Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138: “Ono la Ukombozi wa Wafu”


“Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138: ‘Ono la Ukombozi wa Wafu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

watu katika ulimwengu wa roho

Joseph anamwona baba yake, mama yake, na kaka yake katika ufalme wa selestia (Ono la Joseph Smith la Ufalme wa Selestia, Robert Barrett).

Novemba 29–Desemba 5

Mafundisho na Maagano 137–138

“Ono la Ukombozi wa Wafu’’

Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Sote tunaweza kujiuliza kwa faragha kuhusu hali katika ulimwengu wa roho. … Lakini tusifundishe au kutumia kama mafundisho rasmi kile kisichokidhi viwango vya mafundisho rasmi” (“Mwamini Mungu,” Ensign au Liahona, Nov. 2019, 28). Hakikisha kwamba majadiliano yako yanatokana na maandiko na maneno ya manabii.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Kuna ukweli mwingi wa kimafundisho wenye mwongozo wa kiungu unaopatikana katika Mafundisho na Maagano 137–38. Alika washiriki wa darasa kuorodhesha baadhi yao. Kisha mnaweza kuchukua dakika chache kupitia orodha zao kama darasa na kuzungumza kuhusu ni kwa nini ukweli huu ni muhimu kwao. Je, mtu yeyote alijifunza kitu kutoka katika sehemu hizi ambacho hapo mwanzoni hawakukielewa?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 137; 138:32–37

Kila nafsi itakuwa na nafasi ya kuchagua utukufu wa selestia.

  • Wengi wetu tunawajua watu ambao hawakupata nafasi ya kukubali injili katika maisha haya—ikiwa ni pamoja na wale ambao hufa wakiwa watoto. Alika washiriki wa darasa kushiriki ukweli waliopata katika sehemu ya 137 ambao huwasaidia kufahamu mipango ya Mungu kwa watu hawa. Tunapata kweli zipi tunazopata katika Mafundisho na Maagano 138:32–37 ambao huchangia katika ufahamu wetu juu ya mpango wa Mungu? Washiriki wa darasa wanaweza kueleza jinsi ukweli huu unavyowafanya wahisi kuhusu Baba wa Mbinguni, mpango Wake wa wokovu, na Upatanisho wa Yesu Kristo. Maelezo katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuwa ya faida kwenye mazungumzo haya.

Mafundisho na Maagano 138:1–11–34, 25–30.

Kusoma na kutafakari maandiko hututayarisha kupokea wokovu.

  • Tukio la Joseph F. Smith lililoelezwa katika Mafundisho na Maagano 138:1–11, 25–30 hutusaidia kufahamu jinsi tunavyoweza kujiandaa kupokea wokovu. Pengine washiriki wa darasa wanaweza kufanya kazi pamoja kutambua kile wanachojifunza kuhusu ufunuo kutoka kwenye mistari hii. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kueleza jinsi ambavyo kusoma na kutafakari maandiko kumewatayarisha kupokea wokovu (ona pia Joseph Smith—Historia ya 1:11–12).

  • Ujumbe wa Rais M. Russell Ballard “Ono la Ukombozi wa Wafu” (Ensign au Liahona, Nov. 2018, 71–74) unaeleza juu ya “maandalizi ya maisha yote ya Joseph F. Smith ili kupokea ufunuo huu muhimu [Mafundisho na Maagano 138].” Ikiwa washiriki wa darasa lako walisoma ujumbe wa Rais Ballard wiki hii, wahimize kushiriki kitu kilichowafurahisha. Ama mnaweza kusoma sehemu za ujumbe kama darasa. Ni nini hutufurahisha juu ya maisha na tabia ya Rais Smith? Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake?

    mchoro wa Joseph F. Smith

    Joseph F. Smith, na Albert E. Salzbrenner

Mafundisho na Maagano 138:12–60

Kazi ya wokovu huendelea baada ya kifo.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ukweli katika Mafundisho na Maagano 138:12–60, unaweza kuwapatia maswali mengi kuhusu ulimwengu wa roho ambayo yamejibiwa katika mistari hii. Kwa mfano: Mwokozi alifanya nini alipokuwa katika ulimwengu wa roho? Wajumbe wa Bwana ni akina nani, na ujumbe wao ni upi? Washiriki wa darasa wanaweza kuchagua swali au maswali mengi na kufanya kazi katika vikundi vidogo ili kutafuta majibu. Kisha wanaweza kushiriki wao kwa wao ukweli walioupata. Ukweli huu huleta tofauti gani katika maisha yetu?

  • Tutamwambia nini mtu ambaye huuliza, “Nini kinatokea tukifariki?” Je, tungeshiriki nini kutoka Mafundisho na Maagano 138:12–60 ambacho kingeweza kusaidia kujibu swali hili? (ona pia Alma 40:11–15).

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Mpango wa Mungu hutoa njia kwa watoto wake wote kukubali injili.

Rais Henry B. Eyring alifundisha:

“Ni sehemu ndogo tu ya watoto wa Mungu ndiyo hupokea wakati wa maisha haya ufahamu kamili wa mpango wa Mungu, pamoja na ufikiaji wa ibada za ukuhani na maagano ambayo hufanya nguvu ya Mwokozi ya kupatanisha kufanya kazi kikamilifu katika maisha yetu. …

“Wengine wanaweza kufikiria hili kama sio haki. Wanaweza hata kulichukulia kama ushahidi kwamba hakuna mpango, hakuna mahitaji maalum ya wokovu—wakihisi kwamba Mungu mwenye haki na upendo hawezi kuunda mpango unaopatikana kwa sehemu ndogo sana ya watoto wake. Wengine wanaweza kuhitimisha kwamba Mungu ameshaamua mapema ni nani katika watoto wake atawaokoa na kuwapa injili, huku wale ambao hawakusikia injili ‘hawakuchaguliwa’.

“Lakini wewe na mimi tunajua, kwa sababu ya kweli zilizopatikana kupitia kwa Nabii Joseph Smith, kwamba mpango wa Mungu ni wa upendo na wa haki kuliko hiyo. Baba yetu wa Mbinguni ana hamu ya kukusanya na kubariki familia yake yote. Huku akijua kwamba si wote watakaochagua kukusanywa, mpango Wake humpatia kila mtoto Wake fursa ya kukubali au kukataa mwaliko wake” (“Kukusanya Familia ya Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 20–21).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia maneno ya manabii. “Maandiko na maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho ni chanzo cha ukweli tunaofundisha. Katika kila fursa, wahamasishe wale unaowafundisha wageukie neno la Mungu kwa ajili ya kupata mwongozo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21).