Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 and 2: “Tunaamini”


“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2: ‘Tunaamini,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapil: 2021

blanketi likionesha mikono yenye rangi nyingi za ngozi

Kwa Wanaume Wote Wenye Kustahili, na Emma Allebes

Desemba 6–12

Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2

“Tunaamini’’

Kwa maombi soma Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2, na tafuta mwongozo wa kiungu wa Roho Mtakatifu unapopanga uzoefu wenye maana wa kujifunza kwa washiriki wa darasa siku ya Jumapili.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kukamilisha kauli ifuatayo: “Nina furahi kuwa nilisoma maandiko wiki hii kwa sababu …”

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Makala ya Imani

Makala ya Imani ina kweli za kimsingi za injili iliyorejeshwa.

  • Hii hapa ni njia ya kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki na wengine kile walichopata hasa kilicho na maana katika Makala ya Imani: Unaweza kuandika namba 1 hadi 13 kwenye ubao na kuwataka washiriki wa darasa kuandika kando ya namba hizo kitu walichojifunza kutoka kwenye makala hiyo ya Imani. Je, ni tofauti gani kweli hizi zinaleta katika uhusiano wetu na Wazazi Wetu wa Mbinguni na Yesu Kristo? Pengine washiriki wa darasa wanaweza kuelezea jinsi Makala ya Imani yalivyozidisha kujifunza kwao injili au zilivyowasaidia kushiriki injili na wengine.

Makala ya Imani 1:9; Matamko Rasmi 1 na 2

Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa kwa ufunuo.

  • Kwa nini ufunuo endelevu ni muhimu kwetu? Waalike washiriki wa darasa kuelezea hisia zao kuhusu swali hili. Washiriki wa darasa wanaweza pia kujadili jinsi kanuni ya ufunuo endelevu inavyohusiana na Matamko Rasmi 1 na 2. (Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza nyenzo za msaada zinazohusiana na mafunuo haya.) Tunajifunza nini kutoka kwa Tamko Rasmi 1 na 2 kuhusu nafasi ya ufunuo katika kuliongoza Kanisa? (ona pia Makala ya Imani 1:9 na maelezo ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada”). Washiriki wa darasa wanaweza kufikiria mifano gani mingine ya ufunuo endelevu? Ufunuo huu unagusaje maisha yetu na kutusaidia kujenga ufalme wa Baba wa Mbinguni?

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kufanyia marejeo Tamko Rasmi 1 na 2 na kuelezea kitu kutoka kwenye mafunuo haya ambacho kinaweza kumsaidia mtu ambaye anahangaika kukubali mabadiliko ya hivi karibuni ya sera, ufunuo, au mafundisho ya Kanisa. Je, ni kwa namna gani washiriki wa darasa wamejifunza kumwamini Mungu wakati wanahangaika na kitu fulani katika Kanisa ? Je, ni kwa namna gani kujifunza kwao wiki hii kumeimarisha imani yao kwamba Bwana analiongoza Kanisa Lake? Utambuzi kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf katika “Nyenzo za Ziada” unaweza pia kusaidia.

    mchoro wa Wilford Woodruff

    Wilford Woodruff, na H. E. Peterson

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

“Roho wa Mungu alikuwepo pale.”

Rais Gordon B. Hinckley alikuwa akihudumu kama mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wakati ambapo ufunuo ambao umeelezwa katika Tamko Rasmi 2 ulipopokelewa. Miaka kadhaa baadaye alielezea uzoefu wake:

“Kulikuwa na hali takatifu na ya utakaso katika chumba. Kwangu, ilionekana kana kwamba bomba limefunguka kati ya kiti cha enzi cha mbinguni na nabii wa Mungu aliyepiga magoti chini, akisihi akiungana na viongozi wenzake wa ukuhani. Roho wa Mungu alikuwa pale. Na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kulikuja kwa nabii huyo hakikisho kwamba jambo ambalo aliliomba lilikuwa sahihi, kuwa wakati ulikuwa umefika, na kuwa baraka za ajabu za ukuhani zilipaswa kuenezwa kwa wanaume wanaostahili bila kujali ukoo.

“Kila mwanadamu katika mkusanyiko huo, kwa nguvu za Roho Mtakatifu, alijua kitu hicho.

“Ilikuwa ni tukio lenye utulivu na unyenyekevu. … Bila sauti ya kusikika kwa masikio yetu ya kimwili iliweza kusikika. Lakini sauti ya Roho ilinong’oneza kwa hakikisho katika akili zetu na nafsi zetu” (“Urejesho wa Ukuhani,” Ensign, Okt. 1988, 70).

“Ni asili kuwa na maswali.”

Rais Dieter F. Uchtdorf alisema maneno yafuatayo kwa wale ambao walikuwa na shaka kuhusu historia ya Kanisa au mafundisho:

“Ni jambo la kawaida kuwa na maswali—mbegu ya uchunguzi wa uaminifu mara nyingi imemea na kukomaa na kuwa mwaloni mkubwa wa ufahamu. Kuna washiriki wachache wa Kanisa ambao, kwa wakati mmoja au mwingine, hawajapigana na maswali makubwa au maswali nyeti. Mojawapo ya madhumuni ya Kanisa ni kulea na kukuza mbegu ya imani—hata katika nyakati zingine katika udongo wa kichanga wa shaka na ukosefu wa uhakika. Imani ni kuwa na matumaini kwa mambo ambayo hayaonekani lakini ni ya kweli.

“Kwa hiyo, wapendwa kaka zangu na dada zangu, marafiki zangu wapendwa tafadhalini, kwanza tilieni shaka mashaka yenu kabla ya kutilia shaka imani yenu. Ni lazima tusiruhusu shaka kutuweka mahabusu na kutufungia kupata upendo, amani, na zawadi za kiroho ambazo huja kupitia imani katika Bwana Yesu Kristo” (“Njoo, Jiunge Nasi,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 23; ona pia Lawrence E. Corbridge, “Stand Forever” [Brigham Young University devotional, Jan. 22, 2019], speeches.byu.edu).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ni SAWA kusema, “Sijui.” Huku unapopaswa kufanya kadiri uwezavyo kuwasaidia washiriki wa darasa kujibu maswali yao kuhusu injili, Bwana hategemei wewe ujue kila kitu. Iwapo hujui jinsi ya kujibu kitu, kubali. Kisha elekeza wanafunzi wako kwenye mafundisho yaliyofunuliwa, na utoe ushuhuda wa kweli wa kile unachojua. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,24.)