“Mei 13–19 Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: ‘Nimepungukiwa na Nini?’“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Mei 13–19 Mathayo 19–20; Marko 10 ; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili 2019
Mei 13–19
Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18
Nimepungukiwa na Nini?
Unapojifunza Mathayo 19–20; Marko 10; na Luka 18, Kwa maombi fikiria nini washiriki wa darasa wameweza kujifunza au kuhisi katika mafundisho yao wenyewe.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Inaweza kuwa msaada mara chache kujadili uzoefu wa washiriki wa darasa unaohusiana na ongezeko la mwaka huu la msisitizo kuwa nyumbani kuwe kituo cha kujifunza injili. Ni uzoefu gani wa mafanikio wanaweza kushiriki? Ni vikwazo gani au changamoto wanazokabiliana nazo? Ni ushauri gani wanaweza kutoa?
Fundisha Mafundisho
Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.
-
Kwa kuongezeka, mitazamo ya dunia juu ya ndoa imechepuka kutoka kwenye ukweli wa milele. Kusaidia darasa lako lijifunze kuhusu mtazamo wa Mungu kuhusu ndoa, unaweza kuwaalika wasome Mathayo 19:3–9 na waorodheshe ubaoni ukweli wanaoupata kuhusiana na ndoa. Wanaweza pia kuorodhesha kweli za ziada wanazopata katika yafuatayo: Mwanzo 1:27–28; 1 Wakorintho 11:11, Mafundisho na Maagano 42:22; 49:15:17; 131:1–4; 132:19; na Musa 3:18, 21–24. Jinsi gani kweli hizi zimeongezwa nguvu katika “Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu”? (Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129).
-
Je, unaweza kuwasaidia vipi washiriki wa darasa kuhisi wamejiandaa vyema kuelezea au kutetea mafundusho ya Mungu juu ya ndoa? Unaweza kuwataka waorodheshe ubaoni baadhi ya maswali waliyoyasikia kuhusu mafundisho ya Kanisa kuhusiana na ndoa. Kisha wanaweza kupendekeza majibu kwa maswali haya wakitumia kile wanachokijua kuhusu mpango wa wokovu na maelezo kutoka “Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu.” Mathayo 19:3–9, na mafundisho katika “Nyenzo za Ziada.” Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuigiza jinsi wanavyoweza kuelezea imani zetu kuhusu ndoa kwa mtu fulani anayeamini kitofauti.
-
Fikiria kuanzisha mada ya ndoa kwa dondoo zifuatazo kutoka Mzee Robert D Hales: “Hakuna kati yetu anaoa ukamilifu; tunaoa uwezo wa kuwa” (“Kukabiliana na Changamoto za Ulimwengu wa Leo.” Ensign au Liahona, Nov. 2015 46). Waalike washiriki wa darasa wafikirie kuhusu wanandoa ambao wanawavutia. Ni sifa gani wanandoa hawa wanazo? Ni sifa gani washiriki wa darasa watazitaka kwa mume au mke, na sifa gani wanazozitaka kuzijenga ili kwamba wawe mume na mke mzuri? Pia fikiria kauli gani ungeweza kutumia kutoka kwa Rais Russell M. Nelson “Ndoa ya Selestia” (Ensign au Liahona, Nov. 2008, 92–95) kusaidia kuwahimiza washiriki wa darasa kutafuta ndoa ya Selestia.
Uzima wa milele unapatikana kwa wote—haijalishi ni mapema jinsi gani au tumechelewa kiasi gani kukubali injili.
-
Nini kingewasaidia washiriki wa darasa lako kutumia kanuni katika fumbo la wafanyakazi katika shamba la mizabibu? Unaweza kuwaalika washiriki wachache kujiandaa kuigiza fumbo kwa maonyesho darasani. Baada ya wasilisho, watu walioigiza kama wafanyakazi wangeweza kushiriki jinsi walivyojisikia kuhusu malipo waliyopokea na kwa nini. Je, fumbo hili linaashiria nini kuhusu ufalme wa mbinguni? Ni umaizi gani wa ziada washiriki wa darasa wanapata kuhusu fumbo hili kutoka ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Wafanyakazi katika Shamba la Mizabibu.” (Ensign au Liahona, Mei 2012, 31–33).
Matayo 19:16–22; Marko 10:17–27
Mwokozi atatuongoza karibu Naye tunapoomba msaada Wake.
-
Je, unaweza kuwasaidia vipi washiriki wa darasa lako kutambua na kutumia kanuni katika hadithi ya kijana tajiri? Njia mojawapo inaweza kuwa ni kuwaomba wasome Marko 10:17–27 na kufikiria kama wakati wowote wamewahi kuhisi kama kijana tajiri. Ni nini kilichowasaidia kufuata ushauri wa Mwokozi hata wakati ni vigumu? Kuna yeyote darasani anayeweza kushiriki uzoefu ambao aliuliza, “Mimi nimepungukiwa nini? (Mathayo 19:20) na alipokea ushawishi wa kibinafsi kujiendeleza? Ilileta tofauti gani katika maisha yake?
Tunapaswa kuamini rehema za Mungu, sio kwa haki zetu wenyewe.
-
Fumbo la Mwokozi la kufananisha sala ya Mfarisayo na ya mtoza ushuru linaweza kukusaidia kusisitiza mtazamo ambao Bwana anawaomba wale wanaotafuta kumfuata Yeye. Kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia fumbo hili siku yetu, unaweza kuwaomba waandike upya sala ya Mfarisayo katika njia ambayo inatumia kueleza kila kitu kisasa bali inaeleza wazi msimamo ule ule. Kama utafanya hivyo hivyo kwa sala ya mtonza ushuru na kisha uwaombe washiriki kile walichoandika. Jinsi gani aya 15–17 na 18–24 zinahusika na kile Mwokozi alichofundisha katika fumbo hili?
-
Aya hizi zinaweza kuwahimiza vipi wale unaowafundisha kubaki wanyenyekevu, kama alivyokuwa mtoza ushuru? Labda maelezo yafuatayo kuhusu aya hizi ya Mzee Dale G. Renlund yangeweza kusaidia: “Ujumbe kwa ajili yetu ni wazi: mwenye dhambi anayetubu husogea karibu na Mungu kuliko afanyavyo mtu ajionaye mwenye haki ambaye anamlaani yule mwenye dhambi”(“Our Good Shepherd.” Ensign au Liahona, Mei 2017, 31).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuhimiza darasa lako kujifunza Mathayo 21–23; Marko 11–12; Luka 19–20; na Yohana 12, fikiria kuwauliza, “Ungefanya nini kama ungekuwa na wiki moja tu ya kuishi?” Waambie kwamba sura hizi zinaonyesha kile Mwokozi alifanya katika wiki ya mwisho ya maisha Yake.
Nyenzo za Ziada
Ndoa ni kitovu kwenye mpango wa Mungu.
Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walitoa kauli hii kuhusiana na ndoa ya jinsia moja:
“Tunawahimiza wote kuzingatia azma za Baba wa Mbinguni katika kuumba dunia na kuandaa kuzaliwa kwetu kwa maisha ya kufa na kupata uzoefu hapa kama watoto Wake [ona Kutoka 1:27–28; 2:24] Ndoa kati ya mume na mke ilianzishwa na Mungu na ni kitovu kwenye mpango Wake kwa ajili ya watoto wake na kwa ustawi wa jamii. …
“… Mungu anatutegemea sisi kutetea na kutii amri Zake bila kujali mawazo yanayotofautiana au mienendo ya kijamii. Sheria yake ya usafi wa mwili iko wazi: mahusiano ya kijinsia ni sawa tu kati ya mwanamume na mwanamke ambao kihalali na kisheria wameunganishwa kama mume na mke” (“LDS Church Instructs Leaders Regarding Same -Sex Marriage.” Jan. 10, 2014, mormonnewsroom.org)
Umaizi wa ziada juu ya ndoa.
“Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu” inaweza kuwa msaada katika kujadiliana kwa nini manabii wa Bwana wanaonya dhidi ya chochote ambacho ni kinyume na ndoa kati ya mwanaume na mwanamke. Vipengele vifuatavyo vinaweza pia kuwa msaada:
-
Familia ni dhana ya milele. Sisi wote ni sehemu ya familia ya Mungu, na mpango Wake ni kwamba wanaume na wanawake waoane na kuunganishwa ili kwamba waweze kuishi kama familia milele na milele (ona Kutoka 2:18, 21–24; 1 Wakorintho 11:11).
-
Kama sehemu ya mpango wa Mungu, waume na wake wameamriwa kuongezeka na kuijaza dunia (ona Kutoka 1:28) na kulea watoto wao katika haki.
-
Hatima ya azma ya mpango wa Mungu ni kuinuliwa, au uzima wa milele, katika uwepo wa Mungu, ambako waume na wake waaminifu wanaweza kupata ongezeko la milele na furaha ya milele (ona M&M 132:19–21) Mpango wa Mungu ni njia pekee ya kufanikisha kuinuliwa (ona M&M 131:1–4).
-
Bwana anatutegemea kuonyesha upendo na huruma kwa wale wanaotetea au kushiriki katika kitu fulani zaidi ya mpango wa ndoa, kama vile kukaa kinyumba au ndoa ya jinsia moja (ona mormonandgay.lds.org). Huruma ya kweli inajumuisha kufanya kwa uwezo wetu kwa upendo na kwa subira kuwataka wafuate mpango wa Mungu, ambao ni mpango pekee wa furaha ya kweli. Kukumbatia au kuidhinisha mipango mbadala na mpango wa Mungu kunadhuru zaidi kuliko kunavyosaidia.