Njoo, Unifuate
Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’


“Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Mahubiri ya Mlimani

Mahubiri ya Mlimani, na Jorge Cocco

Februari 18–24

Mathayo 5; Luka 6

“Heri Ninyi”

Andika misukumo ya kiroho unapojifunza Mathayo 5 na Luka 6. Ufunuo utakuja unapotafuta kukidhi mahitaji ya darasa lako. Muhtasari huu unaweza kusaidia kutoa mawazo ya ziada.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Rais Joseph Fielding Smith alisema kwamba Mahubiri ya Mlimani ni “[mahubiri] muhimu sana ambayo yaliwahi kuhubiriwa, kwa kadri tunavyojua” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith [2013], 234). Kwa nini washiriki wa darasa wanahisi kwamba hii ni kweli? Nini wanaweza kushiriki?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 5:1–12

Furaha isiyo na mwisho inakuja kutokana na kuishi njia Yesu Kristo aliyofundisha na kuishi.

  • Mahubiri ya Mlimani ya Mwokozi, ambayo yalikuwa kimsingi akiwahutubia wafuasi wake wa karibu, yanaanza na kauli zinazojulikana kama Hali za Heri, ambazo Kristo anatualika tufikiri tena inamaanisha nini kuishi maisha ya baraka—maisha ya furaha isiyo na kikomo. Kuanza majadiliano kuhusu furaha isiyo na kikomo, waombe washiriki wa darasa kushiriki nini kinawafanya wawe na furaha. Kulingana na Hali za Heri, Yesu alisema ni nini kinamfanya mtu “abarikiwe,” au milele mwenye furaha? Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Kristo ni tofauti na njia nyingine watu wanazojaribu kutafuta furaha?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa istilahi kama roho safi au wapatanishi, unaweza kuorodhesha baadhi ya istihali kutoka aya 3–12 ubaoni. Kisha waalike washiriki wa darasa wapendekeze kinyume cha kila istilahi na kile wanajifunza kuhusu kila istilahi kwa kufanya hivi. Waombe washiriki wa darasa kutafakari kile ambacho wanaweza kubadili ili kuwa aina ya mtu aliyeelezwa katika aya hizi. Ni nini 3 Nefi 12:3, 6 inaongeza kwenye uelewa wetu wa Mathayo 5:3, 6?

  • Njia ingine ya kuchunguza aya hizi ni kumwalika kila mshiriki wa darasa kujifunza maandiko ya ziada kuhusu moja ya Hali za Heri na kushiriki na darasa kile wanajifunza. Ni kwa jinsi gani mtu wanayemfahamu ni mfano kanuni hiyo?

Mahubiri ya Mlimani

Mahubiri ya Mlimani, na Frank Adams

Mathayo 5:14–16

Wafuasi wa Mwokozi wanatakiwa wawe nuru ya ulimwengu.

  • Ni kwa jinsi gani washiriki wako wa darasa wanahisi wanaposoma kauli ya Yesu kwamba wao ni “nuru ya ulimwengu”? Ina maana gani kuficha nuru yetu ”chini ya pishi,” na kwa nini tunaweza kujaribiwa kufanya hivi? Kauli ya Mzee Robert D. Hales katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuhimiza. Nani amekuwa “nuru” kwa washiriki wa darasa lako?

  • Fikiria njia ya kuonyesha mafundisho ya Kristo kwamba sisi ni nuru kwa ulimwengu. Unaweza kuonyesha picha ya jiji linalon’gaa usiku? Unaweza kuleta tochi na kuificha chini ya kikapu? Kwa nini Mwokozi anawafananisha wafuasi Wake na nuru? Tunawezaje kutumia uelewa huu kuwa nuru kwa wengine? (ona M&M 103:9–10). Washiriki wa darasa wanaweza kujadili au kuigiza njia ambazo nuru ya injili inaweza kun’gaa katika maisha yao na kubariki wengine.

  • Baadhi ya maandiko mengine yanayoweza kuongeza kwenye majadiliano yenu kuhusu nuru inajumuisha 3 Nefi 18:24; Mafundisho na Maagano 50:24; 84:44–47; 88:50, 67; na 93:36–40. Washiriki wa darasa wanaweza pia kufurahia kuimba nyimbo kuhusu nuru, kama vile “Bwana ni Nuru Yangu” na “Ongoza, Kwa huruma Nuru Nyimbo, namba 89, 97. Nini kinafanya nyimbo hizi na maandiko kuongeza kwenye uelewa wetu wa Mathayo 5:13–16?

Mathayo 5:17–48

Yesu Kristo alifundisha sheria ya juu ambayo inaweza kutuongoza kwenye ukamilifu.

  • Hali zilizoelezwa katika Mathayo 5 zilikuwa mahususi kwa siku za Mwokozi, lakini kanuni Alizofundisha ni za wakati wote. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuona matumizi kwa maisha yao, waalike wachague mojawapo ya vifungu vifutavyo na wafikirie mfano wa kisasa ambao unaonyesha kile Mwokozi alikuwa anafundisha: aya 21–24; 27–30; 33–37; 38–39; 40–42; na 43–44. Wanaweza kufanya hivi binafsi au washiriki mifano yao na darasa.

  • Vijana wanaweza kufaidi mchezo wa kufananisha ambao unawasaidia kuona kwamba mafundisho ya Mwokozi yanayopatikana katika Mathayo 5:21–48 yanachukua nafasi ya sheria ya Musa. Unaweza kuumba seti moja ya kadi na virai vinavyoanzia na “mmesikia” (kuelezea sheria ya Musa) kutoka Mathayo 5:21–44. Umba seti ingine na virai kutoka aya zinazoanza “lakini nasema” (kuelezea sheria ya juu ya Kristo). Weka seti zote mbili za kadi zikiangalia chini, na mwache mshiriki wa darasa achague moja ya kadi za “mmesikia,” ikifuatiwa na moja kutoka kwa ile seti ingine, mkitafuta mfanano. Endelea mpaka washiriki wa darasa watakapofananisha sheria za Musa na mafundisho mapya ya Kristo. Kwa kila mfanano, jadili kwa nini mafundisho ya Mwokozi yanahitajika siku hizi.

  • Unaweza kuwasaidia vipi washiriki wa darasa kuona kwamba amri ya Mwokozi kuwa “wakamilifu” inamaanisha, kama Rais Russell M. Nelson alivyoelezea, kuwa “kamilika” au “timia”? (Mathayo 5:48; “Kungoja Ukamilifu.” Ensign, Nov. 1995, 86–88). Hapa kuna wazo: kata picha ya Yesu kuwa chemsha bongo, na waalike washiriki wa darasa kuandika nyuma ya kila kipande mafundisho kutoka Mathayo 5 ambayo wanahisi kutiwa moyo kuyatumia katika maisha yao. Waache wafanye kazi pamoja kukamilisha chemsha bongo. Ni kwa jinsi gani upatanisho wa Yesu Kristo unatusaida “kukamilika” au “kutimia?” (ona Kamusi ya Biblia, ”Neema”)

  • Unaweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kuweka lengo la kufanya kazi kwa msukumo walioupata walipokuwa wanajifunza Mathayo 5. Fikiria jinsi unavyoweza kufuatilia juu ya mwaliko huu katika masomo yafuatayo.

ikoni ya kujifunzia

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwapa mwongozo washiriki wa darasa kusoma Mathayo 6–7 wakati wote wa wiki ijayo, unaweza kuwaambia kwamba Rais Harold B. Lee aliyaita Mahubiri ya Mlimani “Katiba ya maisha kamili” (Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee [2000], 200).

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 5; Luka 6

Kuwa nuru.

Mzee Robert D. Hales alifundisha: “Je, umewahi kukoma kufikiria kwamba labda wewe ndiwe nuru iliyotumwa na Baba wa Mbinguni kuongoza mwingine nyumbani salama au kuwa nguzo kutoka mbali yenye kuonyesha njia ya kurudi kwenye njia iliyosonga na nyembamba iendayo kwenye uzima wa milele? Nuru yako ni nguzo na kamwe haipaswi kukoma kuwaka au kupotosha wale wanaotafuta njia ya kwenda nyumbani” (“Ili Muweze Kuwa Watoto wa Nuru” [Brigham Young University fireside, Nov. 3,1996], 9: speech.byu.edu).

Kutafuta ukamilifu.

Rais Harold B. Lee: “Mngedhania kwamba Mwokozi alikuwa anapendekeza lengo ambalo halikuwa linawezekana kufikiwa na kwa hiyo kutudhihaki katika juhudi zetu kuishi na kufikia ukamilifu ule? Haiwezekani kwetu sisi hapa katika maisha haya kufikia hali ile ya ukamilifu ambayo Bwana alisema, lakini katika maisha haya tunajenga msingi ambao juu yake tutajenga katika milele; kwa hiyo, ni sharti tuhakikishe kwamba msingi wetu umejengwa kwenye ukweli, haki na imani” (Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee, 195).

Rais Joseph Fielding Smith alisema: “[Ukamilifu] hautakuja wote mara moja, lakini msitari juu ya mstari na kanuni juu ya kanuni, mfano juu ya mfano, na hata hivyo ilimradi tunaishi katika maisha haya ya kufa. … Lakini hapa tunajenga msingi. Hapa ndipo tunapofundishwa kweli hizi rahisi za Injili ya Yesu Kristo, katika hali hii ya majaribio, kutuandaa kwa ukamilifu huo. Ni wajibu wangu, ni wako, kuwa bora leo kuliko nilivyokuwa jana, na kwako wewe kuwa bora leo kuliko ulivyokuwa jana, na bora zaidi kesho kuliko ulivyokuwa leo” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith [2013], 234–35).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Zidisha kushiriki kwa washiriki wa darasa. Shughuli nyingi zinaweza kufanywa kama darasa, katika vikundi vidogo, katika majozi, au kama jopo la majadiliano. Tumia mbinu mbalimbali ili kuruhusu watu kushiriki wale ambao wasingeweza kwa njia yoyote kupata nafasi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33.)