Septemba 27–Oktoba 3. Mafundisho na Maagano 109–110: ‘Ni Nyumba Yako, Mahali pa Utakatifu Wako,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
Septemba 27–Oktoba 3. Mafundisho na Maagano 109-110,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Septemba 27–Oktoba 3
Mafundisho na Maagano 109–110
“Ni Nyumba Yako, Mahali pa Utakatifu Wako”
Sehemu ya 109 na 110 inaelezea baadhi ya matukio matakatifu sana ya Urejesho. Hakikisha umeruhusu washiriki wa darasa kushiriki walichofikiria na kuhisi walipokuwa wakijifunza matukio haya.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Bwana alitangaza “umaarufu wa nyumba hii [Hekalu la Kirtland] utaenea hadi nchi za kigeni” (Mafundisho na Maagano 110:10). Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushirki kitu walichopata katika masomo yao wanachohisi kwamba wanapaswa kueneza kwa watu duniani kote.
Fundisha Mafundisho
Mafundisho na Maagano 109; 110:1–10
Bwana anataka kutubariki kwenye nyumba yake takatifu.
-
Kusoma Sehemu ya 109 ni fursa ya ajabu ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha ari yao ya kuabudu hekaluni. Unaweza kuandika ubaoni baadhi ya mistari inayotaja baraka za hekaluni—kama vile mistari 12–13, 22–23, 24–28, 29–32. Washiriki wa darasa wangeweza kuchagua mistari ya kusoma na kutafakari, binafsi ama katika vikundi, na kisha kutoa muhtasari wa baraka hizo zinazoelezewa kwa darasa. Washiriki ambao wamewahi kwenda hekaluni wangeweza kushiriki na wengine uzoefu wao juu ya baraka hizi katika maisha yao.
Ungeweza pia kusoma au kuimba “The Spirit of God” (Nyimbo za Kanisa, na. 2), ambao uliimbwa wakati wa kuweka wakfu Hekalu la Kirtland. Washiriki wa darasa wangeweza kutaja baraka za hekaluni zilizoelezwa kwenye wimbo na kueleza uzoefu wowote unaohusiana nazo ambao wamekuwa nao, kama itahitajika.
-
Kupokea baraka za hekaluni mara nyingi kunahitaji dhabihu. Je, Mafundisho na Maagano 109:5 hutufundisha nini kuhusu dhabihu ambazo Watakatifu wa awali walitoa ili kujenga Hekalu la Kirtland? Pengine mtu angeweza kuja akiwa amejiandaa kuongea kuhusu dhabihu hizi (ona “Nyumba ya Mungu Wetu,” Ufunuo katika Muktadha, 169–71). Je, tunatoa dhabihu zipi ili kupokea baraka za hekaluni hivi leo? Pengine washiriki wa darasa wangekuwa tayari kushiriki uzoefu wao. Baadhi ya mifano ya hivi leo inapatikana kwenye video “Sealed Together: The Manaus Temple Caravan” na “Temples Are a Beacon” (ChurchofJesusChrist.org).
-
Kujifunza kuhusu maelezo ya Mwokozi aliyefufuka katika Mafundisho na Maagano 110:1–10 ni njia kubwa ya kujenga imani yetu katika Yesu Kristo. Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutilia maanani lugha ya picha katika mistari hii na kuzingatia kile ambacho picha hizo hufundisha kuhusu Yesu Kristo. “Sakafu iliyofanyizwa kwa dhahabu safi” inaweza kuwakilisha nini? au sauti “ kama ya maji mengi yakimbiayo”?
Mafundisho na Maagano 110:11–16
Funguo za ukuhani zinazohitajika kukamilisha kazi ya Mungu zipo Kanisani leo hii.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufahamu funguo za ukuhani ambazo Musa, Elia na Eliya walikabidhi kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery kwenye Hekalu la Kirtland, ungeweza kuwaalika kusoma na kujadili binafsi au kama makundi maelezo katika “Nyenzo za Ziada.” Kwa nini funguo hizi ni muhimu katika maisha yetu hivi leo? Pia ungeweza kumuomba kila mshiriki wa darasa kuchagua mmoja wa manabii aliyekabidhi funguo hizo—Musa, Elia, na Eliya—na kujifunza juu yake kutoka katika Kamusi ya Biblia au Mwongozo wa Maandiko. Maisha ya manabii hawa yanatufundisha nini kuhusu funguo walizokabidhi? Hii inaweza kupelekea mjadala kuhusu kile ambacho Bwana anatarajia tukifanye sasa kwa kuwa funguo hizi ziko duniani.
Nyenzo za Ziada
Funguo hutoa nguvu na mamlaka kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Mzee Quentin L. Cook alifundisha:
“Hekalu la Kirtland, kwa vyote mahali na ukubwa, lilikuwa limefichika kiasi. Lakini kwa umuhimu wake mkubwa kwa wanadamu, lilikuwa ni la kuandaa umilele. Manabii wa kale walirejesha funguo za ukuhani kwa ajili ya ibada okozi za milele za injili ya Yesu Kristo. Hii ilisababisha furaha kubwa kwa waumini waaminifu.
“Funguo hizi hutoa ‘nguvu kutoka juu’ [Mafundisho na Maagano 38] kwa ajili ya majukumu ya kiungu yaliyoteuliwa ambayo hujumuisha dhumuni kuu la Kanisa. Siku hiyo nzuri ya Pasaka katika Hekalu la Kirtland, funguo tatu zilirejeshwa:
“Kwanza, Musa alitokea na kukabidhi funguo za kuikusanya Israeli kutoka pande nne za dunia, ambayo ni kazi ya umisionari.
“Pili, Elia alitokea na kukabidhi funguo za injili ya Ibrahimu, ambayo inajumuisha urejesho wa agano la Ibrahimu [ona Ibrahimu 2:8–11]. Rais President Russell M. Nelson amefundisha kwamba lengo la funguo za agano ni kuwaandaa washiriki wa ufalme wa Mungu [ona “Maagano,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 88]. …
“Tatu, Eliya alitokea na kukabidhi funguo za uwezo wa kuunganisha katika kipindi hiki, ambazo ni kazi ya historia ya familia na maagizo ya hekalu inayowezesha wokovu kwa walio hai na wafu(“Jiandae Kukutana na Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 114–15).