Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97: “Kwa ajili ya Wokovu wa Sayuni”


Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97: ‘Kwa ajili ya Wokovu wa Sayuni,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

Agosti 30–Septemba 5. Mafundisho na Maagano 94–97,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland, na Al Rounds

Agosti 30–Septemba 5

Mafundisho na Maagano 94–97

“Kwa ajili ya Wokovu wa Sayuni”

Je, unawezaje kuwasaidia vyema zaidi washiriki wa darasa kuwa na hamu ya kupokea baraka zilizoahidiwa katika Mafundisho na maagano 94–97?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuelezea kitu ambacho walikipata katika Mafundisho na Maagano 94–97 ambacho kiliwahamasisha kwenda hekaluni mara kwa mara. Au wangeweza kuelezea ujumbe mwingine ambao uliwahamasisha wao walipokuwa wakisoma sehemu hizi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 95:8; 97:10–17

Katika hekalu Mungu huwabariki watu Wake.

  • Ungewezaje kutumia ukweli uliofundishwa katika Mafundisho na Maagano 95 na97 ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kutafuta Baraka za hekaluni kwa bidii zaidi? Njia mojawapo ni kuweka picha ya hekalu katikati ya ubao na kuwauliza washiriki wa darasa ni kwa nini wanafikiri Bwana huwaamuru Watakatifu Wake kujenga mahekalu. Washiriki wa darasa wangetafuta majibu machache kutoka Mafundisho na Maagano 95:8; 97:10–17 na kuandika walichokipata ubaoni kuzunguka picha ya hekalu. (Wanaweza kupata majibu zaidi katika “Kwa nini Watakatifu wa Siku za Mwisho Hujenga Mahekalu” [temples.ChurchofJesusChrist.org].) Je, ni kwa namna gani malengo haya yametimizwa katika maisha yetu? Tunawezaje kuliweka hekalu kuwa sehemu muhimu zaidi ya maisha yetu?

  • Kanisa hutoa nyenzo mbalimbali zinazofundisha kuhusu mahekalu. Fikiria jinsi ambavyo ungeweza kutumia baadhi ya hizo kuimarisha mjadala wa darasa kuhusu Mafundisho na Maagano 95 na 97 na kuwahamasisha washiriki wa darasa kutafuta baraka za hekalu kwa bidii zaidi. Kwa mfano, kabla ya darasa ungeweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa ili kurejea hizi nyenzo kwenye temples.ChurchofJesusChrist.org au Temples of The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (toleo maalumu la Ensign au Liahona, Okt. 2010). Waombe washiriki wa darasa kuja wakiwa wamejiandaa kuelezea kitu walichojifunza ambacho kinaunga mkono mafundisho yaliyo katika sehemu ya 95 na 97.

    Ikiwa unawafundisha vijana, ungeweza kuwaalika kusoma “Kufanya Hekalu Kuwa Sehemu ya Maisha Yako” (katika Mahekalu ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 77–78) na waelezee jinsi wanavyolipa hekalu kipaumbele maishani mwao.

    Video “Two Apostles Lead a Virtual Tour of the Rome Italy Temple” and “Temples” (ChurchofJesusChrist.org) zinaweza kuwasaidia wale wanaojiandaa kwenda hekaluni.

    Mngeweza pia kuimba kwa pamoja wimbo kuhusu mahekalu na kujadili kile unachofundisha (angalia kielelezo cha mada katika Nyimbo za Kanisa).

Mafundisho na Maagano 97:8–9

Tunaweza kukubalika na Bwana.

  • Je, tunajifunza nini kutoka kwenye Mafundisho na Maagano 97:8 kuhusu kile inachomaanisha kukubaliwa na Bwana? Hilo hutofautiana vipi na jinsi wakati mwingine sisi tunavyotafuta kukubaliwa na dunia? Je, ni baraka gani zimeahidiwa katika mstari wa 9 kwa wale waliokubaliwa na Bwana? Washiriki wa darasa wangeweza pia kurejelea ujumbe wa Mzee Erich W. Kopischke “Kukubaliwa na Bwana” (Ensign au Liahona, Mei 2013, 104–6) na kuelezea jinsi ujumbe huo unavyowasaidia kuelewa mistari hii. Maneno katika “Nyenzo za Ziada” yanahusisha mwaliko wa Mzee Kopischke wa kutafuta kukubaliwa na Bwana maishani mwetu.

Mafundisho na Maagano 97:18–28

Sayuni ni “walio safi moyoni”.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kufikiria kuhusu Sayuni ni nini, ungeweza kuandika ubaoni Sayuni ni nini? na waalike kutafuta majibu katika Mafundisho na Maagano 97:19 na 21 (ona pia Musa 7:18; Mada za Injili, “Zion,” topics.ChurchofJesusChrist.org). Ingeweza kusaidia kujadili jinsi Mwokozi anavyotusaidia kuwa “wasafi moyoni.” Ni nini ambacho tunahisi kuhamasika kukifanya ili kujenga Sayuni maishani mwetu? Katika kata zetu au tawi? katika jumuiya yetu?

    Picha
    Hekalu la Kirtland

    Kujenga Hekalu la Kirtland kuliwafanya watakatifu “kuwa watakatifu zaidi mioyoni.”

  • Bwana alifundisha kuhusu Sayuni baada ya kwanza kuwaamuru Watakatifu kujenga hekalu “kwa ajili ya wokovu wa Sayuni” (ona Mafundisho na Maagano 97:12, 18–28). Kwa nini hekalu ni sehemu muhimu ya kujenga Sayuni? Je, ni kwa namna gani ahadi alizofanya Bwana juu ya Sayuni katika mistari 18–28 zinatimizwa katika siku yetu?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kukubalika na Bwana.

Kwa kurejelea kwenye “mfumo rahisi” unaofundishwa kwenye Mafundisho na Maagano 97:8, Mzee Erich W. Kopischke alifundisha:

“Kutafuta na kupokea kukubaliwa na Bwana kutaongoza kujua kuwa tumeteuliwa na kubarikiwa Naye. Tutapata imani zaidi kuwa atatuongoza na kutuelekeza katika mazuri. Fadhili zake nyororo zitadhihirika mioyoni mwetu, maishani mwetu, na katika familia zetu.

“Kwa moyo wangu wote ninawaalika kutafuta kukubaliwa na Bwana na kufurahia baraka zake zilizoahidiwa. Tunapofuata mpangilio rahisi ambao Bwana ameuweka wazi, tutakuja kujua kwamba tunakubaliwa Kwake, bila kujali vyeo vyetu, hali, au mapungufu yetu ya kimwili” (“Kukubaliwa na Bwana,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 106).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Pata kuwajua wale unaowafundisha. Kila mtu unayemfundisha ana uzoefu, mitazamo na talanta za kipekee. Omba ili ujue jinsi mchango wa kila mtu unavyoweza kuwa baraka kwa darasa zima. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7.)

Chapisha