Mafundisho na Maagano 2021
Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: “Nguvu za Uchamungu”


“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: ‘Nguvu za Uchamungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Joseph Smith akipewa Ukuhani wa Melkizedeki

Urejesho, na Liz Lemon Swindle

Julai 26–Agosti 1

Mafundisho na Maagano 84

“Nguvu za Uchamungu”

Utafanya nini kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza walipokuwa wakisoma Mafundisho na Maagano 84?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kushiriki na mshiriki mwingine wa darasa ukweli ambao waliupata katika sehemu ya 84 ambao uliwatia msukumo au uliwasaidia kuelewa vizuri zaidi ukuhani wa Mungu. Kisha alika baadhi kushiriki pamoja na darasa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 84:1–5, 17–28, 31–42

Sisi sote tunaweza kufikia nguvu ya ukuhani na baraka za Mungu.

  • Bwana anafungua “ufunuo huu kuhusu ukuhani” (Mafundisho na Maagano 84, kichwa cha habari cha sehemu) kwa kufundisha kwamba hekalu litajengwa Sayuni (ona mistari ya 1–5). Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa uhusiano baina ya malengo matakatifu ya hekalu na ukuhani? Unaweza kuanza kwa kuandika swali kwenye ubao kama hili Ni nini malengo ya ukuhani? Na kisha kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta majibu katika Mafundisho na Maagano 84:17–28, 31–42. Ni kwa jinsi gani mahekalu na ibada za hekaluni husaidia kukamilisha malengo haya?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa waelewe nguvu ambazo ukuhani unaweza kuwa nazo katika maisha yao, unaweza kuwaomba wasome Mafundisho na Maagano 84:17–28 na wafikirie namna ambavyo maisha yao yangekuwa tofauti bila ukuhani wa Mungu. Wahimize kushiriki ni kwa nini wana shukrani kwa ajili ya ukuhani, pamoja na uzoefu ambao wamekuwa nao kwenye nguvu za ukuhani—katika familia zao, miito, au maisha yao binafsi. Tunawezaje kupata uwezo wa nguvu ya ukuhani?

  • Kiapo na agano la ukuhani (ona Mafundisho na Maagano 84:31–42) kina maana maalum kwa wale waliotawazwa kwenye ofisi ya ukuhani. Lakini nyingi za baraka zilizoahidiwa katika mistari hii zinapatikana kwa wote. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi ahadi hizi zinavyowafaa, unaweza kuwaalika wasome mistari 33–42 na mzungumze kuhusu njia ambazo tunaweza “kupokea” ukuhani (mstari wa 35), watumishi wa Bwana, na Bwana. Pia wanaweza kusoma kauli katika “Nyenzo za Ziada” kugundua kile tunachohitaji kufanya kupokea baraka za ukuhani. Unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria kuhusu nini kinaweza kujumuishwa katika “yote Baba aliyonayo” (mstari wa 38), kama vile sifa zake na maisha Anayoishi. Ni kipi kingine kinatufurahisha kuhusu mistari na kauli hizi?

    Picha
    mwanamke akipokea sakramenti

    Ibada za ukuhani hubariki watoto wote wa Mungu.

Mafundisho na Maagano 84:61–88

Bwana atawaidhinisha wale wanaomtumikia.

  • Huku mistari hii ikiwalenga wale ambao “watakwenda na kuhubiri injili hii ya ufalme” (mstari wa 80), nyingi za kanuni zilizo ndani yake zinaweza kumfaa mtu yeyote anayemtumika Mungu. Unaweza kumpa kila mshiriki wa darasa sehemu ya Mafundisho na Maagano 84:61–88 asome na kuwaomba kushiriki na mshiriki mwingine wa darasa kile ambacho walijifunza ambacho kinaweza kumfaa yeyote anayemtumikia Bwana. Washiriki wa darasa wanaweza kuchagua mstari wanaoupenda au vifungu vya mistari kwa ajili ya kuvikariri au kuvibandika mahali ambapo wataviona kila siku. Je, ni ahadi gani ambazo wanazifurahia zaidi? Ni nini tunaweza kushiriki kutoka kwenye mistari hii ili kuwatia msukumo wamisionari wanaotumikia kwa sasa au wale wanaojitayarisha kutumikia?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Wote wanaweza kupokea yote aliyonayo Baba.

Rais M. Russell Ballard alifundisha: “Wote ambao wamefanya maagano matakatifu na Bwana na wanaoheshimu maagano hayo wanastahili kupokea ufunuo binafsi, kubarikiwa na huduma ya malaika, na kuzungumza na Mungu, kupokea utimilifu wa injili, na, hatimaye, kuwa warithi ubavuni mwa Yesu Kristo wa yote aliyonayo Baba” (“Wanaume na Wanawake na Nguu za Ukuhani,” Ensign, Sept. 2014, 32).

Urais wa kwanza wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wa Kigingi cha Salt Lake waliandika mnamo 1878: “Tunajihisi hakika wenye shukrani kwamba kupitia baraka ya Baba yetu wa Mbinguni, sisi, wajakazi Wake tumeitwa kuwa watumishi wenza pamoja na ndugu zetu katika kujenga ufalme wa Mungu duniani, katika kutoa msaada kujenga Mahekalu, ambamo ndani yake tunaweza kupokea baraka kwa muda na milele. Katika ibada zote zinazopokelewa katika Nyumba ya Bwana, mwanamke husimama kando ya mwanamume, yote kwa niaba ya walio hai na wafu, ikidhihirisha kwamba si mwanamke pasipo mwanamume wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana” (Mary Isabella Horne, Elmina S. Taylor, na Serepta M. Heywood, “Kwa Marais na Washiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wa Kigingi cha Sayuni cha Salt Lake, Salamu!Woman’s Exponent, Jan. 15, 1878, 123).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Lenga ufundishaji wako kwenye mafundisho. Hakikisha majadiliano yako na darasa yanalenga kwenye mafundisho ya kimsingi katika maandiko. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaomba washiriki wa darasa kusoma maandiko na kisha kushiriki kweli wanazopata, vilevile uzoefu wao wa kuishi kweli hizo. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20–21.)

Chapisha