Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: “Kupokea Utimilifu Wake”


“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: ‘Kupokea Utimilifu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

Stefano anamuona Mungu na Yesu Kristo

Namuona Mwana wa Mtu Amesimama Mkono wa Kuume wa Mungu, na Walter Rane

Agosti 23–29

Mafundisho na Maagano 93

“Kupokea Utimilifu Wake”

Watu unaowafundisha ni wana na mabinti wa thamani wa kiroho wa Wazazi wa Mbinguni na wanao uwezekano wa kiungu. Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 93, je ni kitu gani unajisikia kuhamasika kufanya ili kuwasaidia wao kukua katika “nuru na kweli”? (mstari wa 36).

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika ubaoni katika Mafundisho na Maagano 93,Yesu Kristo alitualika ku … Waalike washiriki wa darasa kupendekeza njia ambazo wangezitumia kukamilisha sentensi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 93

Joseph Smith alimuona Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.

  • Katika kujifunza kwao Mafundisho na Maagano 93, washiriki wa darasa pengine walipata ukweli mwingi kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Waalike washiriki wa darasa kuelezea kile walichokipata. Pia ungeweza kuligawa darasa katika makundi na kulipa kila kundi vifungu kadhaa kujifunza pamoja. Kisha kila kikundi kingeweza kushiriki na darasa kile walichojifunza kuhusu “jinsi ya kuabudu, na … nini [tuna] kiabudu” (mstari wa 19).

Mafundisho na Maagano 93:1–39

Tunaweza “kupokea utimilifu wa [ Mungu], na kutukuzwa.”

dirisha la kioo

Tunapokea nuru ya Mungu tunaposhika amri zake na kujifunza kutoka Kwake.

  • Mafundisho na Maagano 93 ina ukweli mwingi kuhusu asili yetu ya milele na uwezekano wetu kama watoto wa Mungu. Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamegundua ukweli huu wakati wa kujifunza kwao sehemu ya 93 nyumbani (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Wale waliojifunza wangeweza kushiriki kile walichokipata, na mngeweza kugundua kweli zingine kama darasa. Ni kwa namna gani kweli hizi zingeathiri jinsi tunavyowachukulia watu wanaotuzunguka—au sisi wenyewe?

  • Hapa kuna njia nyingine ya kujifunza kuhusu uhalisia wetu wa milele na uwezo: washiriki wa darasa wangeweza kusoma pamoja mstari wa 24 na kuandika ubaoni vichwa vya habari vitatu Tulivyo, Tulivyokuwa, na Tutakavyokuwa. Kisha ungeweza kuligawa darasa katika makundi matatu na kuliomba kila kundi kuchunguza Mafundisho na Maagano 93:6–39, wakitafuta kweli kuhusu hali yetu ya sasa, iliyopita, au ijayo ya utambulisho wa milele. Kila kundi lingeweza kuandika chini ya vichwa vya habari kile walichokipata. Ni kwa jinsi gani ukweli huu huathiri chaguzi tunazofanya?

Mafundisho na Maagano 93:40–50

Tumeamriwa “kupanga nyumba [yetu].”

  • Amri ya “kupanga nyumba yako mwenyewe” (mstari wa 43) sio kuhusu kupanga makabati na vyumba vya faragha ila kuhusu kufundisha—na kujifunza—“nuru na kweli” (mstari wa 42). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuelezea jinsi wanavyojaribu kufuata ushauri huu. Ni changamoto zipi wanazokumbana nazo? Ni ukweli upi au kanuni zipi katika Mafundisho na Maagano 93 zinaweza kusaidia?

  • Kama sehemu ya mjadala wako kwa mistari hii, washiriki wa darasa wangeweza kusoma sehemu za ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Nyumbani Ambako Roho wa Bwana Anaishi” (Ensign au Liahona, Mei 2019, 22–25) na elezea utambuzi wowote unaohusiana na ukweli katika Mafundisho na Maagano 93:40–50. (Tazama pia maelezo katika “Nyenzo za Ziada.”)

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

“Kwamba wawe wenye bidii zaidi na kuwajibika nyumbani.”

Mzee David A. Bednar alifundisha:

“Katika ofisi yangu kuna mchoro maridadi wa shamba la ngano. Mchoro huo ni mkusanyiko mkubwa wa alama—ambazo hakuna ambayo ikiwa peke yake inavutia wala kupendeza. Kwa kweli, ukisimama karibu na mchoro, yote unayoweza kuona ni wingi wa mistari ya njano na ya rangi ya dhahabu na kahawia ambayo inaonekana kutohusiana na kutovutia. Hata hivyo, unaposogea taratibu mbali na picha hiyo, kila mpako wa rangi moja inajumuishwa na zingine na kuzaliwa mazingira ya kupendeza ya shamba la ngano. Nyingi ya alama za kawaida, kila moja hufanya kazi pamoja ili kuumba mchoro unaovutia na maridadi.

“Kila sala ya familia, kila sehemu ya kujifunza maandiko kwa familia, na kila jioni ya familia nyumbani ni alama kwenye mchoro wa nafsi zetu. Hakuna tukio moja linaloweza kuonekana kuwa la kuvutia sana ama la kukumbukwa. Lakini kama vile tu alama za rangi zinavyokamilishana vyema na kuzalisha picha inayovutia, ndivyo pia msimamo wetu wa kufanya mambo yanayoonekana kuwa madogo unavyoweza kusababisha matokeo muhimu ya kiroho. ‘Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu” (M&M 64:33). Uaminifu ni kanuni muhimu tunapoweka msingi wa kazi kuu katika maisha yetu binafsi na tunapofanyika kuwa wenye bidii na kuwajibika katika nyumba zetu wenyewe” (“Wenye Bidii Zaidi na Kuwajibika Nyumbani,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 19–20).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Onesha upendo. “Kulingana na hali yako, kuonesha upendo kwa wale unaowafundisha yaweza kumaanisha kuwapongeza kwa dhati, kutaka kujua hali ya maisha yao, kuwasikiliza kwa makini, kuwashirikisha katika somo, kufanya vitendo vya huduma kwa ajili yao, au kuwasalimia tu kwa furaha unapowaona” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,6).