“Januari 21–27. Yohana 1: Tumemwona Masiya,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)
“Januari 21–27. Yohana 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Januari 21–27
Yohana 1
Tumemwona Masiya
Kabla hujasoma nyenzo yoyote ya ziada, soma na utafakari Yohana 1, na uandike misukumo ambayo umepokea. Hii itamwalika Roho katika maandalizi yako. Njoo Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuwapa mwongozo watu katika darasa lako kuelewa na kutumia mafundisho katika sura hii.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza, unaweza kuwaomba waandike maswali, maoni, au umaizi kutoka kwenye kusoma kwao katika vipande vya karatasi na uviweke kwenye chombo. Chukua vipande kutoka kwenye chombo ili kujadili kama darasa.
Fundisha Mafundisho
Yesu Kristo alikuwa “hapo mwanzo pamoja na Mungu.”
-
Yohana alianza ushuhuda wake wa Kristo kwa kushuhudia wajibu wa Mwokozi kabla hajazaliwa. Yohana alifundisha nini kuhusu Yesu kabla ya hajazaliwa duniani? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu wajibu wa Kristo kabla ya kuzaliwa duniani? Inaweza kusaidia kuandika maswali haya ubaoni na kuwaomba washiriki wa darasa kutafuta majibu katika Yohana 1:1–5 (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana 1:1–5 [katika kiambatisho cha Biblia]) na katika kauli ya Mzee James E. Talmage katika “Nyenzo za Ziada.” Marejeo gani mengine ya maandiko washiriki wa darasa wanaweza kushiriki ambayo yanafundisha zaidi kuhusu Kristo kabla hajazaliwa duniani? (Kwa Mifano, ona “Jesus Christ, Antemortal Existence of” katika Topical guide.) Kama darasa, mnaweza pia kurejea “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Manabii” (Ensign au Liahona, Apr. 2000, 2).
-
Kama ungependa kutumia aya hizi kuzungumza kuhusu uumbaji wa Bwana, unaweza kusoma Yohana 1:3 na uonyeshe picha ambazo zinaeleza uzuri wa dunia. Unaweza kuonyesha video “Nyumbani Kwetu” (lds.org/topics/environmental-stewardship-and-conservation). Waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi uumbaji wa Mwokozi unawasaidia kuhisi upendo Wake.
Yesu Kristo ndiye Nuru.
-
Nuru ya asili inaweza kutusaidia kuelewa uashiriaji wa nuru ya kiroho. Unawezaje kuonyesha uashiriaji huu kwa darasa lako? Unaweza kuzima mwanga katika chumba na uwashe tochi kuonyesha tofauti kati ya nuru na giza. Kisha waombe washiriki wa darasa kupata kila mfano wa neno nuru katika Yohana 1:1–14, na waalike washiriki jinsi Mwokozi na injili Yake hutoa nuru ya kiroho katika maisha yao. Ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa walipata uzoefu wa nuru Yake? Kama sehemu ya majadiliano haya, unaweza kutaka wasome zaidi kuhusu Nuru ya Kristo katika Mafundisho na Maagano 84:45–46; 88:11–13, au unaweza kuwarejesha kwenye “Nuru ya Kristo” katika Kamusi ya Biblia. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa ulimwengu?
-
Kwa sababu Yohana 1:1–14 imeandikwa katika lugha ya uashiriaji, inaweza kuwa vigumu kuelewa. Njia mojawapo ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ushuhuda wa Yohana inaweza kuwa kuwaalika watengeneze orodha ya maneno yanayorudiwarudiwa na virai katika aya hizi na washiriki kile kila mojawapo kinatufundisha kuhusu Mwokozi.
-
Hii ni njia ya kushirikisha washiriki wa darasa katika aya hizi: Onyesha picha kadha (pamoja na moja kutoka kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) hiyo itaonyesha mwelekeo na huduma tukufu ya Yesu Kristo. Waalike washiriki wa darasa kupekua Yohana 1:1–14, wakitafuta maneno au virai ambavyo vingeweza kutumika kama majina ya picha.
Tunaweza kupata ushahidi wetu wenyewe wa Mwokozi na kisha kuwaalika wengine “njoo uone.”
-
Katika Yohana 1, mwaliko wa “njoo uone” unatokea mara mbili (ona aya 39, 46). Tunaweza tusiwe na bahati ya kumwona Mwokozi kimwili kwa njia ambayo Andrea na Nathanaeli walivyofanya, lakini tunaweza kujibu mwaliko huo huo. Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kile wanachofikiri inamaanisha “njoo uone” katika siku zetu na kushiriki uzoefu wao wenyewe wa kupata ushuhuda wa Mwokozi.
-
Kutanguliza majadiliano kuhusu aya hizi, fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki hadithi kuhusu jinsi walivyotanguliza injili ya Yesu Kristo kwa wengine. Ni nani waliyemwalika “njoo uone”? Tunajifunza nini kutoka kwa Andrea na Filipo kuhusu kushiriki ushuhuda wetu wa Kristo?
-
Wakati mwingine watu hawashiriki injili kwa sababu wanaona kwamba kufanya hivyo kunaogofya au ni changamani. Matukio katika Yohana 1:35–51 yanaonyesha kwamba kushiriki injili kunaweza kuwa rahisi na kawaida. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kuzisoma aya hizi na kujadili jinsi wanavyoweza kuzitumia kumsaidia mtu mwingine ambaye ni mwenye wasiwasi kuhusu kushiriki injili. Wanaweza kutumia dondoo ya Mzee Neil L. Andersen katika Nyenzo za Ziada” kwa mawazo. (Ona pia video “Vitu vizuri vya kushiriki” kwenye LDS.org.)
Himiza Kujifunza Nyumbani
Kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza Mathayo 3, Marko 1, na Luka 3, unaweza kuwaomba wamfikirie mtu fulani wangependa kumsaidia kumpeleka kwa Kristo. Waambie kwamba katika sura hizi watasoma kuhusu nabii ambaye huduma yake ilikuwa ni kuwaandaa watu kumpokea Mwokozi.
Nyenzo za Ziada
Yesu Kristo alikuwa pamoja na Baba hapo mwanzo.
Mzee James E. Talmage alifundisha: “Kwamba Neno ni Yesu Kristo, Aliyekuwa na Baba [hapo] mwanzo na ambaye alikuwa mwenyewe amevikwa na uwezo na daraja la Uungu, na kwamba alikuja ulimwenguni na kuishi miongoni mwa watu, kwa hakika wamethibitisha. Kauli hizi zimethibitishwa kupitia kwa ufunuo aliopewa Musa, ambapo aliruhusiwa kuona wingi wa uumbaji wa Mungu, na kusikia sauti ya Baba kuhusiana na vitu ambavyo vimekwisha umbwa: ‘Na kwa neno la uweza wangu, nimeviumba, ambaye ndiye Mwanangu wa pekee, aliyejaa neema na kweli’ [Musa 1:32, 33]” (Yesu Kristo, 3rd ed. [1916], 10).
Tunaweza kuwaalika wengine “njoo uone.”
Mzee Neil L. Andersen alifundisha:
“Mwokozi alitufundisha jinsi ya kushiriki injili. Ninapenda hadithi ya Andrea, ambaye aliuliza, ‘Bwana, unakaa wapi?’ [Yohana 1:38.] Yesu angeweza kujibu pamoja na sehemu ambayo alipoishi. Lakini badala yake alimwambia Andrea, ‘njoo uone ‘[Yohana 1:39]. Ninapenda kufikiri kwamba Mwokozi alikuwa anasema, ‘Njoo uone sio tu wapi ninapokaa bali jinsi ninavyoishi. Njoo uone mimi ni nani. Njoo uhisi Roho.’ Hatujui kila kitu kuhusu siku ile, lakini tunajua kwamba wakati Andrea alipomwona kaka yake Simoni, alitangaza, “Tumemwona … Kristo’ [Yohana 1:41].
“Kwa wale wanaoonyesha kuvutiwa na mazungumzo yetu, tunaweza kufuata mfano wa Mwokozi kwa kuwaalika “njoo uone.’ Baadhi watakubali mwaliko wetu, na wengine hawatakubali. Sisi sote tunamjua mtu fulani ambaye amealikwa mara kadha kabla ya kukubali mwaliko wa ‘njoo uone.’ Acha pia tufikiri kuhusu wale ambao mwanzo walikuwa pamoja nasi lakini ambao sasa tunawaona mara chache, kuwaalika warudi na waone tena. …
“Kwa wale wanaotumia mtandao na simu za mkononi, kuna njia mpya za kuwaalika wengine ‘njoo uone.’ Acha tufanye kushiriki imani yetu katika mtandao kuwe zaidi sehemu ya maisha yetu ya kila siku” (Ni Muujiza.” Ensign au Liahona, Mei 2013, 79).
Muziki unaweza kutufundisha sisi juu ya Kristo.
Fikiria kutumia wimbo ”For the Beauty of the Earth.” Nyimbo, no. 92, unapojadili wajibu wa Mwokozi kama Muumbaji (ona Yohana 1:3). Unaweza pia kutumia video ya “For the Beauty of the Earth” kwenye mormontabernaclechoir.org.