Mafundisho na Maagano 2021
Januari 18–24. Mafundisho na Maagano 3–5: “Kazi Yangu Itaendelea Mbele”


“Januari 18–24. Mafundisho na Maagano 3–5: ‘Kazi Yangu Itaendelea Mbele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Januari 18–24. Mafundisho na Maagano 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2021

Picha
watu wakifanya kazi shambani

Wakati wa Mavuno Ufaransa, na James Taylor Harwood

Januari 18–24

Mafundisho na Maagano 3–5

“Kazi Yangu Itaendelea Mbele”

Kujifunza Mafundisho na Maagano 3–5 kabla ya kufanya mapitio ya mawazo katika mwongozo huu kutakusaidia kupokea misukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kukusaidia kuelewa historia ambayo ilisababisha kutolewa kwa ufunuo ulioandikwa katika sehemu hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache ili wapitie maandiko waliyosoma nyumbani na kutafuta kifungu walichokiona kuwa cha maana. Kisha waalike washiriki kushiriki kile walichojifunza pamoja na mtu mwingine darasani.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mafundisho na Maagano 3:1–15

Tunapaswa kumuamini Mungu badala ya kumwogopa mwanadamu.

  • Kama Joseph Smith, sisi sote tumepata uzoefu wa wakati tulihisi kushawishiwa na watu wengine kufanya kitu tunachofahamu kuwa ni kibaya. Tunajifunza kweli zipi kutoka Mafundisho na Maagano 3:1–15 ambazo zinaweza kutusaidia kubaki waaminifu kwa Mungu katika hali kama hizi?

  • Joseph Smith alihitaji kurudiwa kwa kumuogopa binadamu kuliko Mungu, lakini pia alihitaji kutiwa moyo. Waalike washiriki wa darasa waichunguze sehemu ya 3 kuona jinsi Bwana alimrudi na kumtia moyo Joseph. Kwa mfano, wangeweza kuorodhesha ubaoni virai kutoka mistari ya 1–15 vilivyo na makaripio ya Bwana na virai vingine vilivyo na kutiwa moyo kwake atubu na azidi kuwa mwaminifu. Je, uzoefu wa Joseph Smith unatufundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyotusaidia kushinda makosa yetu?

Mafundisho na Maagano 4

Bwana anatutaka tumtumikie na mioyo yetu yote.

  • Sifa zinazowaelezea watumishi wa Bwana ambazo zimeorodheshwa katika Mafundisho na Maagano 4:5–6 pia ni sifa za Yesu Kristo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza zaidi, ungeweza kuwaalika wachague mojawapo ya sifa hizi na watafute ufafanuzi au maandiko ya ziada ambayo yanawasaidia kuelewa vyema zaidi sifa hiyo (ona, kwa mfano, maneno ya Dada Elaine S. Dalton katika “Nyenzo za Ziada). Kisha ungeweza kuwaomba watu wachache washiriki kile walichopata. Pia wanaweza kushiriki kwa nini sifa waliyoichagua ni sharti la huduma katika ufalme wa Mungu. Tunawezaje kukuza zaidi sifa hizi? (ona mstari wa 7).

  • Mafundisho na Maagano 4 ilitolewa kwa ajili ya Joseph Smith Mkubwa., ambaye alitaka kujua jinsi ambavyo angeweza kutoa msaada katika kazi ya Bwana. Sehemu hii pia inaweza kumsaidia yeyote kati yetu ambaye ana hamu ya kumtumikia Bwana. Hii ni njia moja ya kujifunza sehemu hii: washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi katika makundi madogo kuandika maelezo ya kazi kwa ajili ya watumishi wa Mungu, wakitumia sehemu ya 4 kama mwongozo. Je, ni kwa namna gani sifa hizi zina utofauti na sifa za kazi zingine? Kwa nini sifa hizi ni muhimu katika kufanya kazi ya Mungu? Kauli ya Mzee David A. Bednar katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa kukuza sifa hizi.

Mafundisho na Maagano 5

Ushuhuda wa ukweli huja kwa wale ambao ni wanyenyekevu na waaminifu.

  • Kama bamba za dhahabu zingeonyeshwa wazi kwa dunia, je, hilo lingeshawishi kila mtu kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli? Kwa nini au kwa nini sivyo? (ona Mafundisho na Maagano 5:7). Labda washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza sehemu ya 5 kwa ajili ya umaizi ambao unaweza kuwasaidia kumjibu mtu anayetafuta ushahidi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Je, ni nini Bwana aliwafundisha Joseph Smith na Martin Harris ambacho kinaweza kutusaidia kupata ushuhuda wetu wenyewe kuhusu kweli za injili?

    Picha
    Martin Harris

    Martin Harris, na Lewis A. Ramsey

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Maadili humaanisha nguvu.

Dada Elaine S. Dalton alitoa maelezo haya kuhusu maadili: “Maadili ni neno ambalo huwa hatulisikii kwa kawaida katika jamii ya sasa, lakini neno la kiasili la Kilatini virtus linamaanisha nguvu. Wanawake na wanaume wema huwa na heshima tulivu na nguvu ya ndani. Ni wenye kujiamini kwa sababu wao wanastahili kupokea na kuongozwa na Roho Mtakatifu.” (“A Return to Virtue,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 79).

Kuwa mmisionari.

Mzee David A. Bednar alisema: “Mchakato wa kuwa mmisionari hauhitaji mvulana kuvaa shati jeupe na tai [au msichana kuvaa rinda] kwenda shuleni kila siku au kufuata mwongozo wa wamisionari kwa ajili ya kulala au kuamka. … Lakini unaweza kuongeza hamu yako ya kumtumikia Mungu [ona Mafundisho na Maagano 4:3], na unaweza kuanza kufikiria kama wamisionari wanavyofikiria, kusoma kile wamisionari wanachosoma, kusali kama wamisionari wanavyosali, na kuhisi kile wamisionari wanachohisi. Unaweza kuepuka shinikizo za kidunia ambalo husababisha Roho Mtakatifu kujiondoa, na unaweza kukua katika kujiamini katika kutambua na kuitikia misukumo ya kiroho.” (“Kuwa Mmisionari,” Ensign au Liahona, Nov. 2005, 45–46).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza Maswali yanayohimiza mjadala wenye tija. Maswali ambayo yana zaidi ya jibu moja sahihi huwaalika wanafunzi kujibu kulingana na mawazo, hisia, na uzoefu wao binafsi. Kwa mfano, unaweza kuuliza, “Je, unajuaje wakati Mungu anazungumza nawe?” (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 33.)

Chapisha