Njoo, Unifuate
Januari 28–Februari 3. Mathayo 3; Marko1; Luka 3: ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’


“Januari 28–Februari 3. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3; ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Januari 28–Februari 3. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Yohana Mbatizaji akimbatiza Yesu

Dirisha la kioo kilichotiwa rangi za kuona katika Hekalu la Nauvoo Illinois, na Tom Holdman

Januari 28–Februari 3

Mathayo 3; Marko 1:; Luka 3

“Itengenezeni Njia ya Bwana”

Unaposoma na kutafakari Mathayo 3; Marko 1; na Luka 3, andika misukumo unayopokea. Hii itamwalika Roho katika maandalizi yako. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuwapa mwongozo watu katika darasa lako kuelewa na kutumia mafundisho katika maandiko haya.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki jinsi kujifunza kutoka kwenye Agano Jipya kunabariki maisha yao, unaweza kuandika swali lifuatalo ubaoni: Ni kitu gani ulifanya kwa sababu ya kile ulichokisoma katika Agano Jipya wiki hii?

Picha
ikoni ya kufundisha.

Fundisha Mafundisho

Mathayo 3:1–12; Luka 3: 2–18

Wafuasi wanajiandaa pamoja na wengine kumpokea Yesu Kristo.

  • Tunajiandaa vipi kwa ziara ya mgeni mashuhuri? Swali kama hili linaweza kukusaidia kuwasilisha majadiliano kuhusu jinsi Yohana Mbatizaji alivyowaandaa watu kumpokea Yesu Kristo. Kisha unaweza kugawa darasa katika makundi matatu kusoma Mathayo 3:1–6; Mathayo 3:7–12; na Luka 3:10–15, kutafuta jinsi Yohana Mbatizaji alivyoweza kuwaandaa watu kumpokea Yesu Kristo katika maisha yao. Acha kila kikundi kuchukua zamu kushiriki kile walichopata.

  • Kama vile Yohana Mbatizaji alivyofanya, manabii wanaoishi wanatusaidia kumpokea Mwokozi katika maisha yetu. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufanya muunganisho kati ya manabii wa sasa na Yohana Mbatizaji, unaweza kurejea mafundisho ya Yohana Mbatizaji katika Mathayo 3:1–12 na Luka 3:2–18 na ushauri kadha kutoka kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni. Ni kwa jinsi gani kutii ushauri huu wa kinabii kunatusaidia kujiandaa kumpokea Mwokozi?

  • Tafsiri ya Joseph Smith, Luka 3:2–11 (katika kiambatisho cha Biblia) kinatoa umaizi katika huduma ya Yesu Kristo zaidi ya kile kinachopatikana katika Luka 3:4–6. Washiriki wa darasa wanajifunza nini kutoka aya hizi kuhusu Mwokozi na haja yetu ya kutubu?

    Picha
    Yohana Mbatizaji akihubiri

    Yohana Mbatizaji Akihubiri Nyikani, na Robert T. Barret

Luka 3:3–14

Tunahitaji kuleta kwake “matunda yapatanayo na toba.”

  • Katika Luka 3:8, Yohana Mbatizaji aliwafundisha watu kwamba kabla hawajabatizwa, walihitaji kuonyesha “matunda,” au ushahidi, wa toba yao. Unawezaje kuwasidia washiriki wa darasa kutambua ushahidi wa toba yao? Unaweza kuwauliza wapekue Luka 3:8–14 na kutafuta kile Yohana alifikiria kuwa “matunda” ya toba. Wanaweza pia kurejea Moroni 6:1–3 na Mafundisho na Maagano 20:37. Unaweza kuchora mti wa matunda ubaoni na waache washiriki wa darasa waweke tunda kitambulisho kwenye mti pamoja na “matunda” ya toba wanayoyapata. Huu unaweza pia kuwa muda mzuri wa kuzungumza kuhusu kile inamaanisha kutubu kikweli. Onyesha kwamba njia mojawapo tunayoweza “kunyoosha mapito yake (Luka 3:4) ni kupitia kutubu vikwazo vyovyote ambavyo vingeweza kumzuia Roho asitufikiye.

  • Kuimba wimbo “More Holiness Give Me,” Nyimbo, no. 131 unaweza kuhimiza majadiliano kuhusu jinsi toba inavyoweza kutusaidia kuwa zaidi kama Mwokozi. Kwa video ya muziki ya wimbo huu, ona mormontabernaclechoir.org.

Mathayo 3:13–17

Tunamfuata Yesu Kristo wakati tunapobatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu,

  • Kurejea hadithi ya ubatizo wa Yesu Kristo, jaribu wazo hili: waulize washiriki wa darasa jinsi watakavyotumia Mathayo 3:13–17 kumfundisha mtu fulani, kama vile mtoto au mtu mwingine wa imani ingine, kuhusu ubatizo. (Wanaweza pia kutumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.) Ni sifa gani muhimu za ubatizo watakazotilia mkazo? Wanaweza kufanya mazoezi ya mawazo yao kwa kufundishana wao kwa wao.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukumbuka ubatizo wao wenyewe na kutafakari juu ya umuhimu wa kuishi maagano yao ya ubatizo, unaweza kuwaalika wasome Mathayo 3:13–17 na kauli ya Mzee Robert D. Hales katika “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kushiriki hisia zao kuhusu ubatizo wao wenyewe na maagano yao ya ubatizo. Wanaweza pia kuimba “Come, Follow Me,” Wimbo, no 116

  • Yohana Mbatizaji alifundisha kwamba Mwokozi angebatiza “kwa Roho Mtakatifu, na kwa moto” (Mathayo 3:11). Ubatizo wa moto unatokea wakati tunapothibitishwa na kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa nini lazima tuwe na kipawa cha Roho Mtakatifu kuendelea katika ufalme wa Mungu? Ni athari gani ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu unayo juu yetu? Ona Alma 5:14). Video “Baptism of the Holy Ghost”(LDS.org) ingeweza kusaidia kwenye majadiliano haya.

  • Hapa kuna shughuli ambayo itawasaidia washiriki wa darasa kujadiliana zaidi mafundisho ya ubatizo. Andika maswali yafuatayo kwenye ubao na marejeo ya maandiko kwenye vipande vya karatasi. Waalike washiriki wa darasa kuchagua vipande vya karatasi na kisha wasome kila andiko kama darasa. Jadili swali lipi limejibiwa vizuri na kila andiko. Kuna maandiko mengine au umaizi ambao ungesaidia kujibu maswali haya?

    • Maandiko yanafundisha nini kuhusu umuhimu wa ubatizo? (3 Nefi 11:38)

    • Ubatizo kwa kuzamishwa unaashiria nini? (Warumi 6:3–5.)

    • Jinsi gani maagano yangu ya ubatizo yatabadili namna ninavyoishi? (Mosia 18:8–10)

    • Kwa nini hatuwabatizi watoto wachanga? (Moroni 8:8–12)

    • Kwa nini ni muhimu kwamba ubatizo ufanye na mtu mwenye mamlaka, sio tu dhamira ya kweli? Waebrania 5:4

    • Kama tayari nimebatizwa katika kanisa lingine, kwa nini nahitaji kubatizwa tena? (M&M 22:1–4)

    • Kwa nini lazima ubatizo ufuatwe na kupokea karama za Roho Mtakatifu? (Yohana 3:5)

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza Mathayo 4 na Luka 4–5 nyumbani, waalike wafikirie juu ya majaribu wanayokabiliana nayo, na waambie kwamba sura hizi zitawafundisha kile Mwokozi alifanya alipokabiliana na majaribu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

Maana ya maagano ya ubatizo wetu.

Mzee Robert  D. Hales alifundisha:

“Wakati tunapoelewa agano la ubatizo wetu na kipawa cha Roho Mtakatifu, itabadili maisha yetu na itaanzisha wajibu wetu kamili kwa ufalme wa Mungu. … Kuingia katika ufalme wa Mungu ni muhimu mno kiasi kwamba Yesu alibatizwa kutuonyesha ‘unyoofu wa njia’ [2 Nefi 31:9]. …

“Tunapofuata mfano wa Yesu, sisi, vilevile, tunaonyesha kwamba tutatubu na kuwa watiifu katika kushika amri za Baba wa Mbinguni. Tunajinyenyekeza wenyewe na moyo uliyopondeka na roho iliyovunjika tunapozitambua dhambi zetu na kutafuta msamaha wa makosa yetu [ona 3 Nefi 9:20]. Tunaweka maagano kwamba tuko tayari kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo na siku zote kumkumbuka. …

“Kwa kuchagua kuwa katika ufalme wa [Mungu], tunajitenga—sio kukaa pweke—kutoka ulimwenguni. Nguo zetu zitakuwa za staha, mawazo yetu safi, lugha yetu stahifu. Filamu za sinema na runinga tunazoangalia, muziki tunaosikiliza, vitabu, majarida, na magazeti tunayosoma yatakuwa ya kuinua. Tutachagua marafiki ambao watatuhimiza katika malengo yetu ya milele, na tutawatendea wengine kwa huruma. Tutaepuka tabia mbaya ya uovu, kucheza kamari, tumbaku, pombe, na madawa ya kulevya. Shughuli zetu za Jumapili zitaakisi amri ya Mungu kuikumbuka siku ya Sabato na kuitukuza. Tutafuatia mfano wa Yesu Kristo kwa njia tunayowatendea wengine. Tutaishi kuwa tunaostahili kuingia nyumba ya Bwana” (“Agano la Ubatizo: Kuwa ndani ya Ufalme na washiriki wa Ufalme.” Ensign, Nov. 2007, 7–8)

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha mafundisho ya msingi. Hyrum Smith alifundisha, “Hubiri kanuni za kwanza za Injili—zifundishe tena na tena; utaona kwamba siku baada ya siku mawazo mapya na nuru ya ziada kuzihusu itafunuliwa kwako. Unaweza kuzikuza ili uweze kuzielewa kwa uwazi. Kisha utaweza kuzifanya zaidi kueleweka wazi kwa wale unaowafundisha” (Manuscript History of the Church, vol. E-1, p. 1994 josephsmithpapers.org).

Chapisha