“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83: Na Kila “Aliyepewa Vingi Kwake Huyo Vitatakiwa Vingi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Julai 19–25
Mafundisho na Maagano 81–83
Na Kila “Aliyepewa Vingi Kwake Huyo Vitatakiwa Vingi”
Kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanapata uzoefu wa kiroho wanapojifunza maandiko nyumbani. Kwa sala fikiria namna ambavyo unaweza kuwatia moyo kushiriki uzoefu wao ili wainuane.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike washiriki wa darasa wachague kirai kutoka kwenye kila moja ya sehemu zifuatazo ambacho kingekuwa kichwa cha habari cha sehemu hiyo: Mafundisho na Maagano 81, 82, na 83. Kwa nini walichagua vichwa hivi vya habari?
Fundisha Mafundisho
Mafundisho na Maagano 81:5; 82:18–19
Tunapaswa kutafuta “ustawi wa jirani [yetu].”
-
Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza maswali ya kutafakari kuhusu Mafundisho na Maagano 81:5. Haya pia yanaweza kuwa maswali mazuri ya mjadala katika darasa lako. Pia fikiria kushiriki uzoefu binafsi wakati ulipojihisi “mdhaifu” katika namna fulani na huduma ya mtu mwingine ikakuinua au kukuimarisha. Washiriki wa darasa wanaweza kuwa na uzoefu sawa ambao wangeweza kushiriki. Mnaweza pia kutazama video “Works of God” (ChurchofJesusChrist.org) ili kuwatia msukumo washiriki wa darasa wahudumiane. Pia unaweza kushiriki kauli ya Rais M. Russell Ballard katika “Nyenzo za Ziada.”
-
Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kujifunza Mafundisho na Maagano 82:18–19, wakitafuta kanuni ambazo zinawasaidia kuelewa malengo na baraka za kuwatumikia wengine. Kisha waache washiriki kile walichojifunza. Pia unaweza kuonesha video “Teachings of Thomas S. Monson: Rescuing Those in Need” (ChurchofJesusChrist.org). Ni jinsi gani waumini wa kata ya Askofu Monson walionesha kile mistari 18–19 inachofundisha?
“Mimi, Bwana, ninafungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema.”
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa uhusiano baina ya utiifu wetu wa hiyari na baraka za Mungu zilizoahidiwa, mnaweza kusoma Mafundisho na Maagano 1:37–38; 82:10; 130:20–21 pamoja au katika vikundi vidogo. Ni nini maandiko haya yanatufundisha kuhusu Bwana? Labda washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha maneno ambayo yanaelezea sifa Zake, kulingana na mistari hii.
-
Baada ya kusoma mstari wa 10, washiriki wa darasa wanaweza kuzungumza kuhusu kile ambacho Bwana ametuahidi na namna ambavyo Bwana ameheshimu ahadi Zake. Hadithi ya Dada Virginia H. Pearce inayopatikana katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuona kwamba Bwana hutubariki kulingana na busara Yake, si daima katika njia tunazotaka au kutarajia.
-
Ni nini tunajifunza kutoka katika Mafundisho na Maagano 82:8–10 kuhusu sababu ya Baba wa Mbinguni kutupatia amri? Labda washiriki wa darasa wanaweza kutafuta umaizi katika mistari hii kwa matumizi ya kumsaidia rafiki au mtoto anayedhani kwamba amri ni vizuizi (ona pia video “Blessed and Happy Are Those Who Keep the Commandments of God,” ChurchofJesusChrist.org). Au wanaweza kushiriki uzoefu ambao umewafunza kuona amri kama baraka.
Nyenzo za Ziada
Dini safi.
Rais M. Russell Ballard alifundisha:
“Katika ufuasi wetu, tunayo mahitaji mengi, maswali, na majukumu. Hata hivyo, baadhi ya shughuli ni lazima daima ziwe kwenye kiini cha uumini wetu wa Kanisa. ‘Kwa hiyo,’ Bwana anaamuru, ‘uwe mwaminifu; simama katika ofisi ambayo nimekuteua; uwasaidie wadhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na yaimarishe magoti yaliyo dhaifu’ [Mafundisho na Maagano 81:5; italiki imeongezwa].
“Hii ni Kanisa katika vitendo! Hii ni dini iliyo safi! Hii ni injili katika hali yake halisi tunapowasaidia, kuwainua, na kuwaimarisha wale walio na mahitaji ya kiroho na ya kimwili! Kufanya hivyo kunatuhitaji sisi kuwatembelea na kuwasaidia [ona Yakobo 1:27], ili kwamba shuhuda zao za imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na Upatanisho Wake ziweze kutia nanga mioyoni mwao” (“Zawadi za Thamani Kutoka kwa Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 11).
Bwana hutubariki katika njia Zake za ajabu.
Dada Virginia H. Pearce, aliyekuwa mshiriki wa Urais Mkuu wa Wasichana, alielezea kuhusu mwanamke ambaye alikuwa na wasi wasi juu ya watoto wake waliokuwa watundu. Aliweka lengo kuu la kuongeza uhudhuriaji hekaluni na kuhisi kuwa na uhakika kwamba Bwana angetukuza dhabihu hii kubwa kwa kuibadili mioyo ya watoto wake. Mwanamke huyo alisema:
“Baada ya ongezeko la kuhudhuria zaidi hekaluni kwa kipindi cha miaka kumi na kusali siku zote, ninasikitika kusema kwamba chaguzi za watoto wangu hazijabadilika. …
“Lakini mimi nimebadilika. Mimi ni mwanamke tofauti. … Nimeacha mipaka yangu ya muda na ninaweza kumngoja Bwana. … Matarajio yangu yamebadilika. Badala ya kutarajia watoto wangu wabadilike, ninatarajia hizi huruma nyororo za kila muda na nimejawa na shukrani kwa ajili yao. … Bwana hufanya kazi katika njia za ajabu, na kwa kweli nimejazwa na amani ipitayo akili zote” (katika “Prayer: A Small and Simple Thing,” At the Pulpit [2017], 288–89).