“Januari 4–10. Historia ya—Joseph Smith 1:1–26: ‘Niliona Nguzo ya Mwanga,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Januari 4–10. Historia ya—Joseph Smith 1:1–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021
Januari 4–10
Historia ya—Joseph Smith 1:1–26
“Niliona Nguzo ya Mwanga”
Kumbuka kwamba matayarisho yako muhimu zaidi yatakuwa kujifunza maandiko na kuishi kulingana na kile unachojifunza. Roho anaweza kukusaidia ujue kile unachoweza kufokasi juu yake darasani.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ni umaizi gani washiriki wa darasa walipata walipokuwa wakijifunza Historia ya—Joseph Smith 1:1–26 wiki hii? Labda unaweza kuonyesha picha ya Joseph Smith au ya Ono la Kwanza na waalike washiriki wa darasa waandike ubaoni baadhi ya umaizi kutokana na kujifunza kwao, pamoja na mistari walipoipata. Pia wanaweza kushiriki jinsi ushuhuda wao wa Joseph Smith na kazi yake uliongezeka walipokuwa wakijifunza juu yake wiki hii.
Fundisha Mafundisho
Historia ya—Joseph Smith 1:5–18
Tunapoomba kwa imani, Mungu atatujibu.
-
Washiriki wa darasa lako wanaweza kuelewa hamu ya Joseph kutafuta ukweli katika ulimwengu ambamo mawazo mengi yanayokinzana yanafundishwa. Je, ni kwa namna ipi mkanganyiko katika siku zetu uko sawa na ule aliokuwa nao? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi tunavyoweza kupata majibu ya maswali yetu, unaweza kuwaalika waorodheshe ubaoni njia tofauti ambazo watu huutafuta ukweli. Kisha wanaweza kufanya mapitio ya Historia ya—Joseph Smith 1:5–18 na waongeze kwenye orodha kile Joseph Smith alikifanya kutafuta majibu ya maswali yake.
-
Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki jinsi ambavyo wameweza kufuata mfano wa Joseph Smith katika uchunguzi wao wa kutafuta ukweli na jinsi Mungu amewajibu. Kauli ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada” inapendekeza baadhi ya njia tungeweza kuutafuta ukweli toka kwa Mungu.
Historia ya—Joesph Smith 1:15–20.
Joseph Smith alimuona Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.
-
Ono la Kwanza lilifunua kweli kadhaa kuhusu Mungu ambazo zilikinzana na yale ambayo wengi katika siku za Joseph waliyaamini. Washiriki wa darasa wangeweza kusoma Historia ya—Joseph Smith 1:15–20 na kutambua kitu ambacho wanajifunza kuhusu Mungu. Kwa nini ni muhimu kuzijua kweli hizi kuhusu Mungu?
-
Kama Joseph Smith angetembelea darasa letu, tungemuuliza nini kuhusu uzoefu wake? Video “Ask of God: Joseph Smith’s First Vision” (ChurchofJesusChrist.org) zinaweza kuwapatia washiriki wa darasa umaizi zaidi kuhusu Ono la Kwanza la Joseph Smith (ona pia “Nyenzo za Ziada”). Pengine wanaweza kutafakari jinsi wanavyoweza kukamilisha sentensi kama hii: “Kwa sababu Ono la Kwanza lilitokea, ninajua kwamba …” Ni baraka zipi zimekuja maishani mwetu kwa sababu ya Ono la Kwanza?
6:35 -
Kwa kuongezea kwenye mjadala wako, washiriki wa darasa wangeweza kusoma au kuimba “Sala ya Kwanza ya Joseph Smith” (Nyimbo za Injili na. 26). Ni nini wimbo huu wa injili unatusaidia kuelewa na kuhisi kuhusu Ono la Kwanza? Labda baadhi ya washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi ambavyo wamekuja kujua kwamba Joseph kweli alimuona Mungu Baba na Yesu Kristo katika Kijisitu Kitakatifu. Au unaweza kuwaalika wamisionari (au mmisionari aliyekamilisha misheni) kutembelea darasa na kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo Ono la Kwanza limeathiri maisha ya watu wanaowafundisha.
Historia ya—Joseph Smith 1:21–26
Tunaweza kubaki waaminifu katika kile tunachokijua hata kama wengine watatukataa.
-
Washiriki wa darasa wanaweza kuwa na uzoefu wa baadhi ya vitu ambavyo Joseph Smith alipitia wakati alipoanza kuwaambia watu wengine kuhusu ono lake (ona Historia ya —Joseph Smith 1:21–26). Labda wanaweza kushiriki vifungu ambavyo vinawatia msukumo wakati wengine wanapopinga imani yao.
-
Kama unajua kuhusu washiriki wa kata ambao wamekumbana na upinzani kwa sababu wao ni washiriki wa Kanisa, fikiria kuwaomba kuja darasani wakiwa wamejiandaa kushiriki jinsi ambavyo wanaweka imani yao imara. Tunajifunza nini kutoka kwa mfano wa Joseph Smith katika Historia ya —Joseph Smith 1:21–26?
Nyenzo za Ziada
Fuata mfano wa Joseph.
Rais Russell M. Nelson alifundisha:
“Nabii Joseph Smith aliweka mfano kwa ajili yetu sisi ili kuufuata katika kutatua maswali yetu. Akivutiwa na ahadi ya Yakobo kwamba kama tunapungukiwa na hekima na tuombe dua kwa Mungu [ona Yakobo 1:5], kijana Joseph alipeleka swali lake moja kwa moja kwa Baba wa Mbinguni. Alitafuta ufunuo binafsi, na utafutaji wake ulifungua kipindi hiki cha mwisho cha maongozi ya Mungu.
“Kwa namna hii, utafutaji wako utafungua nini kwa ajili yako? Ni hekima gani unayopungukiwa? Ni nini unakiona ni muhimu kukijua au kukielewa? Fuata mfano wa Nabii Joseph. Tafuta sehemu ya ukimya ambako utakwenda mara kwa mara. Jinyenyekeze mbele za Mungu. Mimina moyo wako kwa Baba yako wa Mbinguni. Mgeukie kwa ajili ya majibu na faraja” (“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 95).
Ono la Kwanza la Joseph Smith.
Kusoma maelezo ya Ono la Kwanza ambalo linagusia juu ya matukio kadhaa ya Joseph Smith, ona Watakatifu, 1:14–16.