Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 9–15. Mafundisho na Maagano 88: “Ijengeni … Nyumba ya Mungu”


“Agosti 9–15. Mafundisho na Maagano 88: ‘Ijengeni … Nyumba ya Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 9–15. Mafundisho na Maagano 88,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

chumba chenye viti na mabenchi

Agosti 9–15

Mafundisho na Maagano 88

“Ijengeni … Nyumba ya Mungu”

Kama mwalimu wa injili, una wajibu wa kulisaidia darasa lako “kufundishana mafundisho ya ufalme” na “maneno ya hekima” (Mafundisho na Maagano 88:77, 118). Kando na kushiriki vitu ambavyo umetiwa msukumo kushiriki kutoka Mafundisho na Maagano 88, wahimize washiriki wa darasa wafundishane kile ambacho wamejifunza.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati mwingine picha inaweza kuchochea kushiriki. Unaweza kuonesha picha ya tawi la mzeituni (au kuchora moja ubaoni) na waalike washiriki wa darasa kushiriki mistari kutoka Mafundisho na Maagano 88 ambayo inawasaidia kuelewa kwa nini Joseph Smith anaweza kuwa aliuita ufunuo huu “‘jani la mzeituni’ … , ujumbe wa Bwana wa amani kwetu sisi” (kichwa cha habari cha sehemu).

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 88:6–50

Nuru na sheria huja kutoka kwa Yesu Kristo.

  • Ili kulisaidia darasa lako kuelewa Mafundisho na Maagano 88:6–50, unaweza kuandika nuru na sheria kwenye ubao na ugawe darasa katika vikundi viwili. Kikundi kimoja kinaweza kufanya mapitio ya Mafundisho na Maagano 88:6–13, 40–50, wakitafuta vitu ambavyo wanajifunza kuhusu Yesu Kristo kuanzia kwenye marejeleo mpaka kwenye nuru katika mistari hii. Kikundi kingine kinaweza kusoma mistari 13–26, 34–42, wakitafuta kile wanachojifunza kuhusu umuhimu wa kufuata sheria Yake. Ni nini kweli kuhusu nuru na sheria katika sehemu ya 88 zinatufundisha juu ya Mwokozi? Ni jinsi gani zinatushawishi kuwa zaidi kama Yeye?

Mafundisho na Maagano 88:62–76; 119–26

Tunaweza kuwa wasafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

  • Amri ya Bwana “jitakaseni” inapatikana mara mbili katika sehemu ya 88 (mistari 68, 74). Kama unahisi kusukumwa kujadili maana yake, mnaweza kuanza kwa kuchunguza pamoja ufafanuzi wa neno takasa au kufanya mapitio ya baadhi ya maandiko yaliyoorodheshwa chini ya “Utakaso” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Unaweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mafundisho na Maagano 88:62–76, 119–26 na wajadili maswali kama haya wakiwa na mwenza: Ni kwa jinsi gani tunatakaswa? Ni ahadi gani kutoka kwa Bwana tunazipata katika mistari hii? Je, ni kwa nini Bwana anataka sisi tuwe wasafi? Pia wanaweza kupata majibu ya maswali haya katika ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Kutakaswa kwa Toba” (Ensign au Liahona, Mei 2019, 91–94; ona pia “Nyenzo za Ziada”).

Mafundisho na Maagano 88:77–78; 118–26

Bwana anatutaka tutafute kuelimika kwa kujifunza na kwa imani.

  • Ushauri uliotolewa na Bwana kusaidia kuanzisha “shule ya manabii” kule Kirtland (mstari wa 137) unaweza kulisaidia darasa lako katika juhudi zenu za “kufundishana mafundisho ya ufalme” (mstari wa 77). Pengine mnaweza kuchunguza mistari 77–78 na 118–26 na kujadili jinsi mnavyoweza kulifanya darasa lenu “nyumba ya kujifunza” (mstari wa 119). Washiriki wa darasa wanaweza kuandika “sheria za darasa” au kanuni kulingana na mistari hii ambazo zitaongoza kujifunza kwenu darasani. Unaweza pia kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wanajaribu kuzitumia kanuni hizi “wanapotafuta maarifa” (mstari wa 118).

    watoto wakisoma maandiko

    Nyumba zetu zinaweza kuwa sehemu za mafunzo ya kiroho.

Mafundisho na Maagano 88:119

Hekalu ni nyumba ya Mungu.

  • Kama inawezekana, weka picha ya hekalu lililo karibu kwenye ubao, na uruhusu darasa liandike kando yake maneno kutoka mstari wa 119 yaliyotumika kuelezea nyumba ya Bwana. Waalike kushiriki uzoefu ambao unaonesha namna ambavyo hekalu linalingana na kila maelezo. Pia unaweza kujadili jinsi mstari huu unavyoweza kuongoza maisha yetu.

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kutakaswa kwa toba.

Rais DallinH. Oaks alifundisha:

“Toba inaanza na Mwokozi wetu, na ni furaha, si mzigo. …

“Ili kutakaswa kwa toba, lazima tuziache dhambi zetu na kuziungama kwa Bwana na kwa waamuzi Wake hapa duniani pale inapohitajika (ona Mafundisho na Maagano 58:43). Alma pia alifundisha kwamba lazima ‘tutende kazi za haki’ (Alma 5:35). Hii yote ni sehemu ya mwaliko wa mara kwa mara wa kuja kwa Kristo.

“Tunahitaji kupokea sakramenti kila siku ya Sabato. Katika ibada hiyo tunaweka maagano na kupokea baraka ambazo zinatusaidia kushinda vitendo vyote na tamaa ambazo zinazuia ukamilifu ambao Mwokozi wetu anatualika kuufikia (ona Mathayo 5:48; 3 Nefi 12:48). ‘Tunapojinyima [wenyewe] ubaya wote, na kumpenda Mungu kwa mioyo [yetu], akili na nguvu,’ ndipo, tunapoweza ‘kukamilika katika Kristo’ na ‘kutakaswa’ kupitia damu Yake iliyomwagika, ili ‘kuwa watakatifu, bila waa’ (Moroni 10:32–33). Ni ahadi iliyoje! Ni muujiza ulioje! Ni baraka iliyoje!” (“Kutakaswa kwa Toba,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 92).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta Nyenzo ambazo zinaunga mkono kanuni. Kando na mapendekezo katika mwongozo huu, unaweza kutafuta video za Kanisa, muziki, au kazi ya sanaa ambayo inafundisha kanuni katika Mafundisho na Maagano 88. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17–18.)