Mafundisho na Maagano 2021
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Nyenzo za Ziada

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika programu ya Makataba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kutohoa shughuli zozote kutoka kwenye nyenzo hii kwa matumizi katika darasa lako la Shule ya Jumapili. Kama washiriki wa darasa wametumia shughuli hizi katika kujifunza kwao binafsi injili au kama familia, wahimize kushiriki na wengine uzoefu na utambuzi wao.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kwa nyongeza kwa matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata nyimbo nyingi na nyimbo za watoto zilizorekodiwa kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika app za Sacred Music na Gospel Media.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya kiada vya seminari na chuo vinatoa chimbuko la kihistoria na fasili ya mafundisho kwa kanuni zinazopatikana katika maandiko. Vinaweza pia kuchochea mawazo ya kufundisha kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili.

Mamajarida ya Kanisa

Majarida ya New Era, Ensign, na Liahona yanatoa makala na habari za ziada ambazo zinaweza kuongezea kwenye kanuni ambazo unafundisha kutoka katika Mafundisho na Maagano.

Mada za Injili

Kwenye Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org) unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo saidizi kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa majibu ya kina ya maswali ya injili na ya kihistoria.

mtu akijifunza taarifa za Kanisa

Preach My Gospel

Mwongozo huu wa wamisionari hutoa maelezo ya jumla ya kanuni za msingi za injili.

Kwa Nguvu ya Vijana

Nyenzo hii inaonesha viwango vya Kanisa vinavyowasaidia vijana na wengine kuwa wanafunzi waaminifu wa Yesu Kristo. Fikiria kuirejelea mara kwa mara, hasa ikiwa unawafundisha vijana.

Video na Sanaa

Sanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media library katika ChurchofJesusChrist.org ili kupitia pitia mkusanyiko wa nyenzo za vyombo vya habari za Kanisa. Nyenzo hizi pia zinapatikana kwenye app ya Gospel Media, na pia taswira nyingi zinapatikana kwenye Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Ufunuo katika Muktadha

Ufunuo katika Muktadha: Hadithi inayohusu Sehemu za Mafundisho na Maagano ni mkusanyiko wa insha kuhusu hadithi inayozunguka ufunuo ulio kwenye Mafundisho na Maagano. Muktadha uliotolewa kwenye nyenzo hii unaweza kukusaidia kuelewa vyema kile ambacho maneno ya Mungu katika Mafundisho na Maagano yanaweza kuwa yamemaanisha kwa Watakatifu wa Siku Mwisho.

Watakatifu

Watakatifu ni historia ya hadithi simulizi juu ya Kanisa. Juzuu ya 1, Standard of Truth, na juzuu ya 2, No Unhallowed Hand, zinaangazia kipindi hicho hicho cha historia ya Kanisa kama vile Mafundisho na Maagano. Historia hizi zinaweza kukupa umaizi wa muktadha unaozunguka ufunuo unaousoma kwenye Mafundisho na Maagano.

Mada za Historia ya Kanisa

Makala nyingi kuhusu watu, michoro, jiografia, na matukio ya historia ya Kanisa yanaweza kupatikana katika ChurchofJesusChrist.org/study/history/topics.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Nyenzo hii inaweza kukusaidia kujifunza na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kufanyiwa kazi katika mikutano ya baraza la walimu.