Njoo, Unifuate
Januari 14–20. Luka 2: Mathayo 2: Tumekuja Kumwabudu


“Januari 14–20. Luka 2; Mathayo 2: Tumekuja Kumwabudu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Januari 14–20. Mathayo 2; Luka 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Mamajusi wakisafiri juu ya ngamia

Acha Tumwabudu, na Dana Mario Wood

Januari 14–20

Luka 2; Mathayo 2

Tumekuja Kumwabudu

Kabla hujasoma mawazo katika muhtasari huu, jifunze Luka 2 na Mathayo 2, na unandike misukumo yako ya kiroho. Hii itakusaidia kupokea ufunuo juu ya jinsi bora ya kukidhi mahitaji ya darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Unaweza kuwahimiza vipi washiriki wa darasa lako kushiriki umaizi na uzoefu waliopata walipokuwa wanajifunza maandiko haya binafsi na pamoja na familia zao? Ingawa wanaelekea kuwa wazoefu na tukio la kuzaliwa kwa Mwokozi, wanaweza daima kupata umaizi mpya wa kiroho. Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kushiriki ujumbe walioupata katika Luka 2 au Mathayo 2 ambao uliwavutia katika njia mpya.

Picha
ikoni ya kufundisha.

Fundisha Mafundisho

Luka 2:1–38; Mathayo 2:1–12

Kuna mashahidi wengi wa kuzaliwa kwa Kristo.

  • Matukio ya moja kwa moja ya waabuduo katika Luka 2 na Mathayo 2 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kutafakari njia wanazoonyesha upendo wao kwa Mwokozi. Hakiki chati katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Baadhi ya watu katika darasa lako wanaweza kuwa na umaizi wa kushiriki kutoka katika shughuli hii, au mnaweza kufanya shughuli kama darasa. Kwa nini ni muhimu kwamba mashahidi hawa wa Kristo walikuja kutoka sehemu mbalimbali? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mifano yao?

  • Kabla mashahidi hawa hawajamwabudu mtoto Kristo, walimtafuta. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka mfano wao, unaweza kuandika ubaoni vichwa vya habari vifuatavyo: Wachungaji, Ana, Simioni na Mamajusi. Kisha waalike washiriki wa darasa kupekua Luka 2 na Mathayo 2 na waandike ubaoni kile watu hawa walifanya kumtafuta Mwokozi. Ni nini matukio haya yanapendekeza kuhusu baadhi ya njia tunazoweza kumtafuta Kristo?

    Picha
    mchungaji na kondoo

    Wachungaji walikuwa baadhi ya mashahidi wa kwanza wa kuzaliwa kwa Mwokozi.

  • Somo la vielelezo lingeweza kuwapa mwongozo washiriki wa darasa kuweka nafasi katika maisha yao kwa Mwokozi? Fikiria wazo lifuatalo: Lete gudulia darasani na, baada ya kuhakiki pamoja Luka 2:7, waombe washiriki wa darasa wajaze gudulia na vitu tofauti ambavyo vinawakilisha njia tunazotumia muda wetu. Wakati gudulia litakapojaa, alika mtu yoyote kujaribu kuitia ndani picha ya Mwokozi. Mfano huu unapendekeza nini kuhusu kutengeneza nafasi kwa ajili ya Kristo katika maisha yetu? Tunaweza kufanya nini tofauti kutengeneza nafasi kwa ajili Yake? Kauli ya Rais Thomas S. Monson katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia kujibu swali hili.

Mathayo 2:13–23

Wazazi wanaweza kupokea ufunuo ili kulinda familia zao.

  • Somo moja kutoka ukimbizi wa Yusufu na Mariamu kwenda Misri ni kwamba Bwana anaweza kutoa ufunuo kuwasaidia wazazi kulinda familia zao kutoka kwenye hatari. Ili kuchochea majadiliano kwa wakati huu, fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha ubaoni baadhi ya hatari familia zinapambana nazo leo. Tunajifunza nini kutoka Mathayo 2:13–23 kuhusu jinsi ya kulinda familia zetu na sisi wenyewe kutokana na hatari hizi? Ni kwa jinsi gani ufunuo binafsi umetusaidia kulinda familia zetu au wapendwa wetu wengine kutokana na hatari? Ni ushauri gani manabii na mitume wametoa kutusaidia kulinda familia zetu?

  • Kama sehemu ya majadiliano haya, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kuimba pamoja “Nyumbani Kunaweza kuwa Mbinguni hapa Duniani.” Nyimbo za dini nambari. 298, au wimbo mwingine kuhusu familia. Wimbo huu unafundisha nini kuhusu kile wazazi wanachoweza kufanya ili kuishi maisha yenye kustahili ufunuo wa kuongoza familia zao?

Luka 2:40–52

Hata akiwa kijana, Yesu alilenga kufanya mapenzi ya Baba Yake.

  • Hadithi ya Yesu akifundisha katika hekalu wakati alipokuwa umri wa miaka 12 tu inaweza kuwa hasa yenye nguvu mno kwa vijana ambao wanashangaa kuhusu mchango wanaoweza kutoa kwenye kazi ya Mungu. Unaweza kuligawa darasa kwenye majozi kusoma Luka 2:40–52 pamoja (ona umaizi kutoka kwenye Tafsiri ya Joseph Smith unaopatikana katika Luka 2:46, tanbihi c). Kila jozi inaweza kuchukua dakika chache kushiriki pamoja kile kinawavutia kuhusu matukio haya. Ni nafasi gani tulizonazo za kushiriki kile tunachojua kuhusu injili? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki?

  • Kama unawafundisha watu wazima, tukio hili linaweza kuwa nafasi ya kujadili jinsi ya kuwasaidia vijana kutimiza uwezo wao. Mtu mwingine anaweza kufanya muhtasari wa tukio katika Luka 2:40–52, na darasa laweza kujadili jinsi matukio haya yanavyoshawishi njia wanayowaona vijana wa Kanisa. Ni nafasi zipi tunazoweza kuwapa vijana kushiriki katika kufanya shughuli [za] Baba kama alivyofanya Yesu? (Luka 2:49). Ni wakati gani tumeshangazwa na umaizi wa kiroho ulioshirikiwa na kijana au mtoto? Maneno haya kutoka kwa Rais Henry B. Eyring yanaweza kuongezwa kwenye majadiliano haya: “Wakati mwenye ukuhani wa Haruni anapozungumza, … siku zote nategemea kwamba nitasikia neno la Mungu. Ni mara chache sana navunjwa moyo na daima nashangazwa,” (“Kwamba Aweze Kuwa na Nguvu Ensign au Liahona, Nov. 2016, 77).

  • Ni nini Luka 2:40–52 inatufundisha kuhusu vile Yesu alikuwa kama kijana? Mwelekeo wa ukuaji binafsi uliopendekezwa katika Luka 2:52 unaweza kuchochea majadiliano juu ya nini tunachofanya kuwa zaidi kama Kristo. Unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa watafakari jinsi wanavyoongezeka katika hekima (kiakili), kimo (kimaumbile), kupendwa na Mungu (kiroho), na kupendwa na wengine (kijamii). Wanaweza hata kuweka malengo katika moja au zaidi ya maeneo haya.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujiandaa kujadili Yohana 1 wiki ijayo, waombe waandike muhtasari wa kila sehemu katika sura ambako mtu fulani anatoa ushuhuda wa Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Luka 2; Mathayo 2

Mbinu ya kumtafuta Kristo.

Rais Thomas S. Monson alifundisha:

“Mbinu ya kumpata Yesu daima imekuwa na daima itakuwa ile ile—yenye ari na maombi ya kweli ya moyo mnyenyekevu na halisi. …

“Kabla hatujafanya kazi ya upekuzi binafsi wa Yesu kwa ufanisi, ni lazima kwanza kuandaa muda kwa ajili Yake katika maisha yetu na nafasi kwa ajili Yake katika mioyo yetu. Katika siku hizi za shughuli nyingi kuna wengi ambao wana muda na kucheza gofu, muda wa kwenda madukani, muda wa kufanya kazi, muda wa kucheza—lakini hawana muda kwa Kristo.

“Nyumba za kupendeza zimetapakaa nchini na zina vyumba kwa ajili ya kula, vyumba vya kulala, vyumba vya michezo, vyumba vya kushonea, vyumba vya runinga, lakini hamna chumba kwa ajili ya Kristo.

Je, tunapata maumivu makali ya dhamira wakati tunapokumbuka maneno yake mwenyewe: ‘Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa mtu hana popote pa kulaza kichwa chake.’ (Mathayo 8:20.) Au tunapata msisimko pamoja na aibu wakati tunapokumbuka, ‘Akamzaa mwanawe kifungua mimba, na akamvika nguo za kitoto, na akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe; kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.’ (Luka 2:7.) Hakuna chumba. Hakuna chumba. Hakuna chumba. Daima imekuwa hivyo.

“Tunapoanza utafutaji wetu binafsi wa Kristo, tukisaidiwa na kuongozwa na kanuni ya maombi, ni muhimu kwamba tuwe na fikira safi ya yule ambaye tunamtafuta. Wachungaji wa zamani walimtafuta mtoto Yesu. Bali tunamtafuta Yesu Kristo, Kaka yetu Mkubwa, Mtetezi wetu kwa Baba, Mkombozi wetu, Mtunzi wa wokovu wetu; yeye aliyekuwa hapo mwanzo pamoja na Baba; yeye ambaye alijichukulia mwenyewe dhambi za ulimwengu na kwa radhi yake akafa ili tuweze kuishi milele. Huyu ndiye Yesu ambaye tunamtafuta” (“Uchunguzi wa Yesu.)” Ensign, Dec.1990, 4–5).

Mchoro wa kuzaliwa kwa Kristo.

Fikiria jinsi mchoro unavyoweza kuboresha majadiliano yenu kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. (Kwa mifano, ona Kitabu cha Sanaa ya Injili au history.lds.org/exhibit/birth-of-christ.)

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajumuishe wanafunzi ambao hawakujifunza maandiko nyumbani. Hata kama baadhi ya washiriki wa darasa hawakuweza kusoma Luka 2 na Mathayo 2 kabla ya darasa, wanaweza bado kushiriki umaizi wa maana mnapojifunza pamoja katika darasa. Hakikisha kwamba washiriki wote wa darasa wana nafasi kushiriki na kuchangia kwenye majadiliano.

Chapisha