Mafundisho na Maagano 2021
Mpangilio wa Kufundisha


“Mpangilio wa Kufundisha,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mpangilio wa Kufundisha,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
darasa limeketi katika mduara

Mpangilio wa Kufundisha

Kila muhtasari kwenye nyenzo hii hufuata mpangilio wa kualika kushiriki na kufundisha mafundisho.

Picha
ikoni ya kushiriki na wengine

Alika Kushiriki

Kama sehemu ya kila darasa, waalike washiriki wa darasa kushiriki na wengine utambuzi na uzoefu waliokuwa nao wiki iliyopita walipojifunza binafsi na kama familia maandiko na kutenda juu ya walichojifunza. Wasaidie washiriki wa darasa kuona kwamba kujifunza kwao binafsi nje ya darasa ni muhimu. Uongofu wao binafsi utakuja sio tu kupitia mafunzo ya Jumapili bali pia kupitia matukio yao ya kila siku. Wakati washiriki wa darasa wanaposikia uzoefu na ushuhuda wa kila mmoja wao kuhusu injili ya Yesu Kristo, wana uwezekano wa kutafuta uzoefu sawa na huo wa kwao wenyewe.

Si kila mmoja atakuwa ameshasoma sura za kila somo, na hata baadhi ya wale waliosoma wanaweza kuhisi hofu kushiriki na wengine. Hakikisha washiriki wote wa darasa wanahisi kuwa sehemu ya thamani ya darasa, bila kujali wana kitu cha kushiriki na wengine au la.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Wewe na washiriki wa darasa lako mnapaswa kufokasi katika Yesu Kristo na mafundisho yake—kweli za milele za injili—zinazopatikana katika aya za maandiko zilizotolewa. Unapojadili mafundisho rasmi kutoka kwenye maandiko, ni mistari ipi, dondoo zipi, uzoefu upi, maswali yapi, na nyenzo zipi za ziada ungeweza kushiriki na wengine? Ungewezaje kutumia nyenzo hizi kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua na kuelewa kanuni za injili? Je, unawezaje kuwasaidia kujenga imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Chapisha