Njoo, Unifuate
Mei 20–26 Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja’


“Mei 20–26. Mathayo 21–23: Marko 11: Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja” Njoo, unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

mtu juu ya mti wakati Yesu anakaribia

Zakaria juu ya Mti wa Mkuyu, na James Tissot

Mei 20-26

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

“Tazama, Mfalme Wako Anakuja”

Unaposoma Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; na Yohana 12, fikiria kuhusu maswali unayoweza kuuliza ambayo yatasaidia kukidhi mahitaji ya washiriki wa darasa lako. Roho Mtakatifu atakupa mwongozo kujua maswali na kanuni gani, ikijumuisha zile zilizotajwa katika muhtasari huu, zitakazokidhi vyema mahitaji hayo.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Wakati wa wiki kabla ya darasa, waalike washiriki wa darasa wachache kuwa wamejiandaa pamoja na kujifunza wiki hii sura walizopangiwa. Ni baraka gani zinakuja kwao wanapojifunza maandiko wakati wa wiki?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Luka 19:1–10

Mwokozi anatujua sisi kibinafsi.

  • Washiriki wako wa darasa wameelekea kujiona kutotiwa maanani au kusahaulika wakati mwingine katika maisha yao. Maelezo ya Zakaria yanaweza kuwasaidia kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawajua na kuwajali. Kuwasaidia washiriki wa darasa kufananisha maelezo haya na maisha yao, waalike kujifikiria wenyewe kama Zakaria. Unafikiri alijifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwa uzoefu huu? Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa juhudi za Zakaria kuhusu kumtafuta Mwokozi?

  • Inaweza pia kusaidia kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria mifano mingine katika maandiko ambako Bwana aliwaita watu kwa majina. (Baadhi ya mifano imetolewa katika “Nyenzo za Ziada.”) Unaweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki uzoefu ambao umethibitisha kwao kwamba Bwana anawajua kibinafsi.

Mathayo 21:1–11; Marko11:1–11; Luka 19:29–44; Yohana12:12–16

Yesu Kristo ni Mfalme wetu.

  • Shughuli rahisi inaweza kuanzisha majadiliano kuhusu kuingia kwa shangwe ya ushindi kwa Mwokozi Yerusalemu: washiriki kadhaa wa darasa wanaweza kuchora ubaoni vitu vinavyohusikana na mfalme, kama vile taji, au kiti cha enzi, wakati wengine wakisie nini wanachochora. Kisha washiriki wengine wa darasa wanaweza kuchora mwanapunda na matawi ya mti. Vitu hivi vinahusika vipi na mfalme? Unaweza kisha kuonyesha picha ya kuingia kwa Mwokozi kwa shangwe ya ushindi Yerusalemu kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na waalike washiriki wa darasa kusoma Marko 11:1–11. Watu hawa waliwezaje kumtambua Yesu kama Mfalme wao? Tunamwabudu vipi Yesu Kristo kama Mfalme wetu kupitia kwa maneno yetu na vitendo?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba Yesu Kristo ni Mfalme wetu, unaweza kuwaomba warejee wimbo “Come, O Thou King of Kings,” Nyimbo na. 59, au wimbo mwingine kuhusu Yesu kama mfalme wetu. Mathayo 21 :1–11; Marko 11:1–11; Luka 19:29–44; na Yohana 12:12–16?

Mathayo 23:34–40

Amri mbili kuu ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine kama tunavyojipenda.

  • Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha kwamba kando na zile amri mbili kuu kufanya vitu vingine zaidi ya kitovu cha maisha yetu ni kama kupiga mishale kwenye ukuta mtupu na kuchora dango kuzunguka mishale (ona “Kulenga Dango.” Ensign au Liahona, Jan. 2017, 4-5). Kuchambua analojia hii kutawasaidia washiriki wa darasa kuelewa Mathayo 22:34–40? Njia mojawapo ya kufanya hivi ingekuwa kutandaza shiti kubwa ya karatasi kwenye sakafu na kuwaruhusu washiriki wa darasa kwa zamu kudondosha peni au penseli juu yake. Kisha wangeweza kuchora dango pale peni zao au penseli zilipogonga karatasi na kuweka alama kila dango pamoja na amri. Baada ya kusoma Mathayo 22:34–40 pamoja, ungeweza kuchora dango jipya ambalo linazingira dango zingine zote na kuliweka alama “Mpende Mungu na Mpende Jirani Yako.” Kulenga amri kuu mbili kunatusaidia vipi kutii amri zingine za Mungu? Tunawezaje kuwa na uhakika tunalenga utii wetu kwenye amri hizi mbili?

Mathayo 23:13–33

Tutalindwa tunapoepuka kufuata viongozi vipofu.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kufaidika kwa kujadili istilahi “viongozi vipofu” ambayo Mwokozi alilitumia kuelezea Mafarisayo na waandishi waliokuwa vipofu kiroho? Mathayo 23:16. Ungeweza kufikiria njia ya kuonyesha ingekuwa namna gani kwa mtu fulani kumfuata mtu asiyeona. Au darasa lingeorodhesha ubaoni tabia za kiongozi kipofu, kama ilivyoelezwa katika Mathayo 23:13–33. Kuongeza kwenye orodha, zingatia kutafuta maandiko ya ziada ambayo yanafundisha kuhusu upofu wa kiroho, kama vile 2 Wakorintho 4:3–4; 2 Nefi 9:28–32; na Yakobo 4:14. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutambua na kuepukana na viongozi vipofu?

  • Unaweza kutaka kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba waandishi na Mafarisayo walilenga zaidi kwenye dhahabu na zawadi hekaluni kuliko maana ya kweli ya hekalu (ona Mathayo 23:16–22). Kufanya hivi, fikiria kushiriki fumbo la lulu na sanduku la Rais Boyd K. Packer katika “Nyenzo za Ziada.” Nini kinachoweza kutuvutia sisi kutoka kufurahia baraka za kweli za hekaluni? za mkutano wa sakramenti?

watu wawili wakisali hekaluni

Mtoza Ushuru Mwenye Toba na Mfarisayo wa Kujifanya Mwenye Haki Hekaluni, na Frank Adams

Yohana 12:42–43

Sifa za watu zinaweza kutuzuia kutokuwa wafuasi jasiri wa Yesu Kristo.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Mwokozi alitabiri kwamba katika siku za mwisho hata wateule hasa watadanganywa (ona Joseph Smith—Mathayo 1:22). Ili kuwapa mwongozo washiriki wa darasa kusoma Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; au Luka 21 wiki ijayo, unaweza kuwaeleza kwamba watapata katika sura hizi kiini cha kuepuka udanganyifu katika siku za mwisho.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–-20; Yohana 12

Baba wa Mbinguni anawajua ninyi binafsi.

Mzee Neal A. Maxwell alitangaza: “Ninashuhudia kwenu kwamba Mungu amewajua ninyi binafsi … kwa muda mrefu, mrefu sana (ona M&M 93:23). Amewapendeni kwa muda mrefu, mrefu sana. Sio tu anajua majina ya nyota zote (ona Zaburi 147:4; Isaya 40:26; Anajua majina yenu na huzuni yenu yote na furaha yenu!” (“Remember How Merciful the Lord Hath Been,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 46).

Mifano ambayo Bwana aliwaita watu kwa jina.

Fumbo la lulu na sanduku.

Rais Boyd K. Packer alishiriki fumbo hili: “Mfanya biashara akitafuta vitu vya thamani hatimaye alipata lulu safi. Alimpata fundi stadi achonge sanduku zuri la vito na kuliwekea kitambaa cha mahameli ndani. Aliweka lulu yake ya thamani kuu kwa maonyesho ili wengine waweze kushiriki hazina yake. Aliwaangalia watu walipokuja kuiangalia. Punde aligeuka kwa huzuni. Ilikuwa ni sanduku walilostaajabia, sio lulu (“The Cloven Tongues of Fire.” Ensign, Mei 2000, 7).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Hauhitaji kushughulikia kila kitu. “Kuna mengi ya kujadili katika kila somo, lakini sio lazima kushughulikia kila kitu katika wakati mmoja darasani ili kugusa moyo wa mtu—mara nyingi kipengele kimoja au viwili vikuu huwa vinatosha. Unapotafakari mahitaji ya wanafunzi, Roho atakusaidia kutambua kanuni, hadithi, au maandiko yapi ambayo hususani yana maana zaidi kwao’ (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7).