Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87: “Simameni Katika Mahali Patakatifu”


“Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87: ‘Simameni Katika Mahali Patakatifu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
familia ikienda hekaluni

Agosti 2–8

Mafundisho na Maagano 85–87

“Simameni Katika Mahali Patakatifu”

Usihisi shinikizo kumaliza kugusia kila mstari—au hata sehemu—ya Mafundisho na Maagano katika Shule ya Jumapili. Acha Roho akuongoze, na itikia kwa kile washiriki wa darasa wanachoona kuwa muhimu katika maisha yao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wanaweza kupitia kwa haraka Mafundisho na Maagano 85–87 kwa ajili ya neno au kirai kinachoonekana kuwa muhimu kwao (labda mojawapo ya kile walichokiwekea alama katika maandiko yao). Waombe waandike maneno au virai vyao kwenye ubao, na chagua vichache kwa ajili ya kuvijadili.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 85:6

Roho huzungumza kwa “sauti ndogo tulivu.”

  • Katika Mafundisho na Maagano 85:6, Nabii Joseph Smith alitumia lugha ya maelezo kusimulia kuhusu namna ambavyo Roho alikuwa amezungumza naye. Je, tunajifunza nini kuhusu Roho Mtakatifu kutoka kwenye maelezo haya? Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa wafikirie kuhusu wakati ambapo Roho alisema nao—Ni jinsi gani wangeelezea uzoefu wao? Wanaweza kupata maelezo ya ziada katika vifungu vya maandiko kama hivi: Luka 24:32; Mosia 5:2; Alma 32:28; Helamani 5:30; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 11:12–13.

  • Je, unaweza kufikiria somo la vielelezo au kuonesha kwa vitendo ambalo unaweza kutumia kuonesha minong’ono tulivu ya Roho? Labda unaweza kuwa na muziki mtakatifu ukicheza kwa sauti ya chini wakati washiriki wa darasa wanapoingia chumbani. Washiriki wa darasa wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi muziki ulivyofanya wahisi na jinsi ambavyo ingekuwa vigumu kuusikia muziki kama kungekuwa na kelele. Hii inaweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu vivuta mawazo katika maisha yetu ambavyo vinatuzuia kusikia sauti ndogo, tulivu. Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile wanachofanya ili kuongeza usikivu wao kwa Roho—baadhi ya ushauri unaweza kupatikana katika “Nyenzo za Ziada.”

Mafundisho na Maagano 86:1–7

Wenye haki wanakusanywa katika siku za mwisho.

  • Shughuli ifuatayo inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ishara zinazopatikana katika fumbo la ngano na magugu: unaweza kuandika virai vya kiishara kutoka kwenye fumbo (kama vile “wapanda mbegu,” “magugu huikaba ngano,” “jani linapoanza kumea,” na “kuikusanya ngano” [mistari 2–4, 7]) na tafsiri zinazoweza kutumika (kama “Mitume,” “Ukengeufu,” “Urejesho,” na “kazi ya umisionari”) kwenye vipande tofauti vya karatasi na uvibandike kwenye ubao. Washiriki wa darasa wanaweza kushirikiana kulinganisha ishara na maana zake, wakitumia kile wanachojifunza kutoka Mafundisho na Maagano 86:1–7 (wanaweza pia kusoma Mathayo 13:37–43). Kwa nini ni muhimu kuwa Bwana anauelekeza ufunuo huu “kwenu ninyi watumishi wangu”? (mstari wa 1). Ni jumbe zipi tunazipata ambazo zinahusiana na huduma yetu kwa Bwana? (ona pia mstari wa 11).

Mafundisho na Maagano 87:2, 6, 8

Amani inapatikana katika “mahali patakatifu.”

Picha
mwanamke nje ya hekalu

Hekalu ni mahali patakatifu ambapo tunaweza kuhisi upendo wa Mungu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa “kusimama … katika pahali patakatifu,” unaweza kuanza kwa kuwaalika waorodheshe baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo katika siku za mwisho. Wanaweza kupata baadhi ya mifano katika Mafundisho na Maagano 87:2, 6. Kisha mnaweza kujadiliana jinsi ambavyo mwaliko wa Bwana katika mstari wa 8 unaweza kuwa msaada kwa changamoto hizi. Maswali kama haya yanaweza kuwa msaada:

    Ni nini cha muhimu kuhusu neno “simameni” katika mstari huu?

    Ni nini kinafanya mahali kuwa patakatifu?

    Nini kinaweza kumtoa mtu kutoka mahali patakatifu?

    Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha kwamba hatuondoshwi?

  • Labda washiriki wa darasa wanaweza kuwa radhi kushiriki na wenzao mifano ya “mahali patakatifu” na nini kinapafanya kuwa patakatifu (unaweza kusema kwamba mahali patakatifu panaweza kuwa zaidi ya sehemu ya nje). Video “Standing in Holy Places” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kutoa mawazo zaidi. Wanaposhiriki, wahimize wazungumze kuhusu kwa nini sehemu hizo ni takatifu kwao. Ni jinsi gani mahali patakatifu panatusaidia kupata amani katikati ya majanga ya siku za mwisho?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Tafuta “muda tulivu na kimya kila siku.”

Dada Vicki F. Matsumori, aliyekuwa mshauri katika Urais Mkuu wa Msingi alitoa ushauri huu: “Kwa maana Roho mara nyingi anaelezewa kuwa sauti ndogo, tulivu, ni … muhimu kuwa na wakati wa utulivu maishani mwetu pia. Bwana Ametushauri ‘tulia, na ujue kuwa Mimi ni Mungu’ [Zaburi 46:10]. Kama tutatenga muda tulivu na kimya kila siku wakati hatushambuliwi na televisheni, kompyuta, michezo ya video, vifaa binafsi vya kielektroniki, tunaipa nafasi ile sauti ndogo na tulivu kutupatia ufunuo binafsi na kutunong’onezea mwongozo mtamu, kuleta hakikisho jipya, na kutufariji” (“Kuwasaidia Wengine Kutambua Minong’ono ya Roho,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 11).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jitayarishe ukiwa na watu akilini. “Acha uelewa wako juu ya wale unaowafundisha uongoze [matayarisho] yako. … Walimu walio kama Kristo hawatumii mtindo au mbinu moja tu; wao hufanya kila juhudi kuwasaidia watu kujenga imani yao katika Yesu Kristo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi7).

Chapisha