Mafundisho na Maagano 2021
Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80: “Nitawaongoza”


“Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80: ‘Nitawaongoza,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
kondoo wakimfuata Yesu

Kwenda Nyumbani, na Yongsung Kim

Julai 12–18

Mafundisho na Maagano 77–80

“Nitawaongoza”

Kumbuka kwamba shughuli zilizoko katika muhtasari huu ni mapendekezo tu. Unaposoma kwa sala Mafundisho na Maagano 77–80, Roho atakuongoza uweze kujua njia bora ya kufundisha washiriki wa darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Baadhi ya washiriki katika darasa lako wanaweza kuwa tayari zaidi kushiriki umaizi wao kama utawaomba mapema. Fikiria kuwasiliana na baadhi yao siku chache kabla ya darasa kuwauliza kama wanaweza kuja wakiwa tayari kushiriki kitu ambacho kiliwavutia sana kutoka Mafundisho na Maagano 77–80.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 77

Mungu hufunua siri Zake kwa wale wanaotafuta kuzijua.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki umaizi walioupata kuhusu ishara katika kitabu cha Ufunuo walipokuwa wakijifunza sehemu ya 77 wiki iliyopita. Kuzungumza kuhusu majibu ambayo Joseph Smith alipokea kunaweza kukaanzisha mjadala kuhusu namna washiriki wa darasa wanavyoweza kutafuta kuelewa wakati wanapojifunza maandiko. Je, tunajifunza nini kutoka kwenye aina ya maswali Joseph aliyouliza? Washiriki wa darasa wanaweza kuwa tayari kushiriki uzoefu wakati maswali yao ya injili yalipopelekea uelewa mkubwa.

Mafundisho na Maagano 78:17–19

Bwana atatuongoza.

  • Ili kuanza mjadala wa Mafundisho na Maagano 78:17–19, Unaweza kuonesha picha za baadhi ya washiriki wa darasa lako wakiwa watoto (waombe kabla waje na picha hizi darasani). Ruhusu darasa libahatishe ni nani yuko katika kila picha. Washiriki wa darasa walioleta picha hizi wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo wamebadilika tangu picha hizo zilipopigwa. Darasa linaweza kusoma Mafundisho na Maagano 78:17–19 na kutafakari maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani sisi ni kama watoto? Ni kwa njia gani Yeye anatutaka tuwe kama watoto (ona Mosia 3:19), na ni kwa namna gani Anatutaka tukue? Ni ushauri gani Yeye anatupatia katika mistari hii ili kutusaidia kukua?

    Ili kupanua uelewa wa washiriki wa darasa lako wa jinsi Bwana anavyoweza “kutuongoza” (mstari wa 18), fikiria kushiriki kauli katika Nyenzo za Ziada.

Mafundisho na Maagano 79–80

Mwito wa kumhudumia Mungu ni muhimu zaidi kuliko mahali tunapohudumu.

  • Kunaweza kuwa na watu katika darasa lako ambao walivunjika moyo mwanzoni kwa wito waliopewa katika kata au tawi au mahali walipopangiwa kutumikia kama wamisionari. Wachache miongoni mwao wanaweza kuwa radhi kushiriki uzoefu wao. Ni jinsi gani ushauri wa Bwana katika Mafundisho na Maagano 80:3 unatusaidia katika hali hizi? Ni nini maana ya kirai “si kitu”? Au kirai “hamwezi kukosea”? Ni nini kinaweza kuwa cha muhimu zaidi kwa Bwana kuhusu miito yetu? Umaizi wa Mzee David A. Bednar kuhusu sehemu ya 80 katika mahubiri yake “Wito kwenye Kazi” unaweza kuwa msaada (Ensign au Liahona, Mei 2017, 68).

  • Funuo katika sehemu za 79 na 80 mwanzoni ziliwalenga watu walioitwa kuhubiri injili, lakini zina kanuni zinazoweza kutufaa sisi wote katika huduma yetu kwa Bwana. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuzipata Kanuni hizi, ungeweza kuwaomba wajifanye wako na rafiki ambaye alijiunga na Kanisa hivi karibuni na kupokea wito wake wa kwanza. Waalike washiriki wa darasa wamwandikie rafiki yao barua ya kumuimarisha na kumshauri, na wahimize wanukuu kutoka sehemu za 79 na 80 wanapoiandika. Kisha washiriki wachache wa darasa wangeweza kuelezea walichoandika.

    Picha
    wanawake wakiongea

    Bwana anafurahia wakati tunapomtumikia Yeye pamoja na wengine.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Bwana atatuongoza kupitia Roho Mtakatifu.

Rais Henry B. Eyring alishiriki uzoefu wa wakati aliposali kwa ajili ya mwongozo kuhusu uamuzi muhimu na akajifunza kuongozwa na Bwana:

“Nilisali, lakini kwa muda wa masaa haikuonekana kama kulikuwa na jibu. Kabla tu ya machweo, hisia ilinijia. Zaidi ya wakati wowote tangu nilipokuwa mtoto, nilijihisi kama mmoja. Moyo na akili yangu vilionekana kuendelea kuwa kimya. Kulikuwa na amani katika utulivu huo wa ndani.

“Kwa namna fulani kwa mshangao wangu, nilijikuta nikisali, ‘Baba wa Mbinguni, haijalishi ninachotaka. Sijali tena ninachotaka. Ninataka tu mapenzi Yako yatimizwe. Hilo tu ndilo ninalotaka. Tafadhali niambie la kufanya.

“Katika wasaa ule nilihisi utulivu ndani yangu namna ambavyo sikuwahi kuhisi. Na ujumbe ulikuja, na nilikuwa na hakika ulitoka kwa nani. Ilikuwa dhahiri kile nilichohitajika kufanya. Sikupata ahadi ya matokeo. Kulikuwa tu na hakikisho kwamba nilikuwa mtoto ambaye alikuwa ameelezwa ni njia ipi iliongoza kufikia kile Yeye alichokitaka kwa ajili yangu” (“Kama Mtoto,” Ensign au Liahona, Mei 2006, 16).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Anza kwa maandiko. Kabla ya kugeukia nyenzo saidizi, kwa bidii jifunze na kutafakari maandiko. Hii itamualika Roho akusaidie kukumbuka kile ambacho ulijifunza wakati unapofundisha (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,12).

Chapisha