Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: “Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Kuliko Mafanikio Yake”


“Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120: ‘Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Kuliko Mafanikio Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Oktoba 11–17. Mafundisho na Maagano 115–120,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Mbali Magharibi

Mbali Magharibi, na Al Rounds

Oktoba 11–17

Mafundisho na Maagano 115–120

“Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Kuliko Mafanikio Yake”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kuwa kusudi lako kuu ni kuwasaidia wengine kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Kabla ya kuongea kuhusu kanuni kutoka sehemu ya 115–20 ambayo ilikuwa na maana kwako, waombe washiriki wa darasa kuelezea kile kilichokuwa cha maana zaidi kwao. Kwa mfano, ungewaalika washiriki wa darasa kukamilisha sentensi hii: “Ninashukuru ninasoma sehemu ya 115–20 kwa sababu …”

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 115:4–6

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ulinzi na kimbilio.

  • Washiriki wa darasa wangeweza kupekua ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Jina Sahihi la Kanisa” (Ensign au Liahona, Nov. 2018, 87–90) kwa ajili ya utambuzi ambao unawasaidia kuelewa mstari wa 4–6. Kwa nini ni muhimu kutumia jina sahihi la Kanisa?

  • Baada ya kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 115:4–6, washiriki wa darasa wangejadili jinsi Kanisa na waumini wake ni kama nuru au kiwango. Ungeweza kuonesha picha ya mnara wa taa ya kuongozea meli wakati wa dhoruba na uwaulize washiriki wa darasa jinsi inavyohusiana na ujumbe wa mistari 5–6. Ni jinsi gani kukusanyika “Sayuni, na … vigingi vyake” kumekupa “kimbilio kutokana na dhoruba”? (mstari wa 6).

    Picha
    mnara wa taa ya kuongozea meli

    Tunaweza kuangaza kama nuru ili kuwasaidia wengine kupata kimbilio katika Kanisa.

Mafundisho na Maagano 117

Dhabihu zetu ni takatifu kwa Bwana.

  • Waalike washiriki wa darasa kufikiria kuwa wao ni Newel K. Whitney au mkewe, Elizabeth, ambao walimiliki duka lenye mafanikio kule Kirtland lakini wakaombwa na Bwana kuacha mali yao na kwenda Missouri. Wangeweza kusoma mistari 1–11 na kuelezea kitu ambacho Bwana alisema ambacho kingewasaidia kufanya dhabihu hii.

  • Vitu vya kutazama kwa macho vingesaidia washiriki wa darasa kufikiria “tone” ambalo wakati mwingine huwa tunatamani badala ya “mambo mazito zaidi” (mstari wa 8). Fikiria juu ya kuonesha vitu kama vile tone la maji na chupa ya maji au kibanzi cha chokoleti na kipande cha chokoleti. Labda washiriki wa darasa wangefikiria mifano mingine. Pia ungeweza kuandika tone na mambo mazito ubaoni na waombe washiriki wa darasa kuorodhesha mifano ya vitu tunavyoweza kuhitaji ili “ku … achilia” (mstari wa 5) ili kupokea “wingi” wa Mungu (mstari wa 7).

  • Ikiwa washiriki wa darasa walikuwa na mawazo yoyote wakati wanasoma maneno ya Bwana kuhusu Oliver Granger katika mistari 12–15, waalike kushiriki. Ni kwa nini dhabihu zetu zaweza kuwa takatifu zaidi kwa Bwana kuliko mafanikio yetu?

Mafundisho na Maagano 119–20

Kwa kulipa zaka, tunasaidia kujenga na “kutakasa nchi ya Sayuni.”

  • Fikiria nguvu za kiriho ambazo zingetoka kwa washiriki wa darasa kushiriki mmoja kwa mwingine baraka ambazo wamepokea kutokana na kutii sheria ya kutoa zaka. Pia wangeweza kusoma Mafundisho na Maagano 119:6 na kujadili jinsi ambavyo sheria hii inaweza “kutakasa nchi ya Sayuni” na kuifanya kata yetu au tawi kuwa “nchi ya Sayuni kwetu [sisi].” Pia wangeweza kusoma Malaki 3:8–12 ili kutambua baraka ambazo Bwana anaahidi kwa kulipa zaka.

  • Ikiwa washiriki wa darasa wana maswali kuhusu jinsi zaka inavyotumika, ungeweza kuwaalika kusoma sehemu ya 120 na ufafanuzi katika “Nyenzo za Ziada.” (Mzee David A. Bednar pia anatoa maelezo ya usaidizi katika “Madirisha ya Mbinguni” [Ensign au Liahona, Nov. 2013, 19–20].) Tunawezaje kuwasaidia wengine kuzidisha imani yao katika sheria ya Bwana ya zaka?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Baraza la Matumizi ya Zaka.

Mzee Robert D. Hales alisema:

“Kama ilivyofunuliwa na Bwana, matumizi ya zaka yanaamuliwa na baraza linalowajumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Askofu Msimamizi. Bwana mahususi anasema kwamba kazi ya baraza ielekezwe ‘na sauti yangu mwenyewe kwao’ [Mafundisho na Maagano 120:1]. Baraza hili linaitwa Baraza la Matumizi ya Zaka.

“Ni ajabu kushuhudia baraza hili likisikiliza sauti ya Bwana. Kila mshiriki anajua juu ya hilo na anashiriki katika maamuzi yote ya baraza. Hakuna uamuzi unaofanywa hadi baraza limekuwa na kauli moja. Fedha zote za zaka hutumika kwa makusudi ya Kanisa, ikijumuisha ustawi—kuwajali masikini na wenye shida—mahekalu, ujenzi wa majengo na utunzaji wa nyumba za mikutano, elimu, mtaala—kwa ufupi, kazi ya Bwana. …

“… ninatoa ushuhuda wangu juu ya baraza hili la Matumizi ya Zaka. Nimekaa katika baraza hili kwa miaka 17, kama Askofu Msimamizi wa Kanisa na sasa kama mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Bila ya kubagua, fedha za zaka za hili Kanisa zimetumiwa kwa makusudi Yake” (“Zaka: Jaribio la Imani lenye Baraka za Milele,” Ensign au Liahona, Nov. 2002, 28).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waalike wanafunzi kufundishana. “Inaweza kuwa sahihi kuwaalika wanafunzi ili kusaidiana kutafuta majibu ya maswali yao. Wakati unapotiwa msukumo na Roho, unaweza kuamua kufanya hivi hata kama unahisi unajua jibu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 24).

Chapisha