Njoo, Unifuate
Januari 21–27. Yohana 1: Tumemwona Masiya


“January 21–27. Yohana 1: Tumemwona Masihi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“January 21–27. Yohana 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
mwanamke akishiriki injili kwenye kituo cha gari moshi.

Januari 21–27

Yohana 1

Tumemwona Masiya

Unaposoma na kutafakari Yohana 1, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Ni ujumbe gani unapata ambao utakuwa na thamani kubwa kwako na kwa familia yako? Nini ungeweza kushiriki katika madarasa yako ya Kanisani?

Andika Misukumo Yako

Umewahi kujiuliza kama ungemtambua Yesu wa Nazareti kama Mwana wa Mungu kama ungekuwa hai wakati wa huduma Yake duniani? Kwa miaka, Waisraeli waaminifu, akiwemo Andrea, Petro, Filipo, na Nathanaeli, walisubiri na kuomba kwa ujio wa Masiya aliyetabiriwa. Walipokutana naye, walijuaje kwamba Alikuwa Ndiye waliyekuwa wakimtafuta? Ni kwa njia hiyo wote tunakuja kumjua Mwokozi—kwa kukubali mwaliko wa “njoni nanyi mtaona” wenyewe (Yohana 1:39). Tunasoma kuhusu Yeye katika maandiko. Tunasikia mafundisho Yake. Tunafuata njia Zake za kuishi. Tunahisi Roho Wake. Njiani, tunagundua, kama Nathanaeli alivyogundua, kwamba Mwokozi anatujua na anatupenda na anataka kutuandaa kupokea “mambo makubwa” (Yohana 1:50).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Injili ya Yohana

Yohana alikuwa nani?

Yohana alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji na baadaye alikuwa mmoja wa wafuasi wa mwanzo wa Yesu Kristo na mmoja wa Mitume Wake Kumi na wawili. Aliandika Injili ya Yohana, nyaraka kadhaa, na kitabu cha Ufunuo. Katika injili yake, alijitambulisha kama mwanafunzi “ambaye Yesu alimpenda” na “mwanafunzi wengine” (Yohana 13:23; 20:3). Ari ya Yohana ya kutangaza injili ilikuwa kubwa kwamba aliomba kubaki duniani mpaka Ujio wa Pili wa Mwokozi ili azilete nafsi kwa Kristo (ona M&M 7:1–6).

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Yohana” na “Yohana, Injili ya.”

Yohana 1:1–5

Yesu Kristo “mwanzo alikuwako kwa Mungu.”

Yohana alianza injili yake kwa kuelezea kazi ambayo Kristo alifanya kabla Hajazaliwa: “Hapo mwanzo … Neno [Yesu Kristo] alikuwako kwa Mungu.” Unajifunza nini kutoka mistari 1–5 kuhusu Mwokozi na kazi Yake? Unaweza kupata maelezo yenye msaada katika Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana 1:1–5 (katika kiambatisho cha Biblia). Unapoanza kujifunza kwako kuhusu maisha ya Mwokozi, kwa nini ni muhimu kujua kuhusu kazi Yake kabla ya kuzaliwa?

Ona pia “Yesu Kristo Alichaguliwa kama Mwokozi,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Yohana 1:1–18

Wanafunzi wa Yesu Kristo wanatoa ushuhuda kumhusu Yeye.

Yohana alipata msukumo wa kumtafuta Mwokozi kwa sababu ya ushuhuda wa Yohana Mbatizaji, ambaye alitangaza kwamba yeye “alitumwa kutoa ushuhuda wa… Nuru ya kweli” (Yohana 1:8–9, 15–18). Yohana mwenyewe alitoa ushahidi wa nguvu wa maisha na huduma ya Mwokozi.

Inaweza kuwa ya kuvutia kuweka orodha ya kweli ambazo Yohana alizijumuisha katika ushuhuda wake wa ufunguzi wa Kristo (mistari 1–18; ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, John 1:1–19 [katika kiambatisho cha Biblia]). Kwa nini unafikiri kwamba Yohana alianza Injili yake kwa kweli hizi? Fikiria kuandika ushahidi wako wa Yesu Kristo—nini ungetaka kushiriki? Ni uzoefu gani umekusaidia kumjua na kumfuata Mwokozi? Ni nani anaweza kubarikiwa kwa kusikia ushuhuda wako?

Yohana 1:12

Inamaanisha nini “kuwa wana wa Mungu”?

Japo wote ni wana na mabinti wa kiroho wa Mungu, tunapotenda dhambi tunakuwa tumefarakana au kutenganishwa Naye. Yesu Kristo hutupatia njia ya kurudi. Kupitia upatanisho Wake na utiifu wetu kwa maagano ya injili, Yeye “[hutupa sisi] nguvu ya kuwa wana [na mabinti]” wa Mungu kwa mara nyingine. Tunazaliwa mara ya pili na kupatanishwa kwa Baba yetu, wastahiki wa urithi Wake wa milele na warithi wa vyote Alivyonavyo (ona Warumi 8:14–18; Yakobo 4:11).

Yohana 1:18

Kuna mtu amemwona Mungu?

Agano la Kale hutoa kumbukumbu ya mifano ya watu ambao walimwona Mungu (ona Mwanzo 32:30; Kutoka 33:11; Isaya 6:5). Sasa kwa nini Yohana Mbatizaji angesema kwamba “hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote”? Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari huu (ona Yohana 1:18, tanbihi c) hutoa ufafanuzi kwamba Mungu Baba huwatokea watu, na Anapowatokea, Hushuhudia juu ya Mwanaye. Kwa mfano, Alipomtokea Joseph Smith katika Msitu Mtakatifu, Alimwambia Joseph, “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!” (Historia ya—Joseph Smith1:17; ona pia M&M 76:23). Kuna kumbukumbu kadhaa zingine za matukio ambapo watu walimwona Mungu Baba katika ono (ona Matendo 7:55–56; Ufunuo 4:2; 1 Nefi 1:8; M&M 137:1–3) au kusikia sauti Yake ikishuhudia juu ya Mwanaye (ona Mathayo 3:17; 17:5; 3 Nefi 11:6–7).

Yohana 1:19–23

Elia ni nani, na nani ndiye “nabii yule”?

Viongozi wa kiyahudi walijiuliza kama Yohana Mbatizaji alikuwa akitimiza unabii wa kale kuhusu manabii ambao siku moja wangekuja kati ya watu. Walimuuliza kama alikuwa Elia, ambalo ni neno la Kigiriki la Eliya, jina la nabii ambaye alitabiriwa kurejesha mambo yote (ona Malaki 4:5–6). Waliuliza pia kama alikuwa “nabii yule,” ambayo yaweza kumaanisha “Nabii” aliyetajwa katika Kumbukumbu la Torati 18:15. Yohana alielezea kwamba hakuwa yeyote kati ya hawa lakini kwamba alikuwa nabii ambaye Isaya alisema angeandaa njia kwa ujio wa Bwana (ona Isaya 40:3).

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Elia.”

Picha
ikoni yakujifunza kwa familia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Picha
msichana akisoma maandiko

Tunaposoma maandiko, tutapokea mwongozo kwa ajili ya maisha yetu.

Yohana 1:4–10

Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia familia yako kupata taswira ya wanachosoma kuhusu nuru katika mistari hii? Ungeweza kuwafanya wanafamilia kupeana zamu kumulika nuru katika chumba chenye giza na kushiriki jinsi Mwokozi alivyo Nuru ya maisha yao. Kisha, unaposoma John 1:4–10, wanafamilia wanaweza kuwa na umaizi wa ziada kwenye ushuhuda wa Yohana juu ya Yesu Kristo, Nuru ya Ulimwengu.

Yohana 1:35–46

Angalia ushuhuda wa Yohana Mbatizaji katika mstari wa 36. Nini yalikuwa matokeo ya ushuhuda wake? (Ona mistari 35–46). Familia yako inajifunza nini kutoka kwa watu walioelezewa katika mistari hii kuhusu jinsi ya kushiriki injili?

Yohana 1:45–51

Ni nini Nathanaeli alifanya kilichomsaidia kupata ushuhuda wa Mwokozi? Tumepataje shuhuda zetu?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shiriki masomo ya vitendo. Waalike wanafamilia kutafuta vitu ambavyo wanaweza kutumia kuwasaidia kuelewa kanuni zinazopatikana katika maandiko mnayosoma kama familia. Kwa mfano, wanaweza kutumia mshumaa kuwakilisha Nuru ya Kristo (ona Yohana 1:4).

Picha
Yesu Kristo akiumba dunia.

Yehova Anaumba Dunia, na Walter Rane

Chapisha