Aprili 29–Mei 5 Yohana 7–10 ‘Mimi ni Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)
Aprili 29–Mei 5 Yohana 7–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Aprili 29–Mei 5
Yohana 7–10
“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”
Wewe na washiriki wa darasa lako mtapata umaizi mnaposoma Yohana 7–10 wiki hii. Kumbuka kwamba mawazo katika muhtasari huu yapaswa kuongeza badala ya kubadilisha mvuto unaopata kwa kujifunza maandiko.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Wakumbushe washiriki wa darasa kuhusu umuhimu wa kufanya nyumba zao kuwa kituo cha kujifunza injili. Ni vifungu gani kutoka Yohana 7–10 washiriki wa darasa walivyovijadili na familia zao wiki hii iliyopita? Ni jumbe gani zilikuwa za msaada mkubwa kwao?
Fundisha Mafundisho
Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu.
-
Kote katika Yohana 7–10, Mwokozi alitoa matangazo kadhaa ambayo yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema huduma yake na kusogea karibu na Yeye. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa wasome vifungu vifuatavyo vya maandiko na kushiriki vinafundisha nini kuhusu huduma takatifu ya Mwokozi. Kristo anatimiza wajibu huu kwa jinsi gani katika maisha yetu?
-
Yohana 7:37–39: “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe”
-
Yohana 8:12; 9:4–5: “Nuru ya ulimwengu”
-
Yohana 8:58: “Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko” (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa umaizi kuhusu aya hii)
-
Yohana 9:8–10, 35–38: “Mwana wa Mungu”.
-
Yohana 10:7–9: “Mlango”
-
Yohana 10:11–14: “Mchungaji Mwema”
-
Tunapoishi mafundisho ya Yesu Kristo, tutakuja kujua ni ya kweli.
-
Washiriki wa darasa wataelewa vyema jinsi gani kuishi amri kunajenga ushuhuda kama watafananisha mpangilio huu na njia ya kujifunza ujuzi kupitia uzoefu binafsi. Kwa mfano, ungeweza kuwataka washiriki wa darasa wanaojua kufanya mazingaombwe au kucheza chombo cha muziki kueleza jinsi walivyokuza ujuzi huo. Jinsi gani kufanya mazoezi wao wenyewe kunawafundisha zaidi kuliko kuangalia tu mtu mwingine akifanya ujuzi ule? Kama darasa, jadilini jinsi juhudi zinazohusika katika kujifunza ujuzi zinafanana na mpangilio wa kiroho Mwokozi alielezea katika Yohana 7:14–17. Ni uzoefu gani washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kuhusu kufuata mpangilio huu kupata elimu ya kiroho.
-
Unawezaje kuonyesha kweli zilizofundishwa katika Yohana 7:14–17? Wazo moja ni kuwaomba washiriki wa darasa lako kushiriki uzoefu ambao kwao walipata ushuhuda wa ukweli wa injili kwa kuuishi. Maelezo yaliyotolewa na Dada Bonnie L. Oscarson katika “Nyenzo za Ziada” pia ni mfano mzuri. Wape muda washiriki wa darasa kufikiria kanuni ya injili ambayo wangependa kupata shuhuda zake za nguvu, na kisha wahimize kuweka malengo bayana kuishi kanuni ile kwa ukamilifu zaidi.
Tunapokuja kumjua Yesu Kristo, tunakuja kumjua Baba.
-
Mzee Jeffrey R. Holland aliona: “Baadhi ya watu katika ulimwengu wa kisasa wanateseka kutokana kueleweka visivyo [Mungu Baba]. … Wengi wa kisasa wanasema wanaweza kuhisi wenye raha mikononi mwa Yesu, lakini wana mashaka wakitafakari mkabiliano mgumu wa Mungu” (“The Grandeur of God.” Ensign au Liahona Nov. 2003, 71). Nini maneno ya Mwokozi yanafundisha katika Yohana 8:18–19, 26–29 kuhusu uhusiano kati ya Yeye na Baba Yake? Baada ya kusoma na kujadiliana aya hizi, washiriki wa darasa wangeorodhesha ubaoni baadhi ya vitu Yesu alifanya, alisema, au kufundisha. Tunajifunza nini kuhusu Mungu Baba kutoka vitu hivi?
Huruma ya Mwokozi imetolewa kwa wote wanaotubu.
-
Kwa wale wanaojiona wamelaaniwa kwa sababu ya dhambi zao, hadithi ya Mwokozi akitoa huruma na toba kwa mwanamke aliyeletwa kwa uzinzi inaweza kuwa chanzo cha kutiwa moyo. Au, kama washiriki wa darasa wanahisi kujaribiwa kulaani wengine kwa sababu ya dhambi zao, hadithi hii inaweza kutumika kama onyo. Unaweza kuwaalika wasome Yohana 8:1–11, wakitafuta majibu kwa maswali kama yafuatayo: Hadithi hii inafundisha nini kuhusu huruma ya Mwokozi? Jinsi gani kupokea huruma Yake tunapofanya dhambi kunatusaidia wakati tunahisi kujaribiwa kuwahukumu wengine? (ona Alma 29:9–10). Unaweza pia kuonyesha video ”Go and Sin No More” (LDS.org).
-
Kuwasaidia washiriki wa darasa kupata uhusiano binafsi katika Yohana 8:1–11, fikiria kugawa darasa katika vikundi vitatu—kimoja kulenga kwenye maneno na vitendo vya Mafarisayo, moja kulenga kwenye maneno na vitendo vya Mwokozi, na moja kulenga kwa maneno na vitendo vya mwanamke. Uliza kila kundi litengeneza orodha ya kweli za kiroho wanazojifunza kutokana na kusoma kila sehemu ya maelezo.
-
Wakati mwingine hatufahamu njia ambazo tunawahukumu wengine. Hapa kuna shughuli ya kuwasaidia washiriki wa darasa kushinda mwenendo huu: liombe darasa likusaidie kutengeneza orodha ya njia tunazowahukumu watu (kwa mwonekano wao, tabia zao, walikotoka, na mengine mengi). Wape washiriki wa darasa vipande vya karatasi vilivyokatwa katika umbo la jiwe, na waombe wachague njia ya kuwahukumu wengine ambao wanawaona wana hatia na waandike kwenye jiwe la karatasi. Nini tunajifunza kutoka na maneno ya Mwokozi kwa Mafarisayo katika Yohana 8:1–11? Alika darasa liandike upande mwingine wa karatasi zao za jiwe kitu fulani ambacho kitawakumbusha kutohukumu (labda msemo kutoka Yohana 8).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waombe washiriki wa darasa wafikirie juu ya wakati walipopoteza kitu fulani ambacho kilikuwa cha thamani kwao. Katika maandiko kwa ajili ya somo la wiki ijayo, watajifunza jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanavyohisi kuhusu wale ambao wamepotea.
Nyenzo za Ziada
Kuishi kanuni kunatusaidia kupata ushuhuda wake.
Dada Bonnie L. Oscarson alisema:
“Mwokozi alifundisha, ‘Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kama mimi nanena kwa nafsi yangu tu’ [Yohana 7:17]. Wakati mwingine sisi hujaribu kufanya kinyume. Kwa mfano, tunaweza kuchukua njia hii: Nitafurahia kuishi amri ya zaka, lakini kwanza nahitaji kujua kwamba ni kweli. Labda hata tunaomba ili kupata ushuhuda wa amri ya zaka na kutumaini Bwana atatubariki na ushuhuda huo hata kabla ya kujaza risiti ya zaka. Haifanyi kazi kwa njia hiyo. Bwana anatutarajia kutumia imani. Ni lazima tulipe zaka kamili mfululizo ili kupata ushuhuda wa zaka. …
“Napenda kushiriki mfano wa jinsi kuishi kanuni kunatusaidia kuwa waongofu kwa kanuni hiyo. … Wazazi wangu na walimu wangu kanisani walinisisitizia thamani ya kuchunga mwili wangu kwa heshima, kuwa na akili safi, na zaidi ya yote, kujifunza kuamini katika amri ya Bwana. Nilifanya uamuzi kuepuka hali ambapo nilijua pombe itapatikana na kukaa mbali na tumbaku na madawa ya kulevya. Hii mara nyingi ilimaanisha sikujumuishwa katika sherehe, na nilifanya miadi mara chache. Matumizi ya madawa yaliendelea kuongezeka zaidi na zaidi miongoni mwa vijana, na hatari hazikujulikana kama ilivyo leo. Wengi wa rika langu baadaye waliteseka uharibifu wa kudumu kutoka kwa madawa ya kubadili akili au kupatikana katika ulevi mkubwa. Nilishukuru kwa kufundishwa kuishi Neno la Hekima katika nyumba yetu, na nikapata ushuhuda wa kina wa kanuni hiyo ya injili nilipofanya imani na kuiishi. Hisia nzuri iliyonijia kwa kuishi kanuni ya kweli ya injili ilikuwa Roho wa Roho Mtakatifu ikithibitisha kwamba kanuni ilikuwa ya kweli.” (“Be ye Converted.” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 77)