Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105: “Baada ya Taabu Nyingi … Huja Baraka”


Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105: ‘Baada ya taabu Nyingi … Huja Baraka,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

Septemba 13–19. Mafundisho na Maagano 102–105,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

wanaume wakiwa na mikokoteni

C. C. A. Christensen (1831–1912), Kambi ya Sayuni, c. 1878, tempera kwenye kitambaa cha pamba, inchi 78 × 114. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, zawadi ya wajukuu wa C. C. A. Christensen, 1970

Septemba 13–19

Mafundisho na Maagano 102–105

“Baada ya Taabu Nyingi … Huja Baraka”

Unapojiandaa kufundisha Mafundisho na Maagano 102–5, sikiliza ushawishi wa Roho. Anaweza kukuongoza kwenye kanuni ambazo hazijatajwa kwenye muhtasari huu ambazo zitawabariki watu unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wangeweza kunakili mstari mmoja au miwili kutoka kwenye Mafundisho na Maagano 102–5 ambayo ni muhimu kwao. Kisha wangeweza kubadilishana mistari na mshiriki mwingine wa darasa na kujadiliana walichojifunza kutoka kwenye kila mstari.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 103;105

Majaribu yetu yanatufundisha masomo muhimu na kutupa uzoefu.

  • Washiriki wa darasa walipokuwa wakisoma sehemu ya 103 na 105 wiki hii, yawezekana wamepata kanuni ambazo zinaweza kusaidia nyakati za majaribu au upinzani; acha waelezee walichokipata. Au ungeweza kuwaalika watafute kanuni kama hizo kwenye Mafundisho na Maagano 103:5–7, 12, 36; 105:5–6, 9–12, 18–19 (ona pia “Nyenzo za Ziada”). Kanuni hizi hupendekeza nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuitikia wakati tunapokumbana na magumu au kukatishwa tamaa? Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wako tayari kushiriki uzoefu ambapo baraka zilikuja “baada ya taabu nyingi” (Mafundisho na Maagano 103:12).

  • Kama unahisi kwamba baadhi ya hadithi za kihistoria au hadithi binafsi kuhusu Kambi ya Sayuni zingeweza kufaa, unaweza kumwalika mtu kufanya marejeo ya mojawapo ya nyenzo zifuatazo kabla ya kuanza darasa na kwa ufupi aelezee kile walichojifunza: Watakatifu, 1:194–206; “The Acceptable Offering of Zion’s Camp” (Ufunuo katika Muktadha, 213–18); au “Sauti za Urejesho: Kambi ya Sayuni” (katika muhtasari wa wiki hii kwenye Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Ikiwa tungeweza kurudisha wakati nyuma na kuongea na Kambi ya Sayuni, je, nini tungekisema ili kuwatia moyo? Je, wangesema nini ili kututia moyo?

    mto mdogo

    Kambi ya Sayuni iliishi kandokando ya kingo za Mto Mdogo wa Uvuvi, uonekanao hapa kwenye picha.

Mafundisho na Maagano 104:11–18

Kila mmoja wetu ni “msimamizi wa baraka za kidunia.”

  • Ili kusaidia washiriki wa darasa kuishi mafundisho kutoka Mafundisho na Maagano 104:11–18, ungeweza kuwaalika kuchukulia kwamba walikuwa wakienda kukabidhi kitu chenye thamani ili kitunzwe na mtu fulani. Wangesema nini kwa mtu huyo? Wangetarajia nini kutoka kwake? Kisha washiriki wa darasa wangeweza kusoma Mafundisho na Maagano 104:11–18 ili kugundua kile ambacho Bwana amekikabidhi kwetu na kile anachokitarajia kutoka kwetu. Ni kwa namna ipi mistari hii inaweza kuathiri namna tunavyofikiria kuhusu ulimwengu, baraka zetu, au watu wanaotuzunguka?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufahamu vyema “ile njia ambayo … Bwana [ameazimia] kutoa mahitaji ya watakatifu [Wake]” (Mafundisho na Maagano 104:16), fikiria kuonesha video ya “The Labor of His Hands” (ChurchofJesusChrist.org). Kulingana na tunachojifunza kutoka kwenye video hii na Mafundisho na Maagano 104:11–18, je, Bwana hutumia njia ipi kuwabariki Watakatifu Wake? Pia unaweza kushiriki maneno haya ya Rais Marion G. Romney: “Bwana … angeweza kutunza [masikini] bila usaidizi wetu kama lingekuwa lengo lake kufanya hivyo. … Lakini sisi tunahitaji uzoefu huu; kwa kuwa ni kupitia tu kujifunza kwetu juu ya namna ya kutunzana ndipo tunajenga ndani yetu upendo na tabia zinazofanana na za Kristo zinazostahili kutuwezesha kurudi katika uwepo wake” (“Kuishi Kanuni za Ustawi,” Ensign, Nov. 1981, 92). Wape washiriki wa darasa dakika chache za kuandika misukumo yao kuhusu jinsi wanavyoweza kuwasadia wengine katika njia ya Bwana.

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Nguvu itakasayo ya majaribu.

Mzee Orson F. Whitney alifundisha: “Hakuna maumivu ambayo tunayapata, hakuna majaribu ambayo tunayapitia ambayo ni bure. Huongezea katika elimu yetu, katika kukuza sifa kama vile subira, imani, ustahimilivu, na unyenyekevu. Yale yote tutesekayo na yale yote tuvumiliayo, hasa wakati tuvumiliapo kwa subira, hujenga sifa yetu, hutakasa mioyo yetu, hupanua nafsi zetu, na hutufanya sisi kuwa wapole sana na wenye hisani, wastahiki zaidi kuitwa watoto wa Mungu … na ni kupitia huzuni na kuteseka, kusumbuka, taabu, kwamba tunapata elimu ambayo tulikuja hapa kuipata na ambayo itatufanya sisi kuwa kama Baba yetu na Mama yetu aliye mbinguni” (katika Spencer W. Kimball, Imani huanza kabla ya Miujiza [1972], 98).

Mzee David A. Bednar alisema: “Katika kiwango Fulani katika kila maisha yetu, tutaalikwa ili kutembea katika Kambi yetu ya Sayuni. Muda wa mialiko utatofautiana, na vikwazo husika ambavyo tunaweza kukumbana navyo katika safari vitakuwa tofauti. Lakini mwitikio wetu endelevu katika mwito huu hatimaye utatoa jibu la swali Je, nani yu upande wa Bwana?’” (“Upande wa Bwana: Masomo kutoka Kambi ya Sayuni,” Ensign, Julai 2017, 35).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fanya kazi pamoja na wanafamilia. “Kwa sababu nyumbani ni mahali muhimu pa kujifunza na kuishi injili, juhudi zako za kumuimarisha mshiriki wa darasa zitakuwa za ufanisi zaidi wakati unaposhirikiana na … wanafamilia [yake]” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8–9).