Aprili 22–28 Mathayo 18; Luka 10: ‘Nifanye Nini Ili Niurithi Uzima Wa Milele?’“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
Aprili 22–28 Mathayo 18; Luka 10 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Aprili 22–28
Mathayo 18; Luka 10
“Nifanye Nini Ili Niurithi Uzima Wa Milele?”
Soma Mathayo 18 na Luka 10, na uandike misukumo yako ya kiroho. Unapopokea misukumo, unaweza kuuliza kama Mzee Richard G. Scott alivyopendekeza, “Kuna chochote zaidi ningetakiwa kujua?” (“To Acquire Spiritual Guidance,” Ensign au Liahona, Nov.2009, 8)
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Sura hizi zina mifano mingi ya mafundisho ya injili ambayo ni tofauti kutoka na kile ulimwengu unatufundisha. Ni kweli gani washiriki wa darasa walizipata katika sura hizi ambazo ni ngumu kwa baadhi ya watu kukubali au kuishi?
Fundisha Mafundisho
Lazima tuwasamehe wengine kama tunataka kupokea msamaha kutoka kwa Bwana.
-
Wakati mmoja au mwingine, sisi wote tunahitaji kumsamehe mtu fulani aliyetukosea. Utawezaje kutumia fumbo la mtumishi asiye na huruma kutia moyo washiriki wa darasa wawe wenye kusamehe zaidi? Labda ungeandika maswali kama yafuatayo ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa kuyatafakari wakati mtu mmoja anasimilia tena fumbo: Mfalme anawakilishwa Nani? Mtumishi asiye na huruma anawakilishwa nani? Deni lake linawakilisha nini? Mfanya kazi wenzake anawakilisha nini? Deni lake linawakilisha nini? Taarifa kuhusu talanta na senti katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kuwapa washiriki wa darasa wazo la jinsi tofauti kubwa madeni mawili katika fumbo yalivyo. Waalike washiriki wa darasa watafakari nini ujumbe wa fumbo linao kwa ajili yao.
-
Ungeweza kuwataka washiriki wa darasa kubuni utohoaji wa fumbo la mtumishi asiye na huruma kwamba linafundisha somo lile lile kuhusu msamaha kwa kutumia hali za kisasa na kwa utondoti. (Fikiria kuwafanya wakanye kazi hii katika vikundi.) Mjadiliane jinsi gani fumbo lilijibu swali la Petro kuhusu ni mara ngapi anatakiwa asamehe.
-
Video “Forgive Every One Their Trespasses: The Parable of the Unmerciful Servant” (LDS.org) ingeweza kusaidia darasa lako kupata taswira ya fumbo. Katika kuongeza kwenye Mathayo 18:35, maandiko yafuatayo yangeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwa nini Bwana anatutaka tumsamehe mtu anaefanya dhambi dhidi yetu: Mathayo 6:12–5; Waefeso 4:32; na Mafundisho na Maagano 64:7–11.
Kupata uzima wa milele, lazima tumpende Mungu na majirani wetu.
-
Hili ni wazo ambalo linaweza kuwapa washiriki wa darasa mtazamo mpya wa fumbo la Msamaria mwema: Waalike waigize kwamba wanapeleleza kesi ya mashambulizi na unyag’anyi barabarani kati ya Yeriko na Yerusalemu. Waombe washiriki wachache wa darasa waje darasani wamejitayarisha kuwawakilisha watu tofauti katika fumbo na kuzungumza kuhusu kuhusika kwao katika kesi. Kwa mfano, kwa nini kuhani na Mlawi hakusimama kumsaidia mtu aliyejeruhiwa? Kwa nini Msamaria alisimama? Mawazo gani mwenye nyumba ya wageni angeongeza? Yule mtu aliyejeruhiwa alihisi vipi kuhusu kila mmoja wao? Hakikisha majadiliano yanawavutia washiriki wa darasa kuwa kama Msamaria mwema na mwenye nyumba ya wageni na kuepuka kuwa kama kuhani na Mlawi. Lini washiriki wa darasa wamejisikia kama “mtu fulani,” ambaye alihitaji msaada wa haraka? Msaada ulikujaje? Ni kwa jinsi gani sisi kama washiriki wa kata tunafanya kazi pamoja kuwasaidia wengine, kama Msamaria mwema na mwenye nyumba ya wageni walivyofanya?
-
Vile vile kufundisha kuhusu nini inamaanisha kumpenda jirani yetu, fumbo la Msamaria mwema lingeweza pia kuashiria uwezo wa Yesu Kristo kutuokoa. (Utondoti kuhusu ufafanuzi huu unaweza kupatikana katika “Nyenzo za Ziada.”) Unaweza kumwalika mshiriki wa darasa kusoma fumbo, akitafuta hili na uwezekano mwingine wa maana za kiishara. Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake tunaposoma fumbo kwa njia hii?
Tunachagua “ile sehemu mzuri” kwa kufanya chaguzi kila siku ambazo zinaelekeza kwenye uzima wa milele.
-
Maisha yamejaa vitu vya maana vya kufanya. Hadithi ya Mariamu na Martha inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria jinsi ya kuchagua “ile sehemu mzuri” (aya 42; ona pia muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Famila). Baada ya kusoma Luka 10:38–42 pamoja, labda ungewauliza washiriki wa darasa jinsi wangeweza kujibu ushauri wa Mwokozi kama wangekuwa katika nafasi ya Martha. Jinsi gani uzoefu huu umeathiri chaguzi zao za baadaye. Je! Tunawezaje kujua vitu gani katika maisha yetu ni vya “lazima”? (Luka 10:42). Jinsi gani ujumbe wa Mzee Dallin H. Oaks “Good, Better, Best” (Ensign au Liahona, Nov. 2007, 104–8) utawasaidia washiriki wa darasa? ’
Himiza Kujifunza Nyumbani
Liambie darasa lako kwamba wanaposoma tangazo la Mwokozi kuhusu uungu Wake katika Yohana 7–10 kwa ajili ya darasa la wiki ijayo, wanaweza kuja kujua kwa uhakika mkubwa kwamba Yeye ndiye Kristo.
Nyenzo za Ziada
Talanta na senti.
Ni vigumu kujua thamani halisi ya kiasi cha fedha iliyotajwa katika fumbo la mtumishi asiye na huruma (ona Mathayo 18:23–35). Hata hivyo, kuna dokezo katika Agano Jipya ambalo linaweza kutusaidia kuelewa tofauti pana kati ya deni la senti 100 na deni la talanta 10,000.
Mtumishi mwenza katika fumbo alidaiwa deni dogo la senti 100. Katika Mathayo 20:2, penny (aina ya kipekee ya neno pence) ujira unaolipwa kwa kazi ya siku moja katika shamba la mizabibu. Kwa hiyo, watumishi wenzake watafanya kazi kwa siku 100 kupata ujira wa senti 100 kulipa deni hili. Lakini kiasi hiki ni kidogo sana unapofananisha na talanta 10,000 deni la mtumishi asiye na huruma. Katika Mathayo 25:14–15, utajiri wote wa mtu—“mali zake”—zina thamini ya talanta nane tuu. Kwa hiyo, itachukuwa utajiri uliolimbikizwa kwa kuunganisha zaidi ya wanaume 1000 kama mtu huyu kulipa deni la mtumishi asiye na huruma.
Deni kubwa mno Yesu Kristo alilipa kwa ajili ya kila mmoja wetu.
Mzee Jeffrey R. Holland alishiriki kile alichojifunza kuhusu fumbo la mtumishi asiye na huruma wakati akihudhuria darasa chuoni:
“[Mwalimu] alitahadharisha kwamba msamaha wa senti 100, ambao sisi wote tulitegemea kutoa na tulikubali kama kiasi cha haki cha fedha, kilikuwa … ni thamani ndogo kuomba kwa kuzingatia talanta 10,000 msamaha Kristo aliotutolea sisi.
“Deni lile la baadaye, deni letu, lilikuwa idadi kubwa sana, [mwalimu] alitukumbusha, takribani lisiloweza kueleweka. Lakini hiyo, alisema, ilikuwa lengo hasa la Mwokozi katika mafundisho haya, sehemu muhimu ya fumbo. Yesu alinuia kwamba wasikilizaji wake wahisi hasa uwezo mdogo wa milele na zawadi ya kina ya huruma yake, msamaha wake, Upatanisho wake
“ … Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nakumbuka kuhisi kitu fulani cha ukubwa wa dhabihu ya Kristo kwa ajili yangu—zawadi inayopakana hadi leo kwa kutoeleweka. Lakini zawadi ambayo ilinifanya mimi, kwa mara ya kwanza, kufikiri kwa dhati haja yangu ya kusamehe watu wengine na kuwa mkarimu daima kuhusu hisia zao na mahitaji yao na hali zao” (“Students Need Teachers to Guide Them” [Church Education System satellite broadcast, Juni 20, 1992).
Ufafanuzi wa Wakristo wa mwanzo wa fumbo la Msamaria mwema.
Zaidi ya karne, Wakristo wamezipata ishara katika fumbo la Msamaria mwema ambazo zinafundisha kuhusu wajibu wa Yesu Kristo kama Mwokozi wetu. Kwa mfano, mtu aliyeanguka miongoni mwa wanya’ganyi anaweza kutuwakilisha sisi wote. Wanyan’ganyi wangewakilisha dhambi na kifo. Msamaria angemwakilisha Mwokozi. Nyumba ya wageni ingewakilisha Kanisa, na ahadi ya Msamaria kurudi ingewakilisha Ujio wa Pili wa Mwokozi. (Ona Yohana W. Welch, “ The Good Samaritan: Forgotten Symbols.” Ensign, Feb. 2007, 40–47.)