Desemba 13-19. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu: ‘Familia ni Kitovu cha Mpango wa Muumbaji,’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Desemba 13–19. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Desemba 13–19
Familia: Tangazo kwa Ulimwengu
“Familia Ni Kitovu cha Mpango wa Muumbaji’’
Unapojifunza “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” wiki hii, zingatia ukweli ambao utawaunga mkono washiriki wa darasa katika juhudi zao za kuimarisha nyumba na familia zao.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwatia moyo washiriki wa darasa kuelezea kitu walichojifunza wiki hii kutokana na kujifunza kwao tangazo la familia, unaweza kuwaomba kuchagua aya yoyote na kutoa muhtasari katika sentensi moja kile aya hiyo inachofundisha.
Fundisha Mafundisho
“Familia ni kitovu cha mpango wa Muumbaji.’’
-
Kanisa linajulikana kwa mkazo wake kwa familia, na tangazo la familia linafunua sababu za kimafundisho za mkazo huo. Ili Kuhimiza mjadala kuhusu hili, ungeweza kuwaalika washiriki darasa kudhania kuwa mtu aliwauliza kwa nini kanisa linatilia sana mkazo familia. Je, ni ukweli gani kutoka kwenye tangazo tungeweza kutoa ili kujibu swali la mtu huyo?
-
Sababu moja ya tangazo la familia kuwa muhimu sana ni kwamba linathibitisha upya kweli ambazo ziko chini ya uvamizi katika siku yetu. Ni kweli zipi katika tangazo zinatusaidia tusidanganywe na maoni ya uwongo kuhusu familia katika ulimwengu wa sasa? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinashawishi chaguzi tunazofanya? Kauli ya Mzee Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuongezea katika mjadala huu.
“Furaha katika maisha ya familia itapatikana kwa urahisi ikiwa imejengwa katika mafundisho ya Bwana Yesu Kristo.’’
-
Kujadili kanuni zilizoko katika aya ya sita na saba ya tangazo la familia ingesaidia washiriki wa darasa lako kupata furaha kuu zaidi katika mahusiano yao ya kifamilia. Fikiria juu ya kuorodhesha kanuni hizi ubaoni na waalike washiriki wa darasa kuchagua kanuni ili kuzijadili wawili wawili. Wangeweza kutumia maswali kama haya kuongoza mijadala yao: Ni mifano ipi ya kanuni hii tumeona katika maisha ya familia? Ni jinsi gani kuishi kanuni hii kutaongoza kwenye furaha katika familia zetu? Ni jinsi gani kuishi kanuni hii kunasaidia kumfanya Mwokozi kuwa msingi wa maisha yetu ya kifamilia? Maandiko yapi yangesaidia familia zetu kuelewa kanuni hii vyema zaidi? (Washiriki wa darasa wangeweza kupata maandiko kwa kutumia Mwongozo wa Mada au Mwongozo wa Maandiko [scriptures.ChurchofJesusChrist.org].) Kila jozi ingeweza kulielezea darasa kile walichopata.
Sisitiza kuwa licha ya hali ya sasa ya familia zetu, tunaweza kujitahidi kujenga familia ya milele juu ya msingi wa Mwokozi na injili Yake.
“Tunatoa wito kwa wananchi wenye kuwajibika … kukuza hatua hizo zilizoundwa ili kuendeleza na kuimarisha familia.”
-
Ni jinsi gani utaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kufahamu jukumu lao la kushikilia kweli zilizoko katika tangazo la familia? Ili kuanza mjadala, unaweza kujadili kile washiriki wa darasa wanachojifunza kutokana na kichwa cha habari cha tangazo. Je, tangazo ni nini? Ni nini kiliwawezesha Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili kutoa tangazo kwa ulimwengu kuhusu familia? Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha kile wanachofikiri kuwa ni ujumbe mkuu wa tangazo (wahimize kuonesha vipengele mahususi). Kisha wajadili njia za kuutangaza ujumbe huu katika jumuiya au taifa lao. Ujumbe wa Dada Bonnie L. Oscarson “Watetezi wa Tangazo la Familia” una mifano ambayo mnaweza kuifanyia marejeo pamoja kama darasa (Ensign au Liahona, Mei 2015, 14–17). Pia mnaweza kutazama video “Defenders of the Faith” (ChurchofJesusChrist.org).
Nyenzo za Ziada
Familia katika mpango wa Mungu.
Rais Dallin H. Oaks alifundisha:
“Watakatifu wa siku za Mwisho wanaoelewa mpango wa Mungu wa wokovu wana mtazamo wa kipekee unaowasaidia kuona sababu kwa amri za Mungu, asili isiyobadilika ya ibada Zake zinazohitajika, na jukumu muhimu la Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Upatanisho wa Mwokozi wetu huturudisha kutoka kwenye kifo na, kwa sharti la toba yetu, hutuokoa kutokana na dhambi. Kwa mtazamo huo, Watakatifu wa Siku za Mwisho wana vipaumbele na tamaduni za kipekee na wanabarikiwa kwa nguvu ya kuvumilia vurugu na maumivu ya maisha katika mwili wenye kufa. …
“Mpango wa injili kila familia inaopaswa kuufuata ili kujiandaa kwa ajili ya uzima wa milele na kuinuliwa umewekwa kimuhtasari katika tangazo la Kanisa la 1995, ‘Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.’ Maazimio yake, kwa kweli, yana muonekano tofauti na sheria za sasa, mila, na utetezi wa ulimwengu ambamo tunaishi. Katika siku yetu, tofauti zilizo dhahiri sana ni kukaa kinyumba bila ndoa, ndoa ya jinsia moja, na kulea watoto katika mahusiano hayo. Wale ambao hawaamini au hawatamani kuinuliwa na wanashawishiwa sana na njia za ulimwengu hufikiria tangazo hili la familia kama maelezo ya sera ambayo inapaswa kubadilishwa. Tofauti na hayo, Watakatifu wa Siku za Mwisho wanathibitisha kuwa tangazo la familia linafafanua aina ya mahusiano ya kifamilia ambapo sehemu muhimu zaidi ya maendeleo yetu ya milele inaweza kutokea” (“Mpango na Tangazo,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 29).