Septemba 20–26. Mafundisho na Maagano 106–108: ‘Mbingu Kufunuliwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
Septemba 20–26. Mafundisho na Maagano 106–108,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Septemba 20–26
Mafundisho na Maagano 106–108
“Mbingu Kufunuliwa”
Unaposoma Mafundisho na Maagano 106–8, zingatia uzoefu wa kiroho ambao washiriki wa darasa wanaweza kuwa nao wakati wanapojifunza sehemu hizi. Unapojiandaa kuwafundisha, ingeweza kusaidia kujua kile ambacho walikiona kuwa cha muhimu kwao kabla ya kukutana pamoja.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Alika washiriki wa darasa kushiriki na wengine mstari kutoka kwenye sehemu hizi ambao hufundisha kanuni ambayo ingeweza kumuimarisha mtu katika huduma yao Kanisani.
Fundisha Mafundisho
Mafundisho na Maagano 106; 108
Bwana huwaelekeza, huhimiza, na kuwasaidia wale ambao Yeye anawaita kuhudumu.
-
Wakati washiriki wa darasa walipojifunza Mafundisho na Maagano 106 na 108 wiki hii, labda wamepata virai ambavyo vingeweza kuwasaidia wale ambao wanahudumu katika miito Kanisani (ona muhtasari wa wiki hii kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Fikiria kuwapa washiriki wa darasa muda wa kuandika virai walivyovipata katika sehemu hizi kwenye ubao na waombe kushiriki umaizi wao. Ni uzoefu upi waliokuwa nao ambao unahusiana na au unaoelezea virai hivi?
Bwana huliongoza Kanisa Lake kupitia mamlaka ya ukuhani.
-
Unaweza kuanzisha majadiliano kuhusu ofisi za ukuhani kwa kulialika darasa kuandika orodha ya sababu kwa nini Bwana hutupatia manabii, mitume, na viongozi wengine wa Kanisa. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuongeza kwenye orodha yao baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 107:18–20. Kisha ungechukua muda kurejea wajibu ambao Bwana huwapa wale ambao wanashikilia ofisi zifuatazo: Urais wa Kwanza (mistari 9, 21–22, 65–66, 91–92), Mitume Kumi na Wawili (mistari 23–24, 33–35, 38, 58), Sabini (mistari 25–26, 34, 93–97), na maaskofu (mistari 13–17, 68–76, 87–88). Tunaweza kufanya nini ili kuwaunga mkono viongozi wetu kwa “matumaini, imani, na maombi” yetu? (mstari 22).
-
Ni kwa jinsi gani tungejibu iwapo rafiki ambaye si wa imani yetu angetuuliza, “Ukuhani ni nini?” au “Funguo za Ukuhani ni nini?” Ni kwa jinsi gani mafundisho kutoka “Nyenzo za Ziada” yangeathiri majibu yetu? Labda washiriki wa darasa pia wangeweza kupata umaizi wa kuwasidia katika Mafundisho na Maagano 107:1–4, 18–20 (ona pia True to the Faith , 124–28). Je, ni kwa jinsi ipi ukuhani hutusaidia kupokea “siri za ufalme” na “kufanya mbingu kufunuliwa [kwetu]”? Ni kwa jinsi gani unatusaida “kufurahia ushirika na uwepo wa Mungu Baba, na Yesu”? (mstari wa 19).
Mafundisho na Maagano 107:27–31, 85
Mungu huendesha ufalme wake kupitia mabaraza.
-
Rais M. Russell Ballard alisema, “Najua mabaraza ndiyo njia ya Bwana na kwamba aliumba vitu vyote ulimwenguni kupitia baraza la mbinguni” (“Mabaraza ya Familia,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 63). Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa jinsi ya kushauriana pamoja nyumbani na Kanisani? Pengine ungeweza kuwaomba washiriki wachache kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki uzoefu wao kanisani au nyumbani ambapo walitumia kanuni za ushauri katika Mafundisho na Maagano 107:27–31, 85 (au ujumbe wa Rais Ballard uliorejelewa hapo juu). Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa katikati ya wiki kuja darasani wakiwa wamejiandaa kushiriki mawazo juu ya vitu ambavyo hufanya baraza kuwa lenye tija. Wahimize washiriki wa darasa kutambua kanuni wanazojifunza katika mjadala huu ambazo zitawasaidia wao kuwa na tija zaidi wakati wanaposhiriki kwenye mabaraza ya nyumbani na kanisani katika siku zijazo.
Nyenzo za Ziada
Mamlaka ya ukuhani.
Rais Dallin H. Oaks alifundisha:
“Hatujazoea kuzungumzia wanawake kuwa na mamlaka ya ukuhani katika miito yao Kanisani, lakini yanaweza kuwa ni mamlaka gani mengine? Wakati mwanamke—mdogo au mkubwa—anaposimikwa kwa ajilli ya kufundisha injili kama misionari, yeye hupewa mamlaka ya ukuhani ili afanye kazi ya kikuhani. Huwa sawa vivyo hivyo wakati mwanamke anaposimikwa kufanya kazi kama ofisa au mwalimu katika kikundi cha Kanisa chini ya uelekezi wa Mwenye kushikilia funguo za ukuhani. Yeyote anayefanya kazi katika ofisi au wito kutoka kwa yule anayeshikilia funguo za ukuhani mtu huyo hutumia mamlaka ya ukuhani katika kutimiza majukumu yake” (“Funguo na Mamlaka ya Ukuhani,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 51).
Mzee M. Russell Ballard alisema:
“Baba Yetu wa Mbinguni ni mkarimu kwa nguvu zake. Wanaume na wanawake wote wanaweza kutumia nguvu hii kwa ajili ya msaada katika maisha yao. Wote waliofanya maagano matakatifu na Bwana na wanaoheshimu maagano hayo wanastahili kupokea ufunuo binafsi, kubarikiwa kwa kutumikiwa na malaika, kuzungumza na Mungu, kupokea utimilifu wa injili, na, hatimaye, kuwa warithi pamoja na Yesu Kristo wa vile vyote Baba Yetu alivyo navyo” (“Men and Women in the Work of the Lord,” New Era, Apr. 2014, 4–5).