Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba 18–24. Mafundisho na Maagano 121–123: “Ee Mungu, Uko Wapi?”


“Oktoba 18–24. Mafundisho na Maagano 121–123: ‘Ee Mungu, Uko Wapi?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Oktoba 18–24. Mafundisho na Maagano 121–123,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
Gereza la liberty

Gereza la Liberty Spring, na Al Rounds

Oktoba 18–24

Mafundisho na Maagano 121–123

“Ee Mungu, Uko Wapi?”

Njia bora ya kujiandaa kufundisha ni kwa kusoma maandiko, fikiria kuhusu watu unaowafundisha, na mfuate Roho. Mawazo yaliyoko katika muhtasari huu yanaweza kuongezea mwongozo wa kiungu unaopokea.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Alika washiriki wa darasa kuchagua ujumbe mmoja kutoka Mafundisho na Maagano 121–23 ambao wangetaka kushiriki na mtu ambaye anateseka. Waruhusu waelezee chaguo lao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 121:1–33;122

Tukivumilia majaribu yetu vizuri, Mungu atatuinua juu.

  • Unaweza kuwa na washiriki wa darasa ambao, kwa sababu ya majaribu magumu, wana hisia sawa na zile ambazo Joseph Smith alionesha katika Mafundisho na Maagano 121:1–6. Baada ya kusoma mistari hii pamoja, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutambua na kushiriki jumbe katika mistari 7–33 zinazowapatia matumaini na utulivu wakati wa majaribu. Ina maana gani “kustahimili … vyema”? (mstari wa 8). Ni jinsi gani Mwokozi anatusaidia kufanya hili? Ni vipi tunaweza kusaidiana kustahimili vyema?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuzingatia jinsi majaribu yanavyoweza “kutupatia uzoefu” na “kuwa kwa faida [yetu]” (Mafundisho na Maagano 122:7), unaweza kuwapatia karatasi na kuwaomba waandike jaribu ambalo wamelipitia. Kwenye upande mwingine wa karatasi, washiriki wa darasa wanaweza kuandika maneno “uzoefu” na “faida”. Mnapojadiliana Mafundisho na Maagano 122pamoja, wahimize washiriki wa darasa kuandika mawazo yoyote waliyonayo kuhusu “upande mwingine” wa majaribu: “uzoefu” au “faida” ambayo wamepata. Washiriki wa darasa wengine wanaweza kuhisi sawa kushiriki jinsi jaribu lao lilivyobadilika na kuwa faida kwao. Ama wanaweza kusoma uzoefu wa Mzee Koichi Aoyagi katika “Hold on Thy Way” (Ensign au Liahona, Nov. 2015, 126–28).

Mafundisho na Maagano 121:34–46

Ni lazima tuwe wenye haki ili kupata “nguvu za mbingu”

  • Inaweza kuwa jambo la kufurahisha kulinganisha jinsi “mamlaka au ushawishi” unavyodumishwa duniani na jinsi Bwana alivyofundisha kwamba mamlaka au ushawishi unapaswa kudumishwa (ona sehemu ya 121). Ili kusaidia katika majadiliano haya, unaweza kuandaa jedwali lenye safu mbili ubaoni na kulipa kichwa cha habari Nguvu za Kiulimwengu na Nguvu za Mbingu. Washiriki wa darasa wanaweza kujaza jedwali hilo kwa maneno na vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 121:34–46. Je, mistari hii inawezaje kubadilisha jinsi tunavyotazama majukumu katika familia zetu, kama akina kaka na akina dada wahudumiaji, ama katika hali nyingine ambapo tuna matumaini ya kushawishi wengine kwa ajili ya mema?

  • Njia moja ya kujadili ushauri na baraka za ajabu katika Mafundisho na Maagano 121:45–46 ni kugawanya darasa katika makundi mawili na kuomba kila kikundi kusoma na kujadili kauli kutoka kwenye mistari hii, kama vile “acha wema uyapambe mawazo yako bila kukoma” au “kama umande kutoka mbinguni”. Wanaweza kutafuta maana ya maneno, kusoma maandiko yanayohusiana katika tanbihi, na kujadili vifungu hivyo vya maneno vina maana gani kwao. Baadhi ya vikundi vinaweza kuchora picha ili kuelezea vifungu vyao. Alika kila kikundi kuelezea kwa darasa kile walichojifunza.

Mafundisho na Maagano 122:8–9

Yesu Kristo amejishusha chini ya vitu vyote na hutuimarisha katika majaribu yetu.

  • Kuelewa kwamba Yesu Kristo “amejishusha chini ya … [vitu] vyote” kunaweza kuwapatia washiriki wa darasa lako kujiamini ili kumgeukia Yeye. Maandiko haya ya ziada yanaweza kusaidia katika kufafanua maana ya kauli hii: Isaya 53:3–4; Waebrania 2:17–18; 1 Nefi 11:16–33; Alma 7:11–13. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari hii, pamoja na Mafundisho na Maagano 122:8, wakitafuta kitu ambacho hujenga imani yao kwamba Yesu Kristo anaweza kuwasaidia katika majaribu yao. Pia wanaweza kupata mwongozo wa kiungu katika nyimbo za kanisa kuhusu Mwokozi, kama vile “Where Can I Turn for Peace?” (Nyimbo za Kanisa, na. 129).

  • Maelezo katika “Nyenzo za Ziada” hutoa utambuzi zaidi kuhusu jinsi Mwokozi alivyojishusha chini ya vitu vyote. Unaweza kufikiria njia ambayo ungeweza kuonesha jinsi kuwa “chini ya” chombo kizito hutufanya “kuwa katika nafasi nzuri ya kukiinua”. Kufahamu kwamba Mwokozi alijishusha chini ya vitu vyote kumetusaidiaje katika majaribu yetu?

    Picha
    Yesu akiwa Gethsemane

    Yesu anafahamu mateso yetu. Walakini si kama Nitakavyo Mimi, Bali kama Utakavyo Wewe, na Walter Rane.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kristo alijishusha chini ya vitu vyote.

Rais Dallin H. Oaks alifundisha, “Kuna mamilioni ya watu wenye hofu-ya Mungu ambao huomba kwa Mungu ili wainuliwe kutokana na mateso yao. Mwokozi wetu amefunua kwamba Yeye ‘alijishusha chini ya vitu vyote’ (M&M 88:6). Kama Mzee Neal A. Maxwell alivyofundisha, ‘Akiwa “amejishusha chini ya vitu vyote,” Yeye anafahamu, kikamilifu na kibinafsi, kiwango kamili cha mateso ya binadamu’ [Ensign, Nov. 1997, 23]. Tunaweza kusema hata kwamba kwa kuwa alijishusha chini ya vitu vyote, Yeye yupo katika nafasi nzuri zaidi ya kutuinua na kutupatia nguvu tunayohitaji ili kuvumilia mateso yetu” (“Kuimarishwa na Upatanisho wa Yesu Kristo,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 64).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wito wako ni wa mwongozo wa kiungu. Kama mwalimu, umeitwa na Bwana ili kubariki watoto Wake. Yeye anataka wewe ufaulu, hivyo ukiishi kwa kustahili msaada Wake, Atakupa Ufunuo unaouhitaji (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5).

Chapisha