Njoo, Unifuate
Februari 11–17. Yohana 2–4: ‘Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili’


“Februari 11–17. Yohana 2–4: ‘Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)

“Februari 11–17. Yohana 2–4,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Yesu akizungumza na Nikodemo

Februari 11–17

Yohana 2–4

“Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili”

Kusoma Yohana 2–4 ni njia mzuri kuanza kujiandaa kufundisha. Andika misukumo ya kiroho yoyote unayopokea, na tumia muhtasari huu kutafuta umaizi wa ziada na mawazo ya kufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Andika vichwa vya habari vitatu ubaoni: Yohana 2, Yohana 3, na Yohana 4. Wape washiriki wa darasa dakika chache kurejea sura hizi, na kisha waombe waandike chini ya kila kichwa cha habari aya ambayo iliwasaidia kuelewa maandiko na matukio katika sura ile. Jadili aya walizoandika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yohana 2:1–11

Maisha yetu yamebadilika tunapomfuata Yesu Kristo.

  • Wakati mwingine tunaweza kupata umaizi kwa kutilia maanani kila kitu katika matukio ya kimaandiko. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Yohana 2:1–11 na kuorodhesha utondoti ambao unaongeza kina cha shukrani zao kwa muujiza kwenye karamu ya harusi. Ni kwa jinsi gani muujiza huu unadhihirisha utukufu wa Mungu? (ona aya 11).

  • Inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa hadithi hii kama watafikiria muujiza huu kwa mtazamo wa kipekee wa wale walioushuhudia. Mitizamo yetu wakati mwingine kwa miujiza inakuwaje kama ile ya watu kwenye karamu ya harusi—kwa mfano, kama Mariamu, ambaye alijua muujiza unaweza kutokea, au mtawala, ambaye hakuwa na habari kwamba muujiza umetokea? Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kutoa simulizi ya karamu kana vile wao walikuwa wa watu waliokuwepo pale.

Yohana 2:13–22

Tunaweza kutetea sehemu na vitu vitakatifu.

  • Unaweza kuwasidia vipi washiriki wa darasa kujifunza kutoka tukio la Yesu kuwafurusha nje ya hekalu wabadilishaji fedha? Wanawezaje kutetea sehemu na vitu takatifu kama nyumba, makanisa, mahekalu, na maandiko? Kauli hii kutoka kwa Rais David O. McKay inaweza kusaidia: “‘Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.’ (Yohana 2:16.) Kuchuma fedha na kutumia fedha, … kutafuta makosa, na hasa umbeya kuhusu majirani katika nyumba za ibada, kimsingi ni ukiukaji wa amri iliyotolewa karibu miaka elfu mbili iliyopita” (katika Taarifa ya Mkutano Mkuu, Okt. 1956, 7). Tunawezaje kudumisha utakatifu wa hekalu na sehemu zingine takatifu?

Yohana 3:1–21

Hatuna budi kuzaliwa mara ya pili ili tuingie ufalme wa Mungu.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa mwaliko wa Yesu wa kuzaliwa mara ya pili (on Yohana 3:3), unaweza kuwaalika washiriki umaizi wanaoupata kutoka kwa kile Mwokozi alichomfundisha Nikodemo katika aya hizi. Ni maneno na virai gani Yeye alitumia? Ni maandiko au kauli gani zingine kutoka kwa viongozi wa Kanisa zinaweza kupanua uelewa wa washiriki wa Kanisa kuhusu mwaliko huu? (Ona Mwongozo wa Maandiko, “Binadamu, Mpya, Kuzaliwa Upya Kiroho” kwa mifano ya kimaandiko; ona “Nyezo za Ziada” kwa maelezo kutoka viongozi wa Kanisa,)

  • Ni kwa jinsi gani waumini wa Kanisa wangeweza kumwelezea mtu fulani wa imani ingine kile inamaanisha kuzaliwa mara ya pili? Ni kwa jinsi gani wanaweza kujumuisha toba, ubatizo, na kuthibitishwa katika mazungumzo haya? Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kufanya mazoezi jinsi wangejibu swali hili na mtu aliyekaa karibu nao. Nukuu kutoka Nabii Joseph Smith katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuzidisha kwenye majadiliano haya.

  • Baadhi ya watu wanaamini kwamba mtu hawezi kubadilika kikweli; Nikodemo, hata hivyo, ni mfano wa mtu fulani aliyebadilika kama matokeo ya kuifuata injili ya Yesu Kristo. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuona hili, waalike kupekua Yohana 3: 1–2; Yohana 7:40–52; Yohana 19: 39–40. Tunajifunza nini kutoka vifungu hivi kuhusu mtazamo na imani ya Nikodemo? Alibadilika vipi baada ya muda? Ni mifano gani tunayoweza kushiriki kuhusu watu tunaowajua ambao wamebadilika kwa sababu ya injili?

  • Kumtazama mtoto au picha ya mtoto inaweza kuwapa washiriki wa darasa lako nafasi ya kufananisha ubora wa mtoto aliyezaliwa hivi karibuni na ubora wa mtu fulani ambaye amezaliwa upya kiroho.

Yohana 4:6–34

Yesu Kristo anatoa kwetu maji ya uhai na “nyama” ya kufanya kazi ya Mungu.

  • Miili yetu inahitaji chakula na maji kila siku. Yesu alirejea haya mahitaji ya kote wakati alipofundisha kwa wote mwanamke Msamaria na wafuasi Wake. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kile Mwokozi alikuwa anafundisha, unaweza kubandika picha za chakula na maji ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa kuandika chini ya kila picha kweli za kiroho ambazo Yesu alifundisha. Ni kwa jinsi gani kumwabudu Mungu katika roho na katika ukweli kunakata kiu chetu cha kiroho? Ni kwa jinsi gani njaa yetu ya kiroho itashibishwa kwa kufanya mapenzi ya Mungu?

    Picha
    Kijito cha maji

    Yesu Kristo anatoa kwetu maji ya uzima.

  • Kutafakari juu ya maendeleo ya ushuhuda wa mwanamke Msamaria kumhusu Yesu Kristo kunaweza kuwasaidia washiriki wako wa darasa kutafakari jinsi walivyoweza kujua Yeye ni Masiya. Kama darasa, watafute istilahi mwanamke Msamaria alitumia kumrejea Mwokozi katika Yohana 4:6–30. Istilahi hizi zinadokeza nini kuhusu uelewa wake wa Yesu? Tumekua vipi katika ushuhuda wetu kwamba Yeye ni Mwokozi wetu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Mathayo 5 na Luka 6, waambie kwamba sura hizi zina kile ambacho Rais Joseph F. Smith alikiita “[mahubiri] muhimu sana ambayo yaliwahi kuhubiriwa, kwa kadri tunavyojua” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith [2013], 234).

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Yohana 2–4

Video za matendo na mafundisho ya Yesu.

“Yesu Anabadili Maji kuwa Divai,” “Yesu Anasafisha Hekalu,” “Yesu Anafundisha juu ya Kuzaliwa Mara ya Pili,” “Yesu Anamfundisha Mwanamke Msamaria” (LDS.org)

Inamaanisha nini kuzaliwa mara ya pili.

Nabii Joseph Smith alifundisha: “Vivyo hivyo mngeweza kubatiza mfuko wa mchanga kama binadamu, kama haitafanyika kwa kuzingatia msamaha wa dhambi na kumpata Roho Mtakatifu. Ubatizo kwa maji bali ni nusu ya ubatizo, na hauna faida yoyote bila ya nusu ile nyingine—ambayo ni, ubatizo kwa Roho Mtakatifu.”(Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 95).

Mzee David A. Bednar alifundisha: “Uongofu … una nguvu sana, sio hafifu—kuzaliwa tena kiroho na mabadiliko ya msingi ya kile tunahisi, kile tunafikiria na kufanya, na vile tulivyo. Kwa kweli, kiini hasa cha injili ya Yesu Kristo inajumuisha mabadiliko ya msingi na ya kudumu katika asili yetu hasa inayowezeshwa kupitia utegemezi wetu kwenye ‘faida, na huruma, na neema ya Masiya Mtakatifu’ (2 Nefi 2:8). Na tunapochagua kumfuata Bwana, tunachagua kubadilishwa—kuzaliwa tena upya kiroho” (“Lazima Mzaliwe Upya Tena.” Ensign au Liahona Mei 2007, 20).

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Unaweza kuuliza, Kwa nini mabadiliko haya makuu hayatokei haraka zaidi kwangu mimi? Unapaswa kukumbuka kwamba mifano ya ajabu ya watu wa Mfalme Benyamini, Alma, na wengine kadha katika maandiko ni—ajabu na si kawaida. Kwa wengi wetu, mabadiliko ni taratibu zaidi na yanatokea kwa muda mrefu. Kuzaliwa mara ya pili, tofauti na kuzaliwa kwetu kimwili, ni mchakato badala ya tukio. Na kushiriki katika mchakato huo ni lengo kuu la maisha ya muda” (“Kuzaliwa Mara ya Pili.” Ensign au Liahona Mei 2008, 78).

Mzee Dallin H. Oaks alifundisha:

“Tulizaliwa mara ya pili wakati tulipoingia katika uhusiano wa agano na Mwokozi kwa kuzaliwa kwa maji na roho na kwa kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo. Tunaweza kufanya upya kuzaliwa upya kule kila siku ya Sabato wakati tunapokea sakramenti.

“Watakatifu wa Siku za Mwisho wanakiri kwamba wale waliozaliwa mara ya pili katika njia hii ni wana na mabinti pekee wa Yesu Kristo (ona Mosia 5:7; 15:9–13; 27:25). Hata hivyo, ili tupate baraka zilizokusudiwa kwa hali hii ya kuzaliwa mara ya pili, lazima bado tushike maagano yetu na kuvumilia hadi mwisho. Kwa wakati huu, kupitia neema ya Mungu, tumezaliwa mara ya pili kama viumbe vipya na uzazi upya wa kiroho na matarajio ya urithi mtakatifu” (“Je, Umeokolewa?” Ensign, Mei 1998, 56).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Mwalimu sio bora kuliko mwanafunzi. Jukumu lako kama mwalimu ni muhimu, lakini wewe sio chanzo tu cha mwongozo darasani. Wasaidie washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwa Roho na shiriki na kila mmoja kile wanachojifunza.

Chapisha