Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 20–26. Krismasi: Zawadi isiyo na Mfano ya Mwana Mtakatifu wa Mungu


Desemba 20–26. Krismasi: Zawadi isiyo na Mfano ya Mwana Mtakatifu wa Mungu,” Njoo, unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

Desemba 20–26. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
sanaa ya Mariamu na mtoto mchanga Yesu

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Shaba na Kijani Kibichi, na J. Kirk Richards

Desemba 20–26

Krismasi

Zawadi Isiyo na Mfano ya Mwana Mtakatifu wa Mungu

Kumbuka kwamba kwa washiriki wa darasa sehemu muhimu sana na yenye ufanisi kwa wao kujifunza injili ni nyumbani mwao. Unapojiandaa kufundisha, fikiria jinsi darasa lako la Shule ya Jumapili linavyoweza kuimarisha kujifunza kwao binafsi na kama familia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Ni jinsi gani kujifunza “Kristo Aliye Hai” (ChurchofJesusChrist.org) wiki hii kumewabariki washiriki wa darasa lako? Ungeweza kushiriki nao maneno haya kutoka kwa Rais Jean B. Bingham, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, na kisha uwaalike washiriki wa darasa kuongea kuhusu aina yoyote ya uzoefu kama huo ambao wamekuwa nao: “Kama nilivyojifunza maisha na mafundisho ya Yesu Kristo kwa fokasi zaidi na kuhifadhi moyoni ‘Kristo Aliye Hai’, shukrani yangu na upendo kwa Mwokozi wetu vimeongezeka. Kila sentensi ya nakala hii yenye mwongozo wa kiungu imebeba mahubiri na imeongeza uwezo wangu wa kuelewa kazi Yake ya kitukufu na misheni yake duniani. Kile ambacho nimejifunza na kuhisi katika muda huu wa kusoma na kutafakari kimethibitisha kuwa Yesu kweli ‘ni nuru, uzima na tumaini la ulimwengu’” (“Ili Shangwe Yako Iwe Timilifu,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 85).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

“Hakuna mwingine aliyewahi kuwa na ushawishi huo wa kushangaza”

  • Washiriki wa darasa wanaweza kusoma aya ya kwanza ya “Kristo Aliye Hai” na kushiriki na wengine mawazo yao kuhusu ni kwa nini ushawishi wa Yesu Kristo umekuwa wa kushangaza sana kuliko wa mtu mwingine yeyote. Ni kauli zipi zingine katika “Kristo Aliye Hai” zinaunga mkono dai hili? Waalike washiriki wa darasa kuelezea jinsi ambavyo Yeye amewashawishi wao. Video ya “Why We Need a Savior” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kuwa nyongeza ya mjadala wenu.

  • Je, washiriki wa darasa wamewahi kulazimika kufafanua kwa mtu wa utamaduni mwingine kwa nini wao husheherekea Krismasi? Pengine wanaweza kutoa mawazo yao. Au unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria kwamba waliulizwa swali hili na mtu ambaye hajui Ukristo. Je, tungeweza kumjibu namna gani kwa swali hili? Himiza washiriki wa darasa kufanyia marejeo “Kristo Aliye Hai” wakiwa na swali hili akilini, na uwaalike wachache kutoa mawazo yao. Kama darasa, mngeweza pia kusoma Luka 2:10–14 au imbeni wimbo ambao unaelezea shangwe ya Krismasi (kama vile “Joy to the World,” Nyimbo za Kanisa, na. 201) na zungumzeni kuhusu kwa nini kuzaliwa kwa Kristo kunaleta “shangwe kuu.” Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha kuongoka kwetu?

    Picha
    Yesu Kristo

    Nuru ya Ulimwengu, na Howard Lyon

“Mungu ashukuriwe kwa zawadi [yake] isiyo na mfano.”

  • Katika “Kristo Aliye Hai,” Mitume humrejelea Mwokozi kama “zawadi” kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza zaidi kuhusu zawadi hii, andika ubaoni Kupitia kwa Yesu Kristo, Mungu hutupa zawadi ya … na uwaalike washiriki wa darasa wapendekeze njia za kukamilisha sentensi hii, kutegemea kile ambacho wao husoma katika “Kristo Aliye Hai” na kauli kutoka kwa Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada.” Je, sisi hupokeaje zawadi hizi? Ungewaalika washiriki wa darasa kuchagua mojawapo ya zawadi hizi na wafanye kazi kupokea zawadi hiyo kikamilifu.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Zawadi ambazo Mwokozi anatoa.

Akiongea juu ya Wakati wa Krismasi, Rais Russell M. Nelson aliorodhesha zawadi nne ambazo Mwokozi hutoa kwa wote walio tayari kupokea:

“Kwanza, Alikupa wewe na mimi uwezo usio na kipimo wa kupenda. Hii inahusisha uwezo wa kupenda wasio pendeka na wale ambao si tu hawakupendi bali kwa wakati huu wanakutesa na kukutumikia isivyo.

“Kwa usaidizi wa Mwokozi, tunaweza kujifunza kupenda jinsi Alivyopenda. …

“Zawadi ya pili Mwokozi anayotoa ni uwezo wa kusamehe. Kupitia Upatanisho Wake usio na mwisho, unaweza kuwasamehe wale waliokuudhi na ambao hawawezi kukubali kuwajibika kwa ajili ya ukatili wao kwako. …

“Zawadi ya tatu kutoka kwa Mwokozi ni ile ya toba. Zawadi hii daima haieleweki vyema. … Toba ni zawadi ya kifahari. Ni mchakato usiopaswa kuogopwa. Ni zawadi kwa ajili yetu kuipokea kwa furaha na kuitumia—hata kuikumbatia—siku baada ya siku tunapotafuta kuwa zaidi kama Mwokozi wetu. …

“Zawadi ya nne kutoka kwa Mwokozi wetu kwa kweli ni ahadi—ahadi ya uzima wa milele. … Uzima wa milele ni mfano na aina ya uzima ambao Baba wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa wanauishi. Baba anapotupatia uzima wa milele, Anasema kwa uhalisia kuwa, ‘ukichagua kumfuata Mwanangu—ikiwa tamanio lako ni hasa kuwa zaidi kama Yeye—hapo basi kwa wakati muafaka unaweza kuishi kama tunavyoishi na kuongoza ulimwengu na falme kama tunavyoongoza.’

“Hizi zawadi maalumu nne zitatuletea furaha zaidi na zaidi tunapozikubali. Ziliwezekana kwa sababu Yehova alijishusha ili kuja duniani kama mtoto Yesu” (“Zawadi Nne Ambazo Yesu Kristo Anatoa Kwako” [First Presidency Christmas devotional, Dec. 2, 2018], broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiandae mwenyewe Kiroho. Ufundishaji injili wenye nguvu haumaanishi tu kutayarisha somo bali pia kujiandaa sisi wenyewe. … Walimu wa injili wenye tija—kabla hawajafikiria kuhusu kutimiza muda wa darasani—hufokasi kwenye kujaza mioyo yao kwa Roho Mtakatifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,12).

Chapisha