Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1: ‘Sikilizeni, Enyi Watu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
Desemba 28–Januari 3. Mafundisho na Maagano 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Desemba 28–Januari 3
Mafundisho na Maagano 1
“Sikilizeni, Enyi Watu”
Unaposoma Mafundisho na Maagano 1, fikiria kuhusu mistari ambayo ungeweza kuisisitiza darasani na jinsi ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka mistari hii.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ungeweza kuanza kujifunza kwenu darasani Mafundisho na Maagano kwa kuwauliza washiriki wa darasa jinsi wanavyohisi kuhusu kujifunza kitabu hiki cha maandiko mwaka huu. Ni kifungu gani kutoka sehemu ya 1 kinawasaidia kuhisi shauku ya kusoma Mafundisho na Maagano? Labda ungeweza kuwaomba wapekue sehemu ya 1 kwa ajili ya mstari wanaoweza kushiriki kama wangekuwa wanajaribu kumshawishi mtu asome kitabu kitakatifu.
Fundisha Mafundisho
Bwana anatualika “zichunguzeni amri hizi.”
-
Mnapojadili “dibaji” ya Bwana kwa Mafundisho na Maagano (mstari wa 6), ingeweza kusaidia kwa mtu katika darasa kuelezea dibaji ni nini na madhumuni inayotimiza katika kitabu. Kisha darasa lingeweza kujadili jinsi sehemu ya 1 inatimiza madhumuni hayo kwa ajili ya Mafundisho na Maagano. Kwa mfano, ni mada zipi za kitabu sehemu ya 1 inatambulisha? Je, kitabu kina madhumuni gani? Tunapata nini katika sehemu hii ambacho kinaweza kuathiri jinsi ambavyo tunasoma Mafundisho na Maagano mwaka huu?
-
Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unatualika tufikirie jinsi tutakavyoshika amri ya Bwana ya “kuzichunguza amri hizi.” (mstari wa 37). Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile wanachopanga kufanya mwaka huu kufanya kujifunza kwao Mafundisho na Maagano kuwa kwenye tija. Je, watatafuta nini? Ni kwa jinsi gani kupekua ni tofauti na kusoma tu? Ni mbinu gani za kujifunza wameona kuwa zina usaidizi mkubwa.
Mafundisho na Maagano 1:1–6, 23–24, 37–39
Mungu huzungumza kupitia Watumishi Wake, na maneno Yake yatatimizwa.
-
Wengi wetu tunao wanafamilia, marafiki, na watu tunaowajua ambao hawashiriki imani yetu kuhusu manabii walio hai. Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kweli walizopata katika sehemu ya 1 ambazo wanaweza kuzitumia kumjibu mtu ambaye anashuku imani yao kuhusu manabii. Ungeweza kupendekeza kwamba watafute hasa katika mistari ya 1–6 na 37–39. Mistari hii inafundisha nini kuhusu Bwana na manabii Wake?
-
Washiriki wa darasa wangeweza kuvutiwa kujifunza kwamba wakati baraza lililoitwa na Joseph Smith kujadili uchapishaji wa ufunuo wa Nabii, baadhi ya wanabaraza walipinga wazo hilo. Waliona aibu kwa ajili ya udhaifu wa Joseph katika kuandika, na walikuwa na wasiwasi kwamba kuchapisha ufunuo huo kungeweza kukasababisha matatizo zaidi kwa Watakatifu (ona Watakatifu 1:140–43). Ni kwa jinsi gani sehemu ya 1 inazungumzia wasiwasi huu? (ona, kwa mfano, mistari ya 6, 24, 38).
-
Maneno ya wimbo wa injili “Njoo, Sikiliza Sauti ya Nabii” (Nyimbo za Injili, na. 21) hufundisha baadhi ya kanuni sawa na zile zinazofundishwa katika sehemu ya 1. Labda mngeweza kuimba au kusoma wimbo wa injili pamoja kisha uwaalike washiriki wa darasa watafute mistari katika wimbo huo wa injili na katika sehemu ya 1 ambayo inafundisha kanuni sawa.
Mafundisho na Maagano 1:12–30, 35–36
Bwana alirejesha injili Yake ili kutusaidia kukabiliana na changamoto za siku za mwisho.
-
Ni fikra gani washiriki wa darasa huwa nazo wasomapo maelezo ya siku za mwisho katika mistari ya 13–16? Ni nini kinatendeka duniani siku hizi ambacho kinatimiza maelezo haya yaliyotabiriwa? Wahimize washiriki wa darasa washiriki kitu chochote walichokipata katika sehemu ya 1 ambacho kiliwasaidia kuhisi amani na ujasiri licha ya changamoto za siku zetu.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari baraka ambazo tunazo kwa sababu injili imerejeshwa, ungeweza kuandika ubaoni Ni nini mistari ya 17–23 inafundisha kuhusu kwa nini Bwana alirejesha injili Yake? Washiriki wa darasa wangeweza kupekua mistari hii na kushiriki mawazo yao wao kwa wao. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani kweli ambazo zilirejeshwa kupitia kwa Joseph Smith zimetusaisia kuongeza imani yetu? (ona mstari 21).
Bwana hutumia “vidhaifu na vya kawaida” kutekeleza kazi Yake.
-
Mojawapo ya mada muhimu ya Mafundisho na Maagano 1 ni kazi ya “vidhaifu na vya kawaida” katika kazi kuu ya Bwana katika siku za mwisho (mstari wa 23). Waalike washiriki wa darasa wapekue mistari ya 19–28 kujifunza jinsi maneno “dhaifu” na “kawaida” yanatumika kwa watumishi wa Bwana. Wakati wakishiriki walichokipata, mngeweza kujadili maswali kama haya: Ni sifa zipi Bwana anawataka watumishi Wake wawe nazo? Ni kipi Bwana atatimiza kupitia kwa watumishi Wake katika siku za mwisho? Ni kwa jinsi gani unabii katika mistari hii unatimizwa kote ulimwenguni na katika maisha Yetu?