumekuja kujua ya kwamba Mkombozi wetu yu hai?
Mafundisho na Maagano 29:26–27; 42:45–46; 63:49; 88:14–17, 27–31; 93:33–34
Kwa sababu ya Yesu Kristo, tutafufuliwa.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kile ambacho Mafundisho na Maagano hufundisha kuhusu ufufuo, ungeweza kuwaalika kufikiria kwamba rafiki au mwanafamilia anauliza nini maana ya kufufuliwa. Tunaweza kumsaidia vipi mtu huyo kuelewa ufufuo ni nini? Watie moyo washiriki wa darasa kupekua Mafundisho na Maagano 88:14–17, 27–31 kwa ajili ya kitu kinachoweza kusaidia. Marejeleo mengine ya maandiko yanayoweza kuwa ya manufaa ni pamoja na Alma 11:40–45 na Alma 40:21–23. Ni nini tunaweza tukashiriki ili kumsaidia rafiki au mwanafamilia ahisi furaha na tumaini ambalo huja kutokana na fundisho la ufufuo.
-
Unawezaje kuwasidia washiriki wa darasa kutafakari karama ya Mwokozi ya ufufuo? Pengine ungeweza kuandika ubaoni Kwa Sababu ya Yesu Kristo … na kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta maneno yanayoweza kukamilisha kirai hiki toka vifungu vifuatavyo: Mafundisho na Maagano 29:26–27; 42:45–46; 63:49; 93:33–34. Je, ni kwa jinsi gani kweli katika mistari hii zinaathiri mtazamo wetu wa kifo? Ni kwa jinsi gani zinaathiri maisha yetu ya kila siku?