Njoo, Unifuate
Februari 4–10. Mathayo 4; Luka 4–5: ‘Roho wa Bwana Yu juu Yangu’


“Februari 4–10. Mathayo 4; Luka 4–5: ‘Roho wa Bwana Yu juu Yangu” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Februari 4–10. Mathayo 4; Luka 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Kristo amshinda Shetani.

Kristo Amshinda Shetani, na Robert T. Barret

Februari 4–10

Mathayo 4; Luka 4–5

“Roho wa Bwana Yu juu Yangu”

Unapojifunza Mathayo 4 na Luka 4–5, andika misukumo yako ya kiroho. Hii itakaribisha mwongozo juu ya njia bora ya kukidhi mahitaji ya darasa lako. Unaweza pia kufikiria kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia vile vile muhtasari huu kupata mawazo ya ziada.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Masomo ya wiki hii yanajumuisha kauli hii: “Wakashangaa mno kwa mafundisho yake: kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo” (Luka 4:32; ona pia Marko 1:22). Ni aya zipi washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kutoka katika sura hizi ambazo ziliwasaidia kuhisi ule uwezo wa kimafundisho wao wenyewe?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 4:1–11; Luka 4:1–13

Baba wa Mbinguni ametupa sisi nguvu na jinsi ya kukinza majaribu.

  • Tukio la Mwokozi akimkinza Shetani linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua njia ambazo Shetani anajaribu kuwajaribu. Washiriki wa darasa wanaweza kuchagua mojawapo ya majaribu katika Mathayo 4:1–14 au Luka 4:1–13 na wafikirie kuhusu majaribu ya kisasa, yaliyo sawa (kauli katika “Nyezo za Ziada” zinaweza kusaidia). Kwa nini inasaidia kujua kwamba Mwokozi alikabiliana na majaribu sawa na hayo tunayokabiliana nayo leo? Kwa nini Kristo aliweza kukinza majaribu? Kwa mifano mingine ya kimaandiko ya watu wakimkinza Shetani, ona Mwanzo 39:7–20; 2 Nefi 4:16–35; na Musa 1:10–22.

  • Njia mojawapo ya kuhimiza majadiliano kuhusu Mathayo 4:1–11 na Luka 4:1–13 inaweza kuwa ni kuandika maswali mawili ubaoni Tunajifunza nini kuhusu Kristo kutoka hadithi hii? Na Nini tunajifunza kuhusu Shetani? Kisha waalike washiriki wa darasa wapekue vifungu ili wapate majibu kwa maswali haya na kuandika majibu yao ubaoni.

  • Ni nini kingesaidia darasa lako kukinza majaribu? Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea mifano katika Mathayo 4:1–11 au Luka 4:1–13 ambayo kwayo uelewa wa Mwokozi wa maandiko ulimsaidia kumjibu Shetani (kwa kusema,“imeandikwa”). Wape washiriki wa darasa muda kutafuta na kushiriki maandiko ambayo yanaweza kuwaimarisha na kuwatia nguvu wakati wanahisi kujaribiwa. (Kwa mawazo, wanaweza kuangalia katika Mwongozo wa Maandiko kuhusu “Majaribu.”

Luka 4:16–30

Yesu Kristo ndiye Masiya aliyetabiriwa.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa vyema tukio hili, unaweza kuelezea kwamba vyeo Masiya na Kristo vyote vinamaanisha “mpakwa mafuta.” Wanaposoma Luka 4:18–21, waombe wafikirie kuhusu kile inamaanisha kusema kwamba Yesu ndiye Kristo, au Mpakwa Mafuta. Wanaweza pia kuona inasaidia kusoma “Mpakwa Mafuta” katika Kamusi ya Biblia. Ni kwa jinsi gani Yesu anatangaza kwamba Yeye ni Masiya hivi leo? Waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi walivyokuja kujua kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wao.

  • Kunaweza kuwa na masomo mengine yanayosaidia kujifunza kwa kutafiti kwa nini watu wa Nazareti hawakumkubali Yesu kama Masiya aliyetabiriwa. Njia moja ya kufanya hivi inaweza kuwa kutofautisha mitazamo yao na ile ya mjane wa Sarepta na Naamani katika Agano la Kale. Unaweza kuwasiliana na baadhi ya washiriki wa darasa mapema na uwaombe waje kama wamejiandaa kufanya muhtasari wa kila mojawapo ya matukio haya (ona 1 Wafalme 17:8–24; 2 Wafalme 5:1–17; Luka 4:16–30). Matukio haya yanatufundisha nini sisi kuhusu miujiza na kuitikia kwa watumishi wa Mungu? Je, washiriki wa darasa wanaona ujumbe wowote kwa waumini wa Kanisa la leo katika maneno ya Mwokozi kwa watu wa Nazareti?

Mathayo 1:16–22; Luka 5:1–11

Sharti la kumfuata Kristo linamaanisha kukubali mapenzi Yake na kuacha ya kwetu.

  • Wakati mwingine mwelekeo anaotupa Bwana hauna maana hapo mwanzo. Washiriki wa darasa wanaweza kupekua Luka 5:1–11, wakitafuta kile Mwokozi alichomwuliza Petro na kwa nini Petro angeweza kuwa na shaka na maelekezo Yake. Ni kwa jinsi gani uzoefu huu waweza kuwa uliathiri mtazamo wa Petro kuhusu Mwokozi na yeye mwenyewe? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki uzoefu ambao walionyesha imani yao katika mwongozo mtakatifu, licha ya kutokuwa na uelewa kamili. Nini yalikuwa matokeo wakati walipotumia imani yao?

    Picha
    Yesu akiwaita Petro na Andrea karibu na bahari

    “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19).

  • Jinsi tu vile wavuvi “waliacha vyote” kumfuata Yesu Kristo(Luke 5–11). Mathayo 4:18–22 inaonyesha nini kuhusu mtazamo na imani ya Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana? Inaweza kuwa msaada kuleta wavu wa kuvulia samaki darasani na uwaalike washiriki wa darasa kuandika vitu walivyotayari kuviacha au tayari wameviacha na kumfuata Kristo na uviweke kwenye wavu. Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kushiriki jinsi maisha yao yalivyobadilika wakati wamechagua kuacha vyote na kumfuata Mwokozi.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Yohana 2–4 wakati wa wiki ijayo, unaweza kuwaomba watafakari kile inamaanisha “kuzaliwa mara ya pili.” Waambie kwamba somo la wiki ijayo litawasaidia kujibu swali hili.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 4; Luka 4–5

Yesu ndiye Masiya

“Yesu Anatangaza Yeye ndiye Masiya” (video, LDS.org)

Aina za majaribu.

Baada ya kuzungumzia aina za majaribu ambayo Mwokozi alipambana nayo nyikani, Rais David O. McKay alifundisha:

“Kila jaribu linalokuja kwako na mimi linakuja katika mojawapo ya sura tatu:

“(1) Jaribu la hamu au shauku;

“(2) Kuruhusu usodai, mtindo wa kisasa, au majivuno;

“(3)Tamaa za utajiri wa kilimwengu au nguvu na mamlaka juu ya ardhi au mali za watu za kidunia” (Teachings of Presidents of the Church: David O. McKay [2003] 82).

Kuzungumzia uzoefu wa Yesu katika Mathayo 4, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mkate.’ …

“Jaribu sio katika kula. … Jaribu, angalau sehemu ningependa kuzingatia, ni kufanya kwa njia hii, kupata mkate wake—kutosheka kwake kimwili, tulizo kwa tamaa yake ya kimwili—njia rahisi, kwa matumizi mabaya ya nguvu na bila kuwa tayari kungoja muda sahihi na njia sahihi. 

“Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini, kutoka juu ya kinara cha hekalu hili …

“Jaribu hapa ni gumu hata kuelezea kuliko la kwanza. Ni jaribu la kiroho, la njaa binafsi, ya kweli zaidi kuliko hamu ya mkate. Mungu angemwokoa? … Kwa nini kutopata uthibitisho wa kiroho, kupata mkutano aminifu, na kumjibu huyu shetani mdogo anayepiga kelele—yote kwa ombi moja kwa nguvu za Mungu? …

“Lakini Yesu anakataa jaribu la pepo. Kanusho na zuio pia ni sehemu ya maandalizi matakatifu. … Hata Mwana wa Mungu lazima asubiri. Mkombozi ambaye kamwe asingeweza kuwapa wengine rehema duni haingewezekana kuomba yoyote mwenyewe. …

“… ‘Haya yote nitakupa, ukianguka na kunisujudia.’

“Shetani … [anauliza],’Taja bei yako? Mkate rahisi unaukataa. Tamthilia duni ya kimasiya unapinga, lakini hakuna binadamu anayeweza kupinga utajiri wa ulimwengu huu. Taja bei yako.’ Shetani anaendelea chini ya makala yake kwanza ya kutokuwa na imani—imani ya dhahiri kwamba unaweza kununua chochote katika ulimwengu huu kwa pesa.

“Yesu siku moja atatawala ulimwengu. Atatawala kila himaya ya mfalme na nguvu ndani yake. Atakuwa Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana . Lakini sio kwa njia hii”(“The Inconvenient Messiah,” Ensign Feb, 1984, 68–71).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Washukuru wanafunzi wako. “Usije ukazingatia somo zaidi kiasi cha kusahau kuwashukuru wanafunzi kwa michango yao. Wanahitaji kujua ya kwamba unathamini utayari wao wa kushiriki umaizi na shuhuda zao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33).

Chapisha